Serikali Tatu ni mhimu. Katiba ya Warioba iendelee

Serikali Tatu ni mhimu. Katiba ya Warioba iendelee

Salam zangu ziwafikie Kabudi, Warioba na Polepole.

Sasa nawaelewa rasmi kwamba maoni ya wananchi yalikuwa sahihi.

Muundo wa Serikali tatu Sasa unaanza kuonekana ni mhimu ukawepo. Serikali Moja na hii ya Sasa zinamapungufu mengi.
Ingawa umechelewa lakini sasa hongera kwa kuamka usingizini
 
unaogopa nini ?
RBC ukitaka kuruka sharti uagane na nyonga....

Wanasiasa wanaweza kuwa na mchango mkubwa sana wa kusababisha machafuko...

Tunaona kule Ethiopia....

Tunaona huko Sudan....

Tuliona KATIBA YAO WENYEWE BURUNDI ilivyowaletea shida...Mwenyekiti Hussein Rajab na katibu wake(Rais wa nchi) hayati Pierre Nkurunzinza......

Tumeona katiba ya Afrika Kusini.....

Mwanadamu ni kiumbe asiyetabirika sana.....[emoji1787][emoji1787]

Binafsi ninaipinga katiba ya serikali 3 kwa kuwa tu huko ni FURSA ya kusababisha machafuko......
 
HIzo nchi unazotolea mifano si ndio Nchi alizotaja Trump?
Mkuu kwanini hutaki kujifunza kwa waliofanikiwa?
 
HIzo nchi unazotolea mifano si ndio Nchi alizotaja Trump?
Mkuu kwanini hutaki kujifunza kwa waliofanikiwa?
Waliofanikiwa ni akina nani ?!!

Nchi za ulaya ?!!!

Unataka kufananisha hulka na tabia zetu waafrika na baadhi ya watu wa ulaya ?!!!

Waafrika hatutofautiani sana historia ya nchi zetu ,hulka zetu na tamaduni zetu......
 
Serikali 3 itatuletea "ceremonial president" wa JMT....[emoji1787][emoji1787]
Mkuu huwa Ninapenda kusahau, nikiona macho ya Saa100,ananikumbusha awamu ya pili mwisho “Statement uliyoandika hapa inakuwa Kweli 100%”
 
Wananchi gani ?!!! [emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]

Ile katiba ya Jaji Warioba ilikuwa na "jaggons za kisheria" zaidi ya UHALISIA wa historia ya taifa hili....

Hayati Nyerere aliona mbali zaidi ya aonavyo mh.mzee Warioba.....

Nilifuatilia mchakato wa ile iitwayo "katiba ya wananchi"....utashangaa kabisa....

Mchakato uliporwa na WANASIASA...kila wapitapo....Chadema ,CUF na wenzao walikuwa wanajazana kupata nafasi ya kutoa MAWAZO YAO(makada watupu) [emoji1787][emoji1787]

Kule Zanzibar ndio hatari zaidi....UAMSHO na COMPATRIOT wao waliiteka mikutano ya kukusanya maoni ya wananchi...

Katiba ya "wananchi" chini ya mzee Warioba ilijaa MANYAGO mengi sana.....[emoji1787][emoji1787]
Nonsense
 
Ajabu ni kuwa kila anapokuwa Rais Mzanzibari...baadhi yetu wabara tunataka muungano uvunjike[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

G55 kipindi cha mzee Mwinyi[emoji1787][emoji1787]

Kuna yasiyo na afya kwa taifa nyuma ya "pirika" hizo....
Mwinyi sio mzanzibari
 
Salam zangu ziwafikie Kabudi, Warioba na Polepole.

Sasa nawaelewa rasmi kwamba maoni ya wananchi yalikuwa sahihi.

Muundo wa Serikali tatu Sasa unaanza kuonekana ni mhimu ukawepo. Serikali Moja na hii ya Sasa zinamapungufu mengi.
Nyie wajinga watu wakidai katiba mpya mnasema haileti ugali mezani. Leo ukhanithi umetawala mnajifanya kujiliza. Tunasema kila siku hii katiba ya kumfanya rais Mungu mtu haifai hamsikii, mnaona rais akipunguziwa madaraka ccm itatoka madarakani, maana mnajua CCM iko madarakani kwa nguvu ya mwenyekiti wake kupitia kofia ya urais.
 
Salam zangu ziwafikie Kabudi, Warioba na Polepole.

Sasa nawaelewa rasmi kwamba maoni ya wananchi yalikuwa sahihi.

Muundo wa Serikali tatu Sasa unaanza kuonekana ni mhimu ukawepo. Serikali Moja na hii ya Sasa zinamapungufu mengi.
Huyo Kabudi na Polepole waliikana katiba mpya ili wafaidi ulaji chini ya dhalimu.
 
KATIBA hii iliyopo inamtaka kiongozi mkuu kulinda Nchi na mipaka na kuitetea.

Kuuza bandari zote za bara bila UKOMO ni kuvuka mipaka yake.

Tuzuie mikataba hiyo au tumuondoe madarakani.

Haikubaliki duniani Wala Mbinguni.

ATUPISHE.
 
[emoji1787][emoji1787]

TANGANYIKA iliyokuwepo haikuwa moja....kulikuwa na tawala za kichifu wa makabila....zilikuwa zinatwangana sana tu....kabila moja tu vita vilikuwa haviishi....walikuja kuunganishwa na Vita vya majimaji dhidi ya ukoloni....tena baada ya kung'olewa PAMBA yao.....

Na si makabila yote yalipigana mstari wa mbele na wajerumani....

Mathalani unajua kuwa WAHEHE hawatosahau walichofanyiwa na WANDALI ?!!! [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nikugaie kidogo....shujaa ,El Comandante Mkwawa alishawashinda nguvu wajerumani baada ya kuwachapa kila wakikutana....wajerumani wakapanga vita vikubwa kuliko vyote vilivyowahi kutokea TANGANYIKA....vikosi vyao vikapitia Dodoma....thubutuuu...Makomandante Wagogo wakawaambia hakuna kupita....mkoloni akaufyata....wakarudi nyuma na kutokezea kwa Wanyakyusa....mababu zangu nao wakaligomea LIKOLONI [emoji1787][emoji1787]

Mzungu akachoka mno....akashuka bonde la Usangu....daah [emoji22][emoji22][emoji22]Wandali wakamruhusu apite kuelekea Kalenga......ruhusa hiyo ndio ikawa anguko la mwamba El Comandante Chifu Mkwawa.....hii ilikuwa kachumbari tu....

Nisikilize.....hivi unajua kuwa baadhi ya machifu wa kaskazini walikataa kumuunga mkono hayati baba wa taifa?!!!!

Nje ya Muungano hakuna AMANI hata kidogo......
Sasa hapo mkuu nipe namna muunguno unatusidia kutunza amani na namna unavyozuia UDINI,ukabila na ugaidi

Ila wandali walizingua alafu vip kuhusu wabena mbona baadhi ya watu wanasema wabena ndo waliwapa nguvu ujerumani
 
Back
Top Bottom