Serikali, wadau waombwa kuwasaidia wanaohudumia watoto wenye kiharusi na kupooza

Serikali, wadau waombwa kuwasaidia wanaohudumia watoto wenye kiharusi na kupooza

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
20220226_125144.jpg

Mkurugenzi wa Sadeline Health Care, Bi Sara Kitainda akizungumza katika Mchana wa Tabasamu, leo Februari 26, 2022.

Serikali na wadau wameombwa kuwawezesha na mitaji ya kibiashara akina mama na walezi wenye watoto wenye kiharusi na waliopooza kwani hutumia muda mwingi kuwahudumia watoto hao na wakati mwingine wakiwa hawana kabisa msaada wa wenzi wao.

Wito huo umetolewa na Bi. Sara Kitainda, Mkurugenzi wa Sadeline Health Care, shirika linalojihusisha na magonjwa yasiyoambukizwa hususani kutoa huduma kwa watoto wenye magonjwa ya kiharusi pamoja na kupooza, wakati akizungumza katika Mchana wa Tabasamu -- tukio lililoandaliwa na taasisi hiyo kuwaleta pamoja wazazi, walezi pamoja na watu wenye magonjwa hayo.

"Tunaomba Serikali iunge mkono mkakati huu ili wanawake wanaouguza watoto waliopooza waweze kujiweza na kuhudumia watoto wao vizuri", amesema Bi. Kitainda.

Naye mmoja wa wazazi anayehudumia mtoto aliye na mtindo wa ubongo, Bw. Daudi Ndabahalie amewataka wazazi na walezi wengine kuhakikisha wanawahudumia kwa mapenzi watoto wao wenye changamoto hizo.

"Tupo akina baba tuliozaa watoto wa namna hii na tumewatelekeza. Mimi nimekubaliana na hali ya mtoto wangu tangu alipozaliwa. Mtoto hatembei wala hakai lakini yupo darasa la 5 sasa na kila siku ninambeba kilomita 2 kumpeleka shule na kumrudisha nyumbani" amesema Bw. Ndabahalie. "Mtoto wa namna hiyo usipompenda unaweza kumpoteza mapema kwani mara nyingi wanakuwa na hasira".

Bw. Ndabahalie pia amesema wazazi walio na watoto wa namna hiyo mara nyingi hawana msaada kwani hata viongozi huzungumza nao tu bila ya kuwasaidia kutatua changamoto zao kwani hata miundombinu ya Choo shuleni si rafiki kwa watoto wenye matatizo hayo.

Shirika la Sadeline Health Care pia limezindua mpango wa miaka mitano utakaowezesha kupita kwenye Serikali za mitaa ili kutambua watoto wanaosumbuliwa na magonjwa yasiyoambukizwa hususani kiharusi na kupooza.
 
Hivi inakuaje mtoto anapata kiharusi? Stroke?
 
Back
Top Bottom