Serikali toeni ufafanuzi unaoelewekaa kuhusu kufunga barabara za jiji

Serikali toeni ufafanuzi unaoelewekaa kuhusu kufunga barabara za jiji

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,436
Reaction score
7,955
Polisi mmetoa tangazo la kufunga barabara za mjini sasa swali langu je shughuli za kikazi zitasimama?

kuna Wanafunzi wanasoma mjini huko je na wenyewe waje shule au wakae nyumbani? wekeni wazi utaratibu wenu tujue moja!

suala la kumuachia Murilo pekeyake aongelee suala la ugeni huu anaweza kuleta shida kwa kuwa anaweza kuongelea kipolisi ila akashindwa kujua mambo mengi nje ya kipolisi! watu wa protocol na msemaji wa serikali uje utoe ufafanuzi

NASISITIZA tena je wanafunzi itakuwaje!? ukizingatia akina kayumba wanazagaa sana mjini na misafara kila dakika hamuoni mtagonga watoto wetu!? toeni tamko wapumzike nyumbani hasa wa Primary school.
 
Mliambiwa bajaji na bodaboda zisifike mjini, maana yake usafiri mwingine ruksa
 
Huu ni wendawazimu uliopitiliza. Yani kwakuwa wanakuja wageni basi shughuli za watu wengine zisimame?

Hawa ndio maana wakienda kwenye nchi za wanaojitambua huwa wanawalundika kwenye daladala la pamoja maana hawajitambui.
Bajaji na bodaboda ni vurugu tu
 
Hizo barabara uwepo wake na matumizi yake vinalazimisha watumiaji kulipa Kodi ambayo inatumika kumlipa Muliro na ndugu yake Chalamila. Mbali na usumbufu wanaoupata walipakodi kwenye shughuli zao za kila siku, Bado Kodi itachuliwa tu licha ya kuwa matumizi yanafanywa na wageni watakaokuwepo kwa siku sijui 4+ ....Huu ni wizi wa kitaasisi ambao hautofautiani na ule wa vibaka wanaokwapua simu na kuishia kuchomwa Moto.
Inashangaza sana kuona mji unasafishwa siku wakija wageni... Mbona nchi nyingine zinapokea wageni wengi tu lakini barabara zao hazifungwi? Shughuli za kila siku hazipaswi kusitishwa! Ruhusuni hao wageni waone tunaishi vipi kwa uhalisia wake.....Sijui huu ushamba wa kufagilia wageni utaisha lini? 😡
 
kuna shida sana ya ufikiri katika nchi za afrika.wanaangalia leo sio kesho.
 
Polisi mmetoa tangazo la kufunga barabara za mjini sasa swali langu je shughuli za kikazi zitasimama?

kuna Wanafunzi wanasoma mjini huko je na wenyewe waje shule au wakae nyumbani? wekeni wazi utaratibu wenu tujue moja!

suala la kumuachia Murilo pekeyake aongelee suala la ugeni huu anaweza kuleta shida kwa kuwa anaweza kuongelea kipolisi ila akashindwa kujua mambo mengi nje ya kipolisi! watu wa protocol na msemaji wa serikali uje utoe ufafanuzi
Kumbe kuna haja ya kuwa na usafiri wa treni na barabara za juu ama za kulipia
 
Binafsi nina wasiwasi, sina barabara mbadala zaidi ya walizozikataza.

Yaani wageni waje kutuharibia maisha yetu kweli? Haingii akilini.
Hizo barabara mbadala ziko wapi?
 
Mliambiwa bajaji na bodaboda zisifike mjini, maana yake usafiri mwingine ruksa
Hii ni sawa na una lala kwenye kitanda chenye kunguni halafu akija mgeni unapiga dawa kuwaua kunguni, akiondoka unaendelea na style ile ile ya kuishi na kunguni. Nionavyo mimi aliyeruhusu biashara ya pkpk na bajaj kuingia kati kati ya miji alikosea sana, kungewekwa na utaratibu wafanyie shughuli zao pembezoni ya miji tu ili kuondoa usumbufu na misongamano iyo ya lazima.
 
Si wangepeleka hata huko Arusha mkutano wenyewe
Arusha ndo wangesumbua watu kabisa. Vibarabara vya Arusha ni finyu balaa. Arusha ikifungwa barabara moja tu ni jam ya kutosha hapo mjini kati.

Huu mkutano wangefanyia dodoma uko, si ndo mji wa shughuli za kiserikali. Ila ni basi tu hatuna viongozi wanaowafikiria wananchi wao.
 
Back
Top Bottom