Serikali: Toeni tamko Land Rover Festival liwe tukio rasmi la kufanywa kila mwaka kama tukio kubwa zaidi la kiutalii kwa Kanda ya Kaskazini

Mkuu ningependa kusikia hoja yako ya kwanini iwekwe kila baada ya miaka mitatu na si kila mwaka. Tafadhali muhenga mwenzangu wa mshahara wa January mnachelewa😁
 
Sio wazo baya, lakini hatuna kiwanda cha kutengeneza Land Rover hapa nchini, sana sana tutakuwa tunatangaza biashara ya watu. Ingekuwa ni product inayotengenezwa hapa nchini hapo sawa.

Inaonekana umehamasika sana na jambo hili hadi umeona serekali itoe tamko, huku ukisahau magari ya Land Rover sio product ya hapa nchini. Kama ni hivyo itabidi kuwe na festival nyingi za magari ya makampuni mengine.
 
Wale watalii walioshiriki jana hujawaona?
Wale hawakuwa watalii bali wazungu wanaoishi humu humu, hasa wengi walitoka Kenya. Ni kweli ni tukio lililoboresha utalii wa ndani. Tatizo langu ni kuwa wenye ubunifu wa hivyo wako wengi, lakini si rahisi kupata ruhusa ya kufanya hivyo kwa milengo ya kisiasa. Unatarajia mtu asiye na madaraka angeweza kupewa nafasi na ushirikiano wa hivyo toka kwenye mamlaka?
 
K

Kwa hiyo kama ninamiliki land rover nahitaji idhini ipi tena?
Kwa hiyo ukinunua chupa mbili za Heineken unaruhusiwa kujianzishia zako Heineken Festival ambapo hapo hapo utakuwa unapromote Safari na Castle Lager?

Ni tukio la watu kuenjoy tu lakini si zaidi ya mnavyotaka liwe.
 


..Sekta binafsi wafanye.

..sio sahihi kutumia KODI za maskini kugharamia tukio hilo.
 
Wale wazungu wachache hata miatano hawafiki ndo wanakuzuzua
Kuna faida nyingi zitokanazo na landrover parade
1. Kuitangaza Arusha/ Tanzania kimataifa kama tukivunja guiness record hivyo kuitangaza na kukuza utalii.
2. Imeongeza mapato ya Arusha na wafanya biashara.
3. Watu wanakutana na kupeana michongo
4. Kukuza utalii wa ndani, maana watalii zaidi ya miasita wameenda mbugani.
5. Pia kama ni mtu unaependa maendeleo hii event inakutia hasira ya kupambana.
 
Kama kilimanjaro marathon imeshindwa kukuza utalii sembuse hiyo festival hata miaka miwili haina
Kumbuka kilimanjaro marathon ina-zaidi ya miaka 10
 
Kama kilimanjaro marathon imeshindwa kukuza utalii sembuse hiyo festival hata miaka miwili haina
Kumbuka kilimanjaro marathon ina-zaidi ya miaka 10
Ni kuweka strategies tu!

Hizi event zikianza kupewa big airtime na kuwa published vizuri nakwambia zinaweza leta karibu milioni 2 kila mwaka kuja kushiriki tu
 
Kama kilimanjaro marathon imeshindwa kukuza utalii sembuse hiyo festival hata miaka miwili haina
Kumbuka kilimanjaro marathon ina-zaidi ya miaka 10
Aisee ndio maana mnaitwa Nyumbu ,hivi Kili marathon huna taarifa kuwa kunakuwepo na washiriki yoka mataifa zaidi 50 kila mwaka
 
Kweli kabisa
 
Naomba kuuliza: hili tamasha ni kwa ajili ya kutangaza utalii Tz au magari ya landrover? Je, kampuni inayotengeneza magari hayo, ambayo ni ya uingereza, imeilipa Tz shilingi ngapi kwa kutangaza bidhaa zake? Na je, baada ya tamasha hili, kutakuwa na tamasha la Toyota na magari aina nyingine? Ingelikuwa ni tamasha la maonesho ya magari aina ya Nyumbu yalokuwa yanatengenezwa kule Ngerengere nisingeuliza maswali haya
 
Ila uwezo wa watanzania ni mdogo yaani serikali imeshindwa kupromote kilimanjaro marathon ili kuvutia watalii ndo sembuse hiyo festival isiyo na kichwa wala miguu sana sana ni kuonyesha ufahari wa watu wachache
Inasikitisha sana
 
Inasikitisha sana
Imagine unawapa free time landrover kuwatangazia bidhaa zao bure
Ndo maana makonda uongozi hawezi sasa akiuliuzwa serekali inapataje hela inapotangaza landrover bure majibu atakua hana

Africa watu weupe wanapata vitu vingi sana bure rasilimali wamechukua bure mda huo huo tunawatangazia brand zao bure kwa nchi maskini kama Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…