imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Ugonjwa wa ajabu uliosababisha vifo vya watu watano kati ya wanane waliougua wilayani Bukoba Vijijini mkoani Kagera umetambuliwa kuwa ni Marburg. Soma: Ugonjwa wa Virusi vya Marburg: Historia, Uambukizwaji, Dalili na Matibabu
Imesema ugonjwa huo huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 21, 2023 jijini Dar es Salaam.
Waziri Ummy amesema ugonjwa huo hauna tiba mahususi bali hutibiwa kwa dalili husika anazokuwa nazo mtu. “Hadi kufikiwa leo siku tano tangu kuripotiwa ni watu nane ndio wameambukizwa na vifo ni vitano na watatu bado wanaendelea na matibabu,
“Tumefanikiwa kudhibiti ugonjwa huu haujatoka nje ya eneo lililolumbwa na ugonjwa huu,” amesema.
Machi 16, 2023 na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu siku chache baada ya ugonjwa huo kuripotiwa amesema umetokea katika vijiji vya Bulinda na Butayaibega vilivyopo katika kata za Marua Kanyangereko wilayani Bukoba. Leo Profesa Nagu amesema watu hao walipata dalili za homa, kutapika, kutokwa na damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi.
Hivyo ili kudhibiti ugonjwa huo usisambae, amewataka watu kuepuka kumgusa mgonjwa au majimaji ya mwili mfano mate, machozi, damu, mkojo na kinyesi yatokayo kwa mgonjwa ama mtu mwenye dalili hizo.
Amesema iwapo mtu atalazimika kumhudumia mgonjwa kwa dharura, achukue tahadhari ya kujikinga majimaji yoyote kabla ya kumhudumia.
Chanzo: Mwananchi
Ripoti ya kuzuka kwa ugonjwa huo, soma: Kagera kuna hali ya hatari, kumezuka ugonjwa wa kutokwa damu puani na mdomoni. Watu 5 wafariki dunia 2 wako hospitali. Serikali ichukue hatua haraka
===
Nimekuwa nikiangalia Ayo TV Wazili wa Afya anasema Ugonjwa ulioua watu huko Kagera ni Marburg, nimefurahishwa na uwazi sijui ingekuwaje kama gonjwa hili ilingeingia walati wa ile Awamu ya laana?.
Huenda lingeitwa "Changamoto ya kuzimia".
============
UGONJWA WA MARBURG UNAWEZA KUSAMBAA KWA WATU NA WANYAMA
Serikali ya #Tanzania imebainisha ugonjwa ulioibuka Mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu kadhaa, Machi 2023 unaitwa Marburg ambao unasababishwa na Virusi vya Marburg (Marburg Viral Disease).
Unaweza kuambukizwa kwa njia ya kugusa majimaji kama mate, mkojo, damu, machozi au kinyesi yatokayo kwenye maiti au mgonjwa mwenye dalili.
Pia, maambukizi yanaweza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kwa kula au kugusa wanyama walioambukizwa.