Serikali toeni haki kwa Kampuni za wazawa watangaze mipira mbali mbali duniani nchini.

realleonia

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2013
Posts
366
Reaction score
138
Serikali ya Naijeria imethubutu kwa kutoa tamko kwamba wanakwenda kutoa ruhusa kwa makampuni ya vizimbuzi nchini humo kuwa na haki ya kumili ki maudhui ya urushaji Epl na Uefa na si DStv pekee Kama ilivyo sasa.Na sisi iwe hivyo tumepigwa vya kutosha jamani .

Sasa hivi DStv wamepunguza Bei baada ya Kampuni ya kifansa (Canal sport)kuingia kimya kimya na kumpa wakati mgumu huyu DStv yapo makampuni mengi yanapenda yarushe mipira bure lakini wanapata upinzani kutoka DStv kwani ndo mwenye haki ukanda huu.Kibaya anacho fanya DStv ni kuzuia Kampuni nyingine kupata haki hiyo muda umefika wa kuwapa haki wazawa.
 
Anayetoa haki ya kuonesha epl siyo serikali ya Tanzania
 
Wewe hujui kuwa kuna vigezo unatakiwa kuwa navyo kuweza kupata leseni ya kuonesha ligi hizo. Kama makampuni mengine hawana hela na idadi kubwa ya watazamaji na coverage hawatakubaliwa.
 
Vigezo ni vigumu kwanza ni lazima coverage yako iwe kubwa kwa maana ulifikie soko lote kwa urahisi na system yako iwe secured na pia quality uwe na channel zote za HD. EPL wanauza bidhaa lakini wanata msambazaji awe na uwezo wa kuifikisha ikiwa bidhaa bora wao wanalinda brand yao na kubwa zaidi mashindano ya kupata haki ni kama mnada mwenye offer kubwa anapewa haki sasa ili ushinde ina maana uwe sub sahara yote uwafikie ndio unaweza kupata faida na changamoto ndio hivyo kuna watu wanaiba signal. nadhani inawezekana ila isio Tz only.
 
Mkumbuke huyo dstv ye mwenyewe ananua hizo right ni hela yako siku hizi kampuni zikiweka bid kubwa kuliko ya dstv watapata tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakuunga mkono kwa 100%. Kumbuka kuna kipindi haki ya kuonesha EPL ilichukuliwa na GTV iliyokuja na malipo ya 46,000/- kwa mwezi tofauti na 133,000/- za DSTV kwa wakati huo. Kwa bahati nzuri kampuni hii iliishia njiani na Watanzania tuliobahatika kupata visimbuzi vyao tukabaki na makopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sawa kabisa
 
Sasa inakuaje serikali ya Naijeria inaingilia Kati na kusema kuwe na haki sawa mbona Kama Kuna kitu ambacho Mimi sikijui kipo chini ya kapeti halafu wenzetu Ulaya hiki kitu kipo free
 
Sasa inakuaje serikali ya Naijeria inaingilia Kati na kusema kuwe na haki sawa mbona Kama Kuna kitu ambacho Mimi sikijui kipo chini ya kapeti halafu wenzetu Ulaya hiki kitu kipo free
Kwanza naomba niweke sawa kidogo hapa, Ulaya hakuna bure ziko kampuni za cable zina haki ya kutangaza na mbaya zaidi mfano England wenyewe hawaoneshi mechi zote na hasa zile za saa 9 mchana na ziko sababu zao. kuna kampuni mbili Sky na BT sports wamepewa haki kama packages na wanalipa pesa nyingi sana. Africa wamegawa Sub Sahara na nchi za north Africa, N.Africa sababu ya lugha ya kiarabu imeunganishwa na M.East ndio utakuta Bein sport kashika soko mpaka nchi kama Sudan. Kuna nchi zinaongea kifaransa wamepewa mwingine. muhimu kuna packages nyingi. Sasa Nigeria wanachosema sio lazima kiwe sawa wao wanadhani wako wengi na soko ni kubwa ikitokea Premier league kutoa package kwa kila nchi washindane watakula hasara ndio maana wamegawa kwa zone. chukulia mfano wametangaza Tanzania tu TV rights katika mnada Azam atashinda kwa bei rahisi sababu hakuna ushindani kama ligi yetu ya bongo. wanatoa kwa sub sahara ili kampuni kubwa zishindane hata hao DSTV wao wananunua kwa sky sports ila labda huko mbeleni wanaweza kugawa haki North, South na west Africa kutegemea na soko mwisho wa siku pesa ina play role. siku wa kigawa hivyo hapo kampuni za Nigeria sijui Ghana watagombea haki. kukiwa na players wengi mnadani chance ni kubwa kuuza haki bei kubwa.
 
Nilikuwa sijui kama azam tv haki ya kuonyesha Laliga wamepewa na serikali

Basi kama ndio hivyo Please serikali ya JPM wapeni azam tv haki ya kuonyesha UEFA na EPL

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…