Serikali, TFF, Bodi ya Ligi na TAKUKURU; Kwa uhuni huu wa GSM ile "Fair Competition" inayotakiwa na FIFA ipo wapi?

Serikali, TFF, Bodi ya Ligi na TAKUKURU; Kwa uhuni huu wa GSM ile "Fair Competition" inayotakiwa na FIFA ipo wapi?

Wambie na Simba ikikutana na "vitimu vidogovidogo" according to you nayo ikaze ili iwapunguze sukari na pressure mashabiki Kama wewe mleta uzi
 
Sportpesa ... Simba, Yanga, Namungo ...
Sportpesa ni kits Sponsor tu lakini

GSM kwenye timu ya Yanga anahusika kwenye management ya Yanga ikiwemo kufanya mchakato wa mabadiliko katika klabu, kufanya usajili na kulipa mishahara.

Mwanzo nilisema GSM wanataka kununua ubingwa kwenye vilabu vidogo kwa mgongo wa udhamini.
 
Sasa ilikuje Coast ambao mdhamini wao GSM alimfunga Yanga katika mechi Muhimu msimu ulio isha,Simba Acheni kulialia hakutawasaidia mmesajili magarasa Sasa pambaneni na Hali yenu.
 
Msimu ulopita mo alizamini namungo mbona hoja kama hizi hamkuleta?
 
Sasa ilikuje Coast ambao mdhamini wao GSM alimfunga Yanga katika mechi Muhimu msimu ulio isha,Simba Acheni kulialia hakutawasaidia mmesajili magarasa Sasa pambaneni na Hali yenu.
Msimu ulopita mo aliizamini namungo na hakukuwa na malalamiko yoyote ila sasa wanaona Yanga iko imara wanatafuta pa kutokea
 
GSM ndiyo Wadhamini Wakuu wa Yanga SC ambayo kwa msimu huu wamedhamiria kuchukua Ubingwa wa NBC Premier League kwa Gharama yoyote na kwa Mbinu zote zile za ndani na nje ya Uwanja.

GSM kuona Mipango yao bado haijakaa sawa ili Kuibeba Yanga SC yao sasa wameamua kutumia Mbinu ya Kipumbavu ambayo hata kwa Sheria za FIFA na za FAIR COMPETITION si tu hazikubaliki bali hazitakiwi pia.

GSM sasa tena kwa kufanya Kimya Kimya / kwa Siri wameamua Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu yaani NBC PREMIER LEAGUE ili zikiwa zinacheza na Yanga SC yao ipate Unafuu wa Ushindi ila Vilabu hivyo vikiwa vinacheza na Wapinzani wao wakubwa Simba SC viwe vinaikazia kwa ama Kuifunga au hata tu kutoka nayo Sare.

Kinachonisikitisha zaidi Uhuni na Upumbavu huu usio na Haki katika Ushindani Michezoni unafanywa na GSM halafu Serikali kupitia Wizara ya Michezo imekaa Kimya, TFF na Bodi ya Ligi wamekaa Kimya na Wahusika Wakuu wa Kupambana na Kuzuia Rushwa na Dalili zake zote TAKUKURU wamekaa Kimya.

Akitokea tu Mtu Mmoja au Klabu Moja ikajipanga vyema kwa Sheria na Ushahidi wa Kutosha juu ya Uhuni na Upumbavu huu wa GSM katika Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu kwa nia ya kupata Unafuu ikicheza nazo na akaenda Kushtaki FIFA kuna uwezekano mkubwa NBC Premier League ikaingia matatizoni, Klabu Moja kubwa Kufungiwa, huyu Mdhamini wao Mkuu GSM Kushtakiwa na hata Mpira wa Tanzania Kuharibika rasmi.

Hakuna Mfanyabiashara Mstaarabu na Muungwana Tanzania hii kama Mzee Bakhressa na Kampuni yake ya Azam. Na hakuna pia Kampuni ambayo ni Tajiri Tanzania nzima kama ya Azam.

Azam Wana Timu yao ya Azam FC ila kwa miaka Saba sasa wanapambana Kuwa Mabingwa ila bado hawajafanikiwa. Lakini sijawahi ama Kuona au Kusikia mahala popote pale Azam wakizihonga Timu mbalimbali za Ligi Kuu ya Tanzania ili ziiachie na iwe Bingwa japo ina uwezo wa Kifedha maradufu ya hawa Matapeli wa GSM ila wameamua Kupambana kwa Kucheza tu Uwanjani.

Kama GSM kweli walikuwa na nia ya Kuvidhamini Vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania NBC PREMIER LEAGUE walikuwa wapi Kujitokeza pale TFF na Bodi ya Ligi walipokuwa wanatafuta Wadhamini?

