Serikali, TFF, Bodi ya Ligi na TAKUKURU; Kwa uhuni huu wa GSM ile "Fair Competition" inayotakiwa na FIFA ipo wapi?

Serikali, TFF, Bodi ya Ligi na TAKUKURU; Kwa uhuni huu wa GSM ile "Fair Competition" inayotakiwa na FIFA ipo wapi?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
GSM ndiyo Wadhamini Wakuu wa Yanga SC ambayo kwa msimu huu wamedhamiria kuchukua Ubingwa wa NBC Premier League kwa Gharama yoyote na kwa Mbinu zote zile za ndani na nje ya Uwanja.

GSM kuona Mipango yao bado haijakaa sawa ili Kuibeba Yanga SC yao sasa wameamua kutumia Mbinu ya Kipumbavu ambayo hata kwa Sheria za FIFA na za FAIR COMPETITION si tu hazikubaliki bali hazitakiwi pia.

GSM sasa tena kwa kufanya Kimya Kimya / kwa Siri wameamua Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu yaani NBC PREMIER LEAGUE ili zikiwa zinacheza na Yanga SC yao ipate Unafuu wa Ushindi ila Vilabu hivyo vikiwa vinacheza na Wapinzani wao wakubwa Simba SC viwe vinaikazia kwa ama Kuifunga au hata tu kutoka nayo Sare.

Kinachonisikitisha zaidi Uhuni na Upumbavu huu usio na Haki katika Ushindani Michezoni unafanywa na GSM halafu Serikali kupitia Wizara ya Michezo imekaa Kimya, TFF na Bodi ya Ligi wamekaa Kimya na Wahusika Wakuu wa Kupambana na Kuzuia Rushwa na Dalili zake zote TAKUKURU wamekaa Kimya.

Akitokea tu Mtu Mmoja au Klabu Moja ikajipanga vyema kwa Sheria na Ushahidi wa Kutosha juu ya Uhuni na Upumbavu huu wa GSM katika Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu kwa nia ya kupata Unafuu ikicheza nazo na akaenda Kushtaki FIFA kuna uwezekano mkubwa NBC Premier League ikaingia matatizoni, Klabu Moja kubwa Kufungiwa, huyu Mdhamini wao Mkuu GSM Kushtakiwa na hata Mpira wa Tanzania Kuharibika rasmi.

Hakuna Mfanyabiashara Mstaarabu na Muungwana Tanzania hii kama Mzee Bakhressa na Kampuni yake ya Azam. Na hakuna pia Kampuni ambayo ni Tajiri Tanzania nzima kama ya Azam.

Azam Wana Timu yao ya Azam FC ila kwa miaka Saba sasa wanapambana Kuwa Mabingwa ila bado hawajafanikiwa. Lakini sijawahi ama Kuona au Kusikia mahala popote pale Azam wakizihonga Timu mbalimbali za Ligi Kuu ya Tanzania ili ziiachie na iwe Bingwa japo ina uwezo wa Kifedha maradufu ya hawa Matapeli wa GSM ila wameamua Kupambana kwa Kucheza tu Uwanjani.

Kama GSM kweli walikuwa na nia ya Kuvidhamini Vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania NBC PREMIER LEAGUE walikuwa wapi Kujitokeza pale TFF na Bodi ya Ligi walipokuwa wanatafuta Wadhamini?

Hivi leo hii Mo Dewji na Kampuni yake / Kampuni zake angeamua nae Kufanya Uhuni na Upumbavu huu usio wa Haki unaofanywa na GSM kwa Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu tena Kisirisiri / Kimya Kimya na kuwaambia wawe wanaikamia tu Yanga SC ila zikiwa zinacheza na Simba SC wawe wanailegezea FAIR COMPETITION ingekuwepo?

