Serikali: Usajili wa taasisi ya kidini (FBO) zaweza chukua hata muda wa serikali kukaa madarakani, yaani miaka mitano ndipo isajiliwe

Serikali: Usajili wa taasisi ya kidini (FBO) zaweza chukua hata muda wa serikali kukaa madarakani, yaani miaka mitano ndipo isajiliwe

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2014
Posts
984
Reaction score
1,179
Novemba 2024 ni mwaka mmoja tokea kuanzishwa na kusajili taasisi ya kidini wizara ya mambo ya ndani kitengo cha msajili wa taasisi zisizo za kiserikali.

Leo hii nimefanya followup kutaka kujua nini kinakwamisha taasisi yetu isisajiliwe.

Afisa akajibu kuwa majibu yanapatikana kupitia mfumo wa mtandao. Nimemwambia mfumo unaonyesha uko ktk hatua ya examination na analysis.

Afisa akasema ndio jibu hilo. Nikamuuliza kwahiyo tunapaswa kusubiri kwa muda gani au turidhike tu na kile kinachoonekana kwenye mtamdao hata kama ni uzembe na kutowajibika. Na kwamba tunaweza kusubiri tu hata kwa miaka 5. Afisa akajibu ni kweli tena kwa taasisi za dini tunazichunguza hata kwa miaka 5.

Jibu hili limenitafakarisha sana. Kwani miaka 5 ndio kipimo cha utendaji cha juu cha utendaji wa serikali. Na kwamba uchaguzi waweza kuuangusha serikali iliopo madarakani. Hii ndio kusema taasisi za dini zaweza kuomba usajili kwa serikali ya awamu ya 6. Na taasisi hiyo isisajiliwe hadi itakapoondoka mamlakani kupitia uchaguzi mkuu.

Majibu yasiyo na mantiki zaidi ya kiburi walichojijengea watumishi wa Umma ambao kimsingi nimejiridhisha kuwa ni sehemu ya wahalifu waliojificha nyumba ya taasisi za serikali.

Kama watz, tunahitaji kuondoa ccm madarakani kwa nia ya kutaka kusafisha serikali dhidi ya wahalifu wanaolindwa na mfumo.

Si tu tunapaswa kuliondoa CCM madarakani. Bali lazima tukubaliane tunauondoa na mfumo wa serikali kuu na kupigania kuundwa kwa serikali za majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yake wenyewe
 
Kama watz, tunahitaji kuondoa ccm madarakani kwa nia ya kutaka kusafisha serikali dhidi ya wahalifu wanaolindwa na mfumo.
Tusije tukaiondoa Serikali ya Kisecular halafu ikazaliwa Serikali ya Kidini.
 
Back
Top Bottom