Serikali tatu haiwezekani Tanzania

Serikali tatu haiwezekani Tanzania

Jirushe

Member
Joined
Apr 1, 2010
Posts
8
Reaction score
0
Ndugu wana JF.

Nnimekaa na kutafakali kuhusiana na hoja ya kuwa na Serikali tatu nimeona ni kama haiwezekani kwa sababu zifuatazo:-

1. Kuhudumia Serikali tatu itakuwa ni mzigo sana na haitaleta tija katika Taifa hususani katika kuhudumia Marais wastaafu,Mawaziri wakuu wastaafu na Makamu wa Rais wastaafu.

2. Kuhudumia marais wote kwa kuwapa haki zote za Urais ( Presidential Prevarreges), ni gharama kubwa mno hatutaweza

3. Idadi ya Watanzania Bara ni zaidi ya milioni arobaini, na Zanzibar wako chini ya milioni tano na kama watazidi hawatazidi milioni tano. Je kwa uwiano huu, Zanzibar watachangia kiasi gani ghalama za uendeshaji wa Serikali ya Muungano? Hapa tu pananipa maswali makubwa sana, tukikubali hoja hii ipo siku Wazanzibar watashindwa kuchangia gharama za kuendeshea Muungano na wataomba kujitoa, na ndio utakuwa mwisho wa Muungano, na hili halitazidi miaka mitatu au mitano muungano utakuwa umekufa. Hivyo basi sidhani kama ni wazo sahihi la watanzania kudai Serikali tatu kwa sasa na sioni sababu, sidhani hata kidogo.

WAZO LANGU:

Mimi nadhani dunia ingetuelewa saana kama tungekuwa na wazo la kuunda Serikali moja yenye majimbo mawili (Proviencies) kama ilivyo Marekani. Tukawa na Governors wawili yaani Bar na visiwani kama ilivyo Calfonia Provience, Florida Provience n.k. hizi si nchi ingawaje kila moja ina mfumo wake wa kiutawala na sera tofauti kulingana Geographical situations and needs, lakini kiongozi wao mkuu ni USA chini ya Barrack Obama. Labda na sisi tungekuwa na wazo kama hili dunia ingetuelewa kulikoni kurudi nyuma.

Ushauli wangu:

Naiomba Serikali au Bunge la Katiba, kuruhusu kura za maoni ili tupige kura za "NDIYO" au "HAPA" kwa nchi nzima ili tubaini, je ni kweli watanzania wameamua Serikali tatu?

Naomba tujadili

Ibrahim mwakyusa
:amen:
 
Wewe ni wa Kupuuzwa na kuonewa Huruma
Sasa hayo Majimbo si ndo Tanganyika na Zanzibar na Gavana.
Issue sio Rais wa Tanganyika /Zanzibar
Au jina Rais linakuchanganya.
Hata TFF wana Rais, Akudo wana Rais and the list goes on.
Unaposema Zanzibar watashindwa kuchangia una maana gani?
Kuwa zanzibar sasa tunawabeba ?
Next time uki post tumia akili
 
Ndugu wana JF.

Nnimekaa na kutafakali kuhusiana na hoja ya kuwa na Serikali tatu nimeona ni kama haiwezekani kwa sababu zifuatazo:-

1. Kuhudumia Serikali tatu itakuwa ni mzigo sana na haitaleta tija katika Taifa hususani katika kuhudumia Marais wastaafu,Mawaziri wakuu wastaafu na Makamu wa Rais wastaafu.

2. Kuhudumia marais wote kwa kuwapa haki zote za Urais ( Presidential Prevarreges), ni gharama kubwa mno hatutaweza

3. Idadi ya Watanzania Bara ni zaidi ya milioni arobaini, na Zanzibar wako chini ya milioni tano na kama watazidi hawatazidi milioni tano. Je kwa uwiano huu, Zanzibar watachangia kiasi gani ghalama za uendeshaji wa Serikali ya Muungano? Hapa tu pananipa maswali makubwa sana, tukikubali hoja hii ipo siku Wazanzibar watashindwa kuchangia gharama za kuendeshea Muungano na wataomba kujitoa, na ndio utakuwa mwisho wa Muungano, na hili halitazidi miaka mitatu au mitano muungano utakuwa umekufa. Hivyo basi sidhani kama ni wazo sahihi la watanzania kudai Serikali tatu kwa sasa na sioni sababu, sidhani hata kidogo.
......Ibrahim mwakyusa
:amen:
Sababu ulizotoa hazina mashiko, Hayo ya gharama ni propaganda tu. Nchi hii ina hela Ibarahim!!!! hayo ya gharama ni propaganda za wasaka vyeo. Mbona Zanzibar wana Rais, na hatujasikia wakisema kuhusu hilo la gharama ila sisi Tanganyika tukidai Tanganyka irudi, eti gharama zitakuwa juu.
Mkataa kwao ni mtumwa
 
Tume ilibaini serikali tatu ni gharama nafuu kuzihudumia kuliko ilivyo sasa kwa serikali mbili, pia ilipendekeza jina Rais litumike kwa kipngozi wa serikali kuu na wengine watafutiwe majina mengine. Hata hivyo mimi wazo langu linabaki pale pale.Muungano wa kweli ni serikali moja tu kinyume na hapo tunasogeza mbele time bomb.
 
hawatakubali serikali moja!!! Wazanzibar. Jaribu hilo uone matusi kutokA Zenj
Tume ilibaini serikali tatu ni gharama nafuu kuzihudumia kuliko ilivyo sasa kwa serikali mbili, pia ilipendekeza jina Rais litumike kwa kipngozi wa serikali kuu na wengine watafutiwe majina mengine. Hata hivyo mimi wazo langu linabaki pale pale.Muungano wa kweli ni serikali moja tu kinyume na hapo tunasogeza mbele time bomb.
 
haha hawa ni vibaraka wa ccm kiroba vimeshawamaliza maskini
 
Zanzibr haimezeki hata nyerere imemshinda,kwanza wameshachoka kutawaliwa na mkoloni kanisa kupitia muungano,ningewaona wa maana sana watanganyika kama mngekuwa mnapanga kwenda kuungana na malawi au msumbiji na sio kuendelea na mawazo ya kuitawala zanzbar,zanzibr kwanza.
 
Zanzbar hawataki serikali mbili wala moja. By the way,zanzbar wana rais wao,nyimbo ya taifa,bendera nk,sasa tanganyika nayo kudai uhuru wake ndio ionekane mara gharama,mara marais wengi,mara muungano utavunjika...mawazo ya ki nafki kabisa na hayana mashiko!
 
Basi kwa miaka 50 zanzibar wamekuwa na serikali yao. Kama haiwezekani serikali 3, Nashauri Tanganyika nayo ifufuker nayo iwe active for 50years na halafu tuwe na Muungano, serikali ya Tanganyika na Tanzania Visiwani. kama ilivyo sasa Muungano, Serikali ya ZANZIBAR na Tanzania bara.
 
Back
Top Bottom