Serikali Tatu ni Gharama- Sadifa

Serikali Tatu ni Gharama- Sadifa

Head teacher

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2012
Posts
1,796
Reaction score
412
Mwenyekiti wa UVCCM taifa, amesema serikali tatu hazitekelezi kwa kuwa zina gharama na zitavunja muungano. Amependekeza muundo wa serikali mbili uliopo uendelee.

My take:
1.Kwa nini tung'ang'anie serikali mbili ambazo zimeivunja serikali ya Tanganyika.
2. Kama tupo fair, kwa nini tusiwe na serikali moja ambayo itaimarisha muungano na una gharama nafuu kuiendesha...!
 
Wasiwe vilaza, kung'ang'ania serikali mbili ndiko kutavunja muungano.Wasidhani wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba ni wajinga!
 
Mleta mada, nimependa pendekezo lako la pili, japokuwa lina changamoto zake katika kulifanikisha.

Ila kuhusu serikali ya Tanganyika, kwa tafiti zilizo fanywa, watanzania hawahitaji serikali ya Tanganyika, mambo ya serikali tatu ni kama tunaumega zaidi muungano wetu wa kipekee.
 
Naona Wazenji wameshtuka kuwa kukiwa na serikali tatu itakula kwao sasa wanataka muundo huu uliopo uendelee ila kufanyike marekebisho yatakayowapendelea. Mi naona bora serikali tatu ili kila nchi ijitegemee na hapo ndo tutaheshimiana
 
Ni afadhali gharama nyingi zilizo rasmi, kuliko gharama nyingi zisizoonekana.
Ni heri baba maskini anaehudumia familia ya watu 10, kuliko yule mwenye mtoto mmoja na vimada wa tano.

tragedy of the commons
 
Wasiwe vilaza, kung'ang'ania serikali mbili ndiko kutavunja muungano.Wasidhani wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba ni wajinga!
Pole ndugu, Wazenji si vilaza kama unavyodhani ila wana akili sana!!! Manufaa ya serikali mbili kwa Zanzibar ni kubwa sana kiasi hakuna haja ya wao kutafuta pesa maana asilimia 4.5 ya kila mwezi ni kubwa sana kwao. Wanatupumbaza sie watanganyika. Nadhani Mtanganyika halisi atakataa serikali mbili. Kama wanataka tatu basi na iwe moja tu. Kwa nini tunawabembeleza wakati sie ndio tunaumia?
 
Katika mfumo huu wa sasa, tuna viongozi kama saba hivi amabao tunaweza kuwaita marais ukichanganya na waziri mkuu. Wizara nazo ziko nyingi ambazo zimejaza mawaziri ambao wengine hata kazi zao hazifahamiki vizuri. Sioni kwa vipi serikali 3 zitakuwa gharama kama mfumo huu wa sasa ukivunjwa na kupunguza ukubwa wa serikali.
 
wanashituka saizi wacha zije hizo tatu wajionee wenyewe!
 
Mwenyekiti wa UVCCM taifa, amesema serikali tatu hazitekelezi kwa kuwa zina gharama na zitavunja muungano. Amependekeza muundo wa serikali mbili uliopo uendelee.

My take:
1.Kwa nini tung'ang'anie serikali mbili ambazo zimeivunja serikali ya Tanganyika.
2. Kama tupo fair, kwa nini tusiwe na serikali moja ambayo itaimarisha muungano na una gharama nafuu kuiendesha...!

Serkali tatu si gharama kwa mfano serkali ya Tanganyika inaweza kuwa na Wizara 15 na ile ya muungano inakuwa na wizara 10 au chini.Je ukilinganisha wizara zilizopo sasa na pendokezo langu ni ipi ina gharama?Hii issue ya kuvunja muungano naikubali sana hasa wakiingia wakorofi kama Maalim Seif hivi lakini nani anataka muungano any way?Zanzibar walikwisha vunja muungano wanachotaka sasa ni complete autonomy.Serkali tatu ni bora kwa kuwa moja wapemba hawaitaki.
 
