Serikali: Vitambulisho Milioni 1 na nusu na zaidi vya NIDA viko tayari, nendeni mkavichukue

Serikali: Vitambulisho Milioni 1 na nusu na zaidi vya NIDA viko tayari, nendeni mkavichukue

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Utekelezaji wa kampeni hii, kwa sisi hapa Tanzania, tumeamua tuje na kaulimbiu inayosema "Kipo, Kichukue, Kamilisha Safari Yako."

Lengo letu kubwa ni kuwakumbusha wananchi wote waliosajiliwa kwenda kuchukua vitambulisho vyao.

Tunayo changamoto, kama nilivyosema kwenye takwimu, tumesajili Watanzania wengi zaidi ya milioni 27. Vitambulisho zaidi ya milioni 21 viko tayari... lakini vitambulisho milioni moja na nusu na zaidi bado havijachukuliwa, viko kwenye ofisi za NIDA.

Kwahiyo, tunataka tutumie kipindi hiki kuwahamasisha Watanzania ambao wamesajiliwa na vitambulisho vyao viko tayari—na bahati nzuri huwa tunawatumia ujumbe kwenye namba zao za simu kuwajulisha kwamba kitambulisho chako kiko tayari—nedeni mkachukue vitambulisho vyenu.
 
Usikute ndio wale Marehemu wa oktoba 29, nyie mnasubiri bible Dubai.
 
Back
Top Bottom