Jirushe
Member
- Apr 1, 2010
- 8
- 0
Ndugu wana JF.
Nnimekaa na kutafakali kuhusiana na hoja ya kuwa na Serikali tatu nimeona ni kama haiwezekani kwa sababu zifuatazo:-
1. Kuhudumia Serikali tatu itakuwa ni mzigo sana na haitaleta tija katika Taifa hususani katika kuhudumia Marais wastaafu,Mawaziri wakuu wastaafu na Makamu wa Rais wastaafu.
2. Kuhudumia marais wote kwa kuwapa haki zote za Urais ( Presidential Prevarreges), ni gharama kubwa mno hatutaweza
3. Idadi ya Watanzania Bara ni zaidi ya milioni arobaini, na Zanzibar wako chini ya milioni tano na kama watazidi hawatazidi milioni tano. Je kwa uwiano huu, Zanzibar watachangia kiasi gani ghalama za uendeshaji wa Serikali ya Muungano? Hapa tu pananipa maswali makubwa sana, tukikubali hoja hii ipo siku Wazanzibar watashindwa kuchangia gharama za kuendeshea Muungano na wataomba kujitoa, na ndio utakuwa mwisho wa Muungano, na hili halitazidi miaka mitatu au mitano muungano utakuwa umekufa. Hivyo basi sidhani kama ni wazo sahihi la watanzania kudai Serikali tatu kwa sasa na sioni sababu, sidhani hata kidogo.
WAZO LANGU:
Mimi nadhani dunia ingetuelewa saana kama tungekuwa na wazo la kuunda Serikali moja yenye majimbo mawili (Proviencies) kama ilivyo Marekani. Tukawa na Governors wawili yaani Bar na visiwani kama ilivyo Calfonia Provience, Florida Provience n.k. hizi si nchi ingawaje kila moja ina mfumo wake wa kiutawala na sera tofauti kulingana Geographical situations and needs, lakini kiongozi wao mkuu ni USA chini ya Barrack Obama. Labda na sisi tungekuwa na wazo kama hili dunia ingetuelewa kulikoni kurudi nyuma.
Ushauli wangu:
Naiomba Serikali au Bunge la Katiba, kuruhusu kura za maoni ili tupige kura za "NDIYO" au "HAPA" kwa nchi nzima ili tubaini, je ni kweli watanzania wameamua Serikali tatu?
Naomba tujadili
Ibrahim mwakyusa
:amen: