Serikali walikosea kwenye swala la uuzaji wa mahindi

Usiwe na narrow mind. Hawashindwi kutuacha na kwenda Southern Sudan na Somali, pote huko wameshapenetrate zaidi yetu, these guys are Capitalist sio sisi ambao Hatujitambui hadi leo. Hayo Masoko Mawili yanaweza kuwatosha Sana Wakenya na kuwa substitute ya Tanzania licha ya political instabilities!
 
Kwani lazima yauzwe Kenya, hapo kwa wananchi wa Sumbawanga, Mbeya, Songwe na Ruvuma watayauza Zambia na Kenya watayanunua wakijua yametokea Zambia
Kenya ni karibu zaidi.usafirishaji wake hautagharimu na mkulima atanufaika.
 
Ni kweli umetoa logistics options lakini ingependeza kama pia ungetoa na uchambuzi wa gharama zake ili kupata ulinganifu wa kitaarifa.
Kuhusu cost inapunguwa pia sababu mahindi husafirishwa in bulk so wanaweza safirisha kwa train which is cheap mode of transport hadi Msumbiji kisha wakapakia kweli meli port of beira which is also cheap (economies of scale) mzigo utapelekwa Mombasa port then sgr ya Kenya itayachukua hadi interior, umeona hapo ni train na meli tu zimefanya kazi ya kubeba mzigo mwingi kwa gharama nafuu mwisho multmodal itaishia huko Nairobi, Kisumu etc hadi kwa mlaji wa mwisho
 
Kwa hiyo hujui kuwa kuna aina mbalimbali za usafiri...Kenya wameshatuacha mbali hatuwezi kutunishiana nao msuli
Sidhani kama uko sahihi ndugu, wanatutegemea sana kwa soko la bidhaa zao. Mazungumzo na uimarishaji wa diplomasia ni muhimu baina yetu. Hilo la usafiri nimeshalijibu sana.
 
Itabidi yauzwe cheaper zaidi kuliko ambavyo wangeuza moja kwa moja Kenya. Zambia pia wanaweza kuhitaji kulinda soko lao, hivyo wasinunue mahindi ya Tz! Kwani suala la Mbaazi na Choroko na Dengu limekuwaje? Tuache Akili za Kiburi, hakitusaidii!
Huko ndo usiseme, nilikuwa Karatu juzi watu wako taabani mbaazi kilo tsh 300 hamna wa kununua
 
Hawajapata Njaaaa hao Kenya.
Njaa ikiwakolea watakuja kulialia "

Kenyatta, utamsikia akisema haya, "Wajameni, sisi ni majarani zenyu, mutupee chakula na hizo mahindi zenyu!!!
 
Hawajapata Njaaaa hao Kenya.
Njaa ikiwakolea watakuja kulialia "

Kenyatta, utamsikia akisema haya, "Wajameni, sisi ni majarani zenyu, mutupee chakula na hizo mahindi zenyu!!!
Wasingekuwa na njaa wasingeivuka Tz wakaenda Zambia. Hapo ndo ujue Wana njaa haswa, otherwise they could bow to us wakanunua kwetu! Sisi Sasa Labda tuloge Zambia nako kuwe na Ukame na Kenya iwe hivyo na Uganda ili wakose Options!
 
Huko ndo usiseme, nilikuwa Karatu juzi watu wako taabani mbaazi kilo tsh 300 hamna wa kununua
Ndo hivyo Mkuu! Adhma ya kutufanya Tuishi Kama Mashetani naona inatekelezwa Vyema!
 
Hivi nani vile alipiga kelele nchi hii ina njaa? mpaka akajitia eti ataawagizia chakula wananchi cjui yeye akiwa kama nani? je hukuona busara ilitumika kuzuia uuzwaji wa mazao ili kusikiliza hayo malalamiko yaliyoshikiwa bango mpk na wale mamluki wa kijerumani isije kuonekana dharau kuwa mna njaa then mnauza mazao nje! sasa baada ya mahindi na mazao mengine kuzidi na kukosa soko leo zinaibuka hoja za kuunganisha matukio sijui mahindi yamekataliwa kenya kwani ni kenya tu ndio wannaopaswa kununua hayo mahindi? au kuna jambo unataka kulisema unasingizia mahindi
 
Zambia kwenda kenya unapitia wapi vile? Ushuru wa mahindi toka zambia kupita tanzania kwenda kenya tuupige 10000% tuone sasa, kama mbwai mbwai tu, kama vp wakayachukie kwa ndege na wasipite anga yetu la sivyo tunawatungua tu. Hapa kazi tu hakuna kulemba.
 