Haya ndo makosa yetu Watanganyika, kwa nini tuangalie wapemba wanataka nini? Achana nao na kama ulivyosema muungano hauna faida ila KARAHA kwa Sie Watanganyika
 
Katika mfumo huu wa sasa, tuna viongozi kama saba hivi amabao tunaweza kuwaita marais ukichanganya na waziri mkuu. Wizara nazo ziko nyingi ambazo zimejaza mawaziri ambao wengine hata kazi zao hazifahamiki vizuri. Sioni kwa vipi serikali 3 zitakuwa gharama kama mfumo huu wa sasa ukivunjwa na kupunguza ukubwa wa serikali.
\
Mzigo tulio nao wa mawaziri na manaibu wao ni zaidi ya serikali tano
 
mimi mpaka leo sielewi hata kwa nini tuna serikali 2 katika nchi moja
 
Serkali tatu si gharama kwa mfano serkali ya Tanganyika inaweza kuwa na Wizara 15 na ile ya muungano inakuwa na wizara 10 au chini.Je ukilinganisha wizara zilizopo sasa na pendokezo langu ni ipi ina gharama?Hii issue ya kuvunja muungano naikubali sana hasa wakiingia wakorofi kama Maalim Seif hivi lakini nani anataka muungano any way?Zanzibar walikwisha vunja muungano wanachotaka sasa ni complete autonomy.Serkali tatu ni bora kwa kuwa moja wapemba hawaitaki.

mimi napendekeza serkali moja kwa kuwa hoja ya kuwa na serkali mbili au tatu haina mshiko ndugu zangu . hii itasaidia kuwafanya watanganyika wasiwe wanyonge mbele ya wazanzibar ambao wanajiamulia mambo yao kupitia baraza la mapinduzi zanzibar, na baraza la wawakilishi vitu ambavyo huku bara hatuna kabisa. sioni sababu ya bara kusacrifice kwa ajili ya huu muungano ilhali wazenji hawako tayari kuiachia serkali yao.
 
Mfumo waserikali mbili unatunyonya watanganyika,na umefuta kbs utaifa! Ni sawa na dagaa kummeza nyangumi. Km hoja ni muungano,mfumo mzuri ni waserikali moja. Mfumo wa serikali tatu ni hatari kwa usalama wetu,kutokana na mahusiano ambayo Z'bar hutaka kushirikiana na nchi za kiarabu ambazo zimewekeza kwny ugaidi. Kuthibitisha hilo mpk sahv Zbar inafuata sheria za kiislam. Wkt wa mfungo wa mwezi wa ramadhani,watu wafungwa jela kwa kosa la kula hadharani,huku katiba haisemi mambo ya kidini. Mfumo shahihi ni serikali moja.
 
Vinchi vidogo hivi! Mkimaliza la muungano karibu la ukabila, udini na ukanda! Dhambi ya ubaguzi ka kula nyama ya nguruwe!
 
Je huyu raisi wa Muungano kama tuna serikali tatu ..atakuwa na mamlaka gani wakati bajeti ya serikali ya Bara ni mara 10 ya serikali ya Muungano?

Angalia huu mfani.

1. Bajeti ya Zanzibar Shs Bilioni 500

2. Bajeti ya Tanganyika Shs Trilioni 16

3. Bajeti ya Muungano Shs Trilioni 02

Je ni nani hapo ana nguvu zaidi??

Je kweli huyu raisi wa Muungano atakuwa na mamlaka gani kwa Raisi wa Tanganyika?
 
Mleta mada, nimependa pendekezo lako la pili, japokuwa lina changamoto zake katika kulifanikisha.

Ila kuhusu serikali ya Tanganyika, kwa tafiti zilizo fanywa, watanzania hawahitaji serikali ya Tanganyika, mambo ya serikali tatu ni kama tunaumega zaidi muungano wetu wa kipekee.
utafiti huo kafanya bbako mbu zi weee acha ujinga dai taifa lako usiwe mamluki kwa buku 7000
 
Back
Top Bottom