Hivi leo hii Mo Dewji na Kampuni yake / Kampuni zake angeamua nae Kufanya Uhuni na Upumbavu huu usio wa Haki unaofanywa na GSM kwa Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu tena Kisirisiri / Kimya Kimya na kuwaambia wawe wanaikamia tu Yanga SC ila zikiwa zinacheza na Simba SC wawe wanailegezea FAIR COMPETITION ingekuwepo?

Sasa kama unatamba kuwa na Kikosi kizuri na unasema msimu huu Kombe ni lako kwa Soka Kubwa unalocheza kwanini unahangaika Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu kisha unavipa Ahadi ya Tsh Milioni 15 vikiishinda Simba SC na Tsh Milioni 10 vikitoka nayo Sare mpaka unasababisha Wachezaji wa hizo Timu Kuikamia Simba SC, Kuwaumiza kwa Makusudi Wachezaji wake na pale Wakifungwa baada ya Filimbi ya mwisho badala ya kuondoka Uwanjani wanaanza Kuangua Vilio, Kugombana na Kulaumiana mno?

GSM wameshaiharibu Ligi Kuu ya NBC.
jikaze ww, nani ana muda wa kuhonga hizo team banaaa!!!ww msimu huu team huna ndo maana unalalamikalalamika!!mwamedi alikua anahonga kila mechi now kajiweka pembeni mnalalamika!!makolo banaaa!!ulibwanji makolo
 
Mimi nadhani kama Simba ikicheza kwa ushindani ikashinda mechi zake zote dhidi ya wapinzani wanaohongwa, hii biashara itakufa automatically. Ni kweli timu yetu mwaka huu bado inajitafuta. Lakini je tunataka wapinzani dhaifu ili tuokote pointi? Mimi nasema GSM waendelee kuhonga tena wapandishe dau timu zipate morali zicheze vizuri zije zifungwe zikiwa vizuri bila kisingizio
 
Msimu ulopita mo alizamini namungo mbona hoja kama hizi hamkuleta?
Mo alidhamini Namungo kwa bidhaa gani ?

Kama Mo msimu uliopita alifanya makosa unataka kuhalalisha makosa ya GSM kupitia makosa ya Mo ?

Sisi tunataka fair competition badala hii ya sasa unaenda kununua vilabu karibu vyote vya ligi kuu na vikicheza na hasimu wako unaahidi million 10 ili iweje ?
 
Sportpesa ni kits Sponsor tu lakini

GSM kwenye timu ya Yanga anahusika kwenye management ya Yanga ikiwemo kufanya mchakato wa mabadiliko katika klabu, kufanya usajili na kulipa mishahara.

Mwanzo nilisema GSM wanataka kununua ubingwa kwenye vilabu vidogo kwa mgongo wa udhamini.
vp kuhusu Azam
 
SPPRTPESA INADHAMINI SIMBA, YANGA, NAMUNGO

Msiwe wapumbavu. Wakati ligi haina wadhamini tulikua tunalalamika , timu zinashindwa hata kulipia gest house. Leo wanakuja mnaleta nongwa??
 
NENDA WEWE COASTAL AU YANGA UKAWEKE HELA NYINGI KULIKO GSM ILI GSM ATOKE UDHAMINI WEWE[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Acheni upumbavu nyie Mikia, Azam anadhamini haki za matangazo mbona anatimu? Fly Emirates anadhamini timu ngapi? Sportspesa anadhamini timu mpaka Simba na boss wake ni Tarimba Abass, mwenyekiti wa zamani wa Yanga hilo linaleta mgongano wa maslahi.......acheni kutafuta visababu, tengenezeni timu na hizo propaganda zenu mnapoteza muda tu
 
Tatizo ni njaa kali

TFF njaa
Takukuru njaa
Serikali njaa/Omba omba
Vilabu njaa
Wanasiasa njaa
Marefa njaa
Wachambuzi njaa
Mashabiki njaa

Nchi hii maskini jameni.
Hata mikia njaa maana Sportspesa inawadhamini, na boss wake ni mwenyekiti wa zamani wa Yanga
 
Mimi nadhani kama Simba ikicheza kwa ushindani ikashinda mechi zake zote dhidi ya wapinzani wanaohongwa, hii biashara itakufa automatically. Ni kweli timu yetu mwaka huu bado inajitafuta. Lakini je tunataka wapinzani dhaifu ili tuokote pointi? Mimi nasema GSM waendelee kuhonga tena wapandishe dau timu zipate morali zicheze vizuri zije zifungwe zikiwa vizuri bila kisingizio
Umeongea kwa kutumia akili kubwa sana na kuweka ushabiki wako pembeni.
 
Back
Top Bottom