Sidhani kama uko sahihi ndugu, wanatutegemea sana kwa soko la bidhaa zao. Mazungumzo na uimarishaji wa diplomasia ni muhimu baina yetu. Hilo la usafiri nimeshalijibu sana.
Tatizo la watanzania kama wewe huwa mnakuwa proud na vitu vyenu mpaka mnahisi dunia nzima ni nyie tu mmebarikiwa and mnahisi nchi zote zinawategemea nyinyi...dunia ya sahivi Luna kila aina ya option...ukikataa wewe kufanya biashara na mtu fulani yupo mwingine ambaye atafanya...Kenya washatuacha mbali and hats bila sisi wanaweza ku survive tu
 
Narrow minded?
Somalia watu 14,317,996 makadirio ya 2016. GDP(PPP) $4.431bn. Per capital $400
South Sudan watu 12,230,730(makadirio ya 2016), GDP(PPP) $20.038bn, per capital $1525.
Tanzania watu 55,572,201 GDP $163.522bn, per capital $3296.
Ndugu nakuomba tutumie uhalisia wa mambo bado sisi ni soko kubwa na la muhimu sana kwa Kenya industrial produce na hii ni kwa vyote uwezo wa kununua na idadi ya watu. As you said, Kenyans are more development oriented than us hivyo sifikirii kama wataacha potential market kama Tanzania.
Kama nilivyopendekeza mazungumzo ni muhimu sana juu ya hii hali ya sasa ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili na kwa faida ya wote.
 
Ni kweli ndugu na itakuwa vizuri kama pendekezo nililotoa hapo mwishoni litafanyiwa kazi. Lakini ni sababu zipi zilitufanya tujitoe COMESA?

Walidai eti tulikuwa tumejiunga kwenye hizo taasisi nyingi. Yaani COMESA, SADC, PTA, EAC etc
 
Umeandika suala la muhimu ndugu lakini kumbuka hata sisi tuna tazara na Dar es salaam port ambayo imeanzia kwao na nafikiri ni fupi na cheap kuliko kupitia Beira port.
 
Wata-survive lakini lazima wayumbe kidogo kiuchumi sisi bado ni soko kubwa sana kwao.
Na kuhusu resources wala sisi hatujabarikiwa kiivyo kama tunavyoaminishwa. Mfano wa jirani: DRC ana untapped minerals worth $21+trillions sawa na Tsh 40+quadrillions, land bank almost two times our land bank, the mighty Congo river ambayo inaweza supply umeme sehemu kubwa ya bara la Africa, mvua za kutosha na misitu minene ya kitropiki kuliko sisi. Kwa ufupi DRC ni tajiri mkubwa wa natural resources kuliko nchi nyingi duniani.
Kwa kweli bado Kenya inatuhitaji kama soko lao la msingi na sisi pia tunaihitaji. Hivyo kuirudisha hali hii ya sasa iwe kama awali kwa kupitia mazungumzo ni muhimu kwetu site.
 
Hawawezi kuyumba kama wewe unavyofikiria...unadhani kenya hamna wachumi wabobezi ambao washafanya evaluation kwa maamuzi wanayofanya...or wewe una akili kuliko magwiji wanaofanya mipango ya maendeleo nchini kenya
 
Walidai eti tulikuwa tumejiunga kwenye hizo taasisi nyingi. Yaani COMESA, SADC, PTA, EAC etc
Nafikiri linaweza kuwa kosa hasa kwa wakati huu ambao tunasema tunataka nchi ya viwanda. Endapo kama ndoto hii itatimia basi tutahitaji masoko ya nje mengi kadiri tuwezavyo.
 
Hawawezi kuyumba kama wewe unavyofikiria...unadhani kenya hamna wachumi wabobezi ambao washafanya evaluation kwa maamuzi wanayofanya...or wewe una akili kuliko magwiji wanaofanya mipango ya maendeleo nchini kenya
Sawa MZEE MSASAMBEGU inawezekana najibizana na mtu ambae ana umri kama wa baba yangu.
Siku njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…