Ndugu, kwanza fahamu kwamba na mimi ni mkulima ambae nina mahindi ndani yanasubiri bei ipande yauzwe ili pesa iingizwe kwenye kilimo tena.
Pili itakuwa vyema endapo utanipatia gharama za kupitisha mahindi toka Zambia, Zimbabwe/Malawi then beira port Mozambique kisha yapakiwe kwenye meli hadi Mombasa port. Baada ya hapo tulinganishe na kutumia tazara railway au Capetown-Cairo highway. Vivyo hivyo na kwa usafiri wa anga pia.
Mwisho lakini muhimu sana, NAIPENDA SANA NCHI YANGU, na KAMWE sitathubutu kufanya/kushiriki jambo au kutoa ushauri wa KUHARIBU nchi yangu, siwezi KABISA.
Na hapo mwishoni kama umesoma vizuri nimetoa pendekezo nini kifanyike.