Serikali Tanzania yawapa wazalishaji wa saruji siku nane kushusha bei

Sir mgax

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2023
Posts
2,160
Reaction score
3,831
Serikali ya Tanzania imewapa wazalishaji wa saruji muda wa siku nane kuongeza usambazaji na kushusha bei, baada ya mfuko wa saruji wa kilo 50 kufikia hadi shilingi 26,000 pesa za Tanzania sawa na dola 9.8 katika baadhi ya maeneo.

Wizara ya Viwanda na Biashara iliitisha kikao cha dharura na wazalishaji tarehe 18 Agosti, na kuwapa hadi Agosti 28 kuchukua hatua za kukabiliana na upungufu wa saruji na kupunguza bei.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Rajabu Salum, amesema serikali itafuatilia kwa karibu bei na upatikanaji wa saruji kabla ya kuamua iwapo hatua zaidi zitahitajika.

Wazalishaji wamehusisha upungufu wa bidhaa hiyo na hitilafu katika baadhi ya mitambo mikubwa ya uzalishaji wa klinka, ikiwemo kiwanda cha Maweni mkoani Tanga na Dangote. Wasambazaji, kwa upande wao, wametaja kupanda kwa gharama za mafuta na usafirishaji.

Hata hivyo, tofauti kati ya bei ya saruji kutoka kiwandani na ile ya rejareja imeibua maswali kuhusu ongezeko la bei katika mnyororo wa usambazaji.

Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa saruji ilikuwa ikiuzwa kwa wastani wa shilingi 321,251 pesa za Tanzania sawa na dola 121.47 kwa tani kabla ya kodi ya ongezeko la thamani, sawa na takriban shilingi 16,063 kwa mfuko wa kilo 50.

Baraza la Taifa la Ujenzi linasema ongezeko la mahitaji ya ujenzi, gharama za usafirishaji na kuvurugika kwa usambazaji ni miongoni mwa sababu zinazochangia kupanda kwa bei.

Hatua ya serikali inakuja wakati bei ya saruji ikiwa na athari kwa gharama za ujenzi, huku watumiaji na wafanyabiashara wakisubiri kuona iwapo agizo hilo litashusha bei katika siku zijazo. imewapa wazalishaji wa saruji muda wa siku nane kuongeza usambazaji na kushusha bei, baada ya mfuko wa saruji wa kilo 50 kufikia hadi shilingi 26,000 pesa za Tanzania sawa na dola 9.8 katika baadhi ya maeneo.

Wizara ya Viwanda na Biashara iliitisha kikao cha dharura na wazalishaji tarehe 18 Agosti, na kuwapa hadi Agosti 28 kuchukua hatua za kukabiliana na upungufu wa saruji na kupunguza bei.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Rajabu Salum, amesema serikali itafuatilia kwa karibu bei na upatikanaji wa saruji kabla ya kuamua iwapo hatua zaidi zitahitajika.

Wazalishaji wamehusisha upungufu wa bidhaa hiyo na hitilafu katika baadhi ya mitambo mikubwa ya uzalishaji wa klinka, ikiwemo kiwanda cha Maweni mkoani Tanga na Dangote. Wasambazaji, kwa upande wao, wametaja kupanda kwa gharama za mafuta na usafirishaji.

Hata hivyo, tofauti kati ya bei ya saruji kutoka kiwandani na ile ya rejareja imeibua maswali kuhusu ongezeko la bei katika mnyororo wa usambazaji.

Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa saruji ilikuwa ikiuzwa kwa wastani wa shilingi 321,251 pesa za Tanzania sawa na dola 121.47 kwa tani kabla ya kodi ya ongezeko la thamani, sawa na takriban shilingi 16,063 kwa mfuko wa kilo 50.

Baraza la Taifa la Ujenzi linasema ongezeko la mahitaji ya ujenzi, gharama za usafirishaji na kuvurugika kwa usambazaji ni miongoni mwa sababu zinazochangia kupanda kwa bei.

Hatua ya serikali inakuja wakati bei ya saruji ikiwa na athari kwa gharama za ujenzi, huku watumiaji na wafanyabiashara wakisubiri kuona iwapo agizo hilo litashusha bei katika siku zijazo.
 
Hili la Cement inaonekana limegusa miradi yao (MAFISADI) moja kwa moja, ndio sababu wanalivalia njuga bei ipungue, maana hela nyingi za wizi wanazificha kwenye Ujenzi.

Napongeza kwa hatua hii, walau na sisi wananchi wa kipato cha kati tutapata unafuu kwenye miradi yetu.

Tanzania bila Rushwa, haiwezekani.
 
Mimi naona walivyopewa muda wa wiki moja wa kujitadhmini ni sawa kabisa
Wakishindwa kutekeleza Serikali Iruhusu Cement iagizwe kutoka India na China ambapo hadi ifike Nchini bei yake ya reja reja itakuwa takribani shs 16,000 kwa mfuko wa kilo 50.
Kwa kule India kwa mijini mfuko wa cement wanauza kama shs 10,000 za kitanzania na China mfuko ni kama shs 9000 hivi (reja reja)
 
Cartel...price fixing. Awamu hii wafanyabiashara hasa hawa waarabu koko wanaiendesha serikali watakavyo.
Mpaka mzee mzima mwenzangu comment hii
Nimekubali,ni kweli hawa jamaa wanafanya watakalo
Ila huko mbele ya safari watakuja tu kushikana mashati wenyewe

Ova
 
Mimi naona walivyopewa muda wa wiki moja wa kujitadhmini ni sawa kabisa
Wakishindwa kutekeleza Serikali Iruhusu Cement iagizwe kutoka India na China ambapo hadi ifike Nchini bei yake ya reja reja itakuwa takribani shs 16,000 kwa mfuko wa kilo 50.
Kwa kule India kwa mijini mfuko wa cement wanauza kama shs 10,000 za kitanzania na China mfuko ni kama shs 9000 hivi (reja reja)
Unazani itawezekana?
 
Back
Top Bottom