Serikali, viwanja mlivyopanga kujenga vitakuwa na hadhi ya kuandaa AFCON au ni kuweka nyasi bandia tu?

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Habari wapenzi wa michezo.

Serikali inasema kuanzia mwaka ujao wa Fedha itaanza kujenga viwanja mikoani na itaanza na mikoa 10.

Ni jambo jema,sasa swali je hivi viwanja vitakuwa na standards za sports complex au ndio kufanya Bora liende kwa kuweka manyasi bandia basi?

Nashauri serikali ianze na viwanja vichache Kama vi 5 tuu ila viwe viwanja kweli sio utopolo.

Screenshot_20220220-161205.png
 
KAMA NI VIWANJA VYA KISASA NAAMINI VITAKIDHI FIFA STANDARDS NA VITAFAA KUHOST MASHINDANO MAKUBWA LOCAL NA INTERNATIONAL

WATAZAMAJI 40,000, 50,000, 60K NA KUENDELEA
 
Kujenga kiwanja kimoja chenye kukidhi viwango vya kimataifa kwa kujibana sana ni Tshs. bilioni mia moja, chini ya hapo ni kujidanganya bure.

Sidhani kama serikali hii ina uwezo wa kujenga viwanja vyenye hadhi hiyo kama miradi yote ya sasa inasuasua kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa kukopeshwa na hivyo viwanja bila shaka haviwezi kujengwa bila mikopo.

Kwa serikali inayoongozwa na watu wenye akili haiwezi kuongelea ujenzi wa viwanja vya michezo wakati sasa hivi shule karibu zote za mijini hazina madarasa ya kutosha wala viwanja vya michezo kwani viwanja vyote ni majengo tupu.

Kuna haja ya serikali kuanzisha mradi maalum wa kujenga maghorofa kwenye shule zote za mijini ili maeneo yapatikane tena kwa ajili ya viwanja vya shule na swala la viwanja vya mpira mikoani lisogezwe kwanza mbele.
 
Tatizo sisi maskini tunawaza ngono tuu...kazi kuzaana bila mpango. Ina maana serikali kila mwaka kazi yake iwe kujenga madarasa tu kisa ngono za wananchi wake zilizopitiliza.

Madarasa ya covid19 yanatosha jengeni hata viwanja navyo vitakuwa sehemu ya manufaa sio kila siku madarasa tuu na wasomi wenyewe hawaonekani.
 
Wanajenga vipya au wanakarabat vilivopo Kama wanakarabat vilivopo hilo n jambo zuri ukiangalia arusha jiji kubwa kabisa la utalii ET halina kiwanja kikubwa cha maana
 
Majiji matano haya yangeanzwa kujengwa mbeya mwanza Arusha dodoma na tanga wangetenga billion miatano au mia nne na tff wasaidie zile wanazopewa na FIFA pesa
 
Naomba kuuliza?

Hivi CCM wanaweza kukubali serikali ijenge kiwanja cha kisasa katika mkoa ambao CCM wana kiwanja chao kikubwa, japo kimechoka ila huwa wanakikodisha wanapata hela ya matumizi?

Kama CCM watakubali serikali ijenge viwanja, basi kweli CCM watakuwa wamebadilika!
 
Mimi mawazo yangu ni tofauti kidogo mimi nashauri serikali iwekeze nguvu kubwa kwenye kutenga maeneo ya michezo kila kitongoji na mtaa nchi nzima kisha vijengwe viwanja vingi vya vya gharama ndogo ili kumwezesha kila mtanzania mwenye kipaji chake apate mahali pa kucheza kirahisi.
 
Naomba kuuliza?

Hivi CCM wanaweza kukubali serikali ijenge kiwanja cha kisasa katika mkoa ambao CCM wana kiwanja chao kikubwa, japo kimechoka ila huwa wanakikodisha wanapata hela ya matumizi?

Kama CCM watakubali serikali ijenge viwanja, basi kweli CCM watakuwa wamebadilika!

Hivyo viwanja ni mali ya Watanzania, na siyo CCM! Binafsi nadhani lingekuwa ni jambo la busara kama hao ccm wange virejesha viwanja vyote Serikalini, halafu vingekarabatiwa upya, na kusimamiwa na Halmashauri zetu. Full stop
 
Tuache ujuaji sana, viwanja vimekua kero kubwa ,sana kama tumepigia kelele at least nyasi bandia au kapeti bas tushukuru hata wazo la kuvikarabati vilivyopo kwa angalau sehemu ya kuchezea (pitch) mambo mengine ni ya kushukuru kwanza
 
KAMA NI VIWANJA VYA KISASA NAAMINI VITAKIDHI FIFA STANDARDS NA VITAFAA KUHOST MASHINDANO MAKUBWA LOCAL NA INTERNATIONAL

WATAZAMAJI 40,000, 50,000, 60K NA KUENDELEA
ukizungumzia Afcon Ni pamoja na kupkea wageni. Huko mikoani Kuna sehemu za maana za malazi.
 
Back
Top Bottom