Sasa kama unatamba kuwa na Kikosi kizuri na unasema msimu huu Kombe ni lako kwa Soka Kubwa unalocheza kwanini unahangaika Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu kisha unavipa Ahadi ya Tsh Milioni 15 vikiishinda Simba SC na Tsh Milioni 10 vikitoka nayo Sare mpaka unasababisha Wachezaji wa hizo Timu Kuikamia Simba SC, Kuwaumiza kwa Makusudi Wachezaji wake na pale Wakifungwa baada ya Filimbi ya mwisho badala ya kuondoka Uwanjani wanaanza Kuangua Vilio, Kugombana na Kulaumiana mno?

GSM wameshaiharibu Ligi Kuu ya NBC.
 
Simba hamtaki kukubali kama timu yenu ya msimu huu mbovu.

Kwa hiyo timu hazipaswi kuwakazia mkiwa mnacheza nazo mechi.

Jwaneng galaxy tu wamewakazia kidogo taifa wakawapiga 3 pale pale kwa mkapa. Je na hao walizaminiwa na gsm na kupewa hela ndio maana wakawakazia kwa mkapa?
 
Msukule kawapa mbinu ya kuchukua ubingwa
Simba SC wakijipanga vyema kwa Hoja na Ushahidi na kwenda Kushtaki FIFA nakuhakikishia Ndugu Ligi Kuu ya Tanzania NBC inaenda kuingia matatizoni na kuna Balaa Kubwa litatokea katika Soka la Tanzania.

GSM wasidhani Watanzania wote ni Wapumbavu kama walivyowazoea wa Klabu yao ambao wamezoea Kuwahadaa na Kuwadanganya Kutwa huku wakiwadhulumu katika Pesa za Uuzaji wa Jezi zao.
 
Wajinga hawaishi.
Yaah muongeze mleta post kweny list yao.

Kama vilabu vikubwa tu huko Ulaya huwa vinachabangwa na vitimu vidogo tena sometimes vile vilivyopanda daraja maimu huo tu, simba ni timu gani isifungwe?

Analalamikia eti wanakamiwa, sasa waungwana kuna timu inaingia uwanjani ikiwa imejiandaa kufungwa tu kisa inacheza na simba kweli?? Huu upuuzi sijui utaisha lini na hizi timu kubwa 2 kuanza kuheshimu vilabu vingine.
 
Yaah muongeze mleta post kweny list yao.

Kama vilabu vikubwa tu huko Ulaya huwa vinachabangwa na vitimu vidogo tena sometimes vile vilivyopanda daraja maimu huo tu, simba ni timu gani isifungwe??

Analalamikia eti wanakamiwa, sasa waungwana kuna timu inaingia uwanjani ikiwa imejiandaa kufungwa tu kisa inacheza na simba kweli?? Huu upuuzi sijui utaisha lini na hizi timu kubwa 2 kuanza kuheshimu vilabu vingine.
Wana simba wanajua sana simba ya mwaka huu sio simba tena Bali ni nyau kimbulu.matokeo yao niyakuokotaokota tuu.wanatakiwa watulize mshono
 
Mbali na unazi hili jambo litazamwe

IMG-20211104-WA0008.jpg
 
achu uboya kulialia kama mjane subirini dawa iwaingie mlizoea kununua mechi msimu huu azam kagawa hela timu haziuzi tena mechi wanapigania nafasi bora mwisho wa msimu, fly emirates anadhamini timu kibao huko barani ulaya na watu wanapiga mbungi kama kawa, ushauri wangu mwambieni mwamedi atumie mo protekta kudhamini timu zingine ili ziwe zinawaachia mkicheza nazo
 
Kwani GSM mbona mda mrefu alikua akidhhamini vilabu! Msimu uliopita mbona cost alimfunga Yanga, coast si ana dhaminiwa na GSM, Mbumbumbu fc pambaneni na Hali yenu.
Mliambiwa mnasajili magarasa, mpambe wa MO ndugu Magori akasema Simba imesajili wachezaji wa viwango vya juu Sasa mpira ni Mchezo wa wazi endeleeni kudanganyana mkija kustuka mmeshuka daraja.
 
Back
Top Bottom