Serikali walikosea kwenye swala la uuzaji wa mahindi

Serikali walikosea kwenye swala la uuzaji wa mahindi

Siyo rahisi kivile. Hivi unawajua Wazambia? Pia ujue bei yao ni ndogo kuliko yetu kwa sababu ya Economy of scale,wana mashamba makubwa ya kufa mtu.
Tuanzie hapo kwanini sie tunashindwa kulima mashamba makubwa wakati ardhi nzuri tunayo, jibu ni kuwa kilimo hatukipi mkazo unaotakiwa
 
Kwani lazima yauzwe Kenya, hapo kwa wananchi wa Sumbawanga, Mbeya, Songwe na Ruvuma watayauza Zambia na Kenya watayanunua wakijua yametokea Zambia

Ni sawa na kupeleka ule Mchele wa Japan Kyela uuzie kule ndio wanunuzi waone umetoka Kyela.. Nonsence.
 
Wanao umia sasa niwakulima wadogo kutokana namaamuzi ya hovyo ya viongozi wetu.wanasahau kuwa binaadamu tunaishi kwa kufaidiana.so chuki na visasi hatitakiwi miongoni mwetu.
Athari yake ni vita baridi maana wafanyabiashara wa tz wanao tegemea kenya na wakenya wanao tegemea tz watakua na utata tu
 
Ndugu, kwanza fahamu kwamba na mimi ni mkulima ambae nina mahindi ndani yanasubiri bei ipande yauzwe ili pesa iingizwe kwenye kilimo tena.
Pili itakuwa vyema endapo utanipatia gharama za kupitisha mahindi toka Zambia, Zimbabwe/Malawi then beira port Mozambique kisha yapakiwe kwenye meli hadi Mombasa port. Baada ya hapo tulinganishe na kutumia tazara railway au Capetown-Cairo highway. Vivyo hivyo na kwa usafiri wa anga pia.
Mwisho lakini muhimu sana, NAIPENDA SANA NCHI YANGU, na KAMWE sitathubutu kufanya/kushiriki jambo au kutoa ushauri wa KUHARIBU nchi yangu, siwezi KABISA.
Na hapo mwishoni kama umesoma vizuri nimetoa pendekezo nini kifanyike.
Nimetoa logistics options sasa wewe usinilaumu mimi walaumu wanaoweka vikwazo vya biashara nadhani unawajua
 
Tatizo kubwa ni mikataba ya kimataifa tunayoingia kama taifa. Unakumbuka Tanzania ilijitoa COMESA wakati wa utawala awamu ya 3 wakat Waziri wetu alikuwa Mh. Idd Simba. Zambia na Kenya bado wako COMESA. Tanzania na Zambia wako SADC. Kenya na Tanzania wako EAC.

Sasa hapa ndiyo migongano ugumu inapoanza. Ukikataza mahindi ya Zambia yasipite Tanzania kwenda Kenya , kwanza unavunja mikataba ya SADC na EAC, pili unaharibu uhusiano na nchi hizi.
Ni kweli ndugu na itakuwa vizuri kama pendekezo nililotoa hapo mwishoni litafanyiwa kazi. Lakini ni sababu zipi zilitufanya tujitoe COMESA?
 
Tuanzie hapo kwanini sie tunashindwa kulima mashamba makubwa wakati ardhi nzuri tunayo, jibu ni kuwa kilimo hatukipi mkazo unaotakiwa
1. Tufanye land policy reform. Siyo rahisi kupata mwekezaji wa kweli kwenye kilimo huku akijua wakati wowote atanyanganywa eneo na kugawiwa watu. This is where the nucleus of agric investiment failure starts.
2. Mashamba makubwa yaliyokuwa ya serikali yabaki yaboreshwe,yasigawiwe watu hovyohovyo ambao hawana nyenzo na hata ya kwao yamewashinda. Vijana wetu mf.kutoka SUA wawezeshwe,waendeshe na wasimamie mashamba haya mfano lile la Mbarali
3.......
4....
 
Kenya bei ya bhangi imepanda sana baada Tanzania kufyeka mashamba ya bhangi, kumbuka 40% ya wakenya wanavutana bhangi wakiongozwa na rais wao
 
Nimetoa logistics options sasa wewe usinilaumu mimi walaumu wanaoweka vikwazo vya biashara nadhani unawajua
Ni kweli umetoa logistics options lakini ingependeza kama pia ungetoa na uchambuzi wa gharama zake ili kupata ulinganifu wa kitaarifa.
 
Taarifa umeipata wapi ndugu?
Na mahindi ya Zambia si lazima yapitie Tanzania ndipo yaende Kenya?
Iwapo na sisi tukizuia yasipite itakuwaje?
Nadhani umefika wakati wawakilishi wa mataifa haya wakae na kuzungumza. Hizi "stunts" hazitamfaidisha yeyote yule.
Unaweza kudhani Ni lazima yapite Tanzania kumbe yakapita Msumbiji kwa Treni na kupakiwa kwenye Meli kisha kuletwa Kenya, kitu ambacho Ni cheaper kuliko kukatiza Tz na Malori! Zambia to Mozambique by Rail inawezekana ikawa cheap zaidi! So tusiringe Sana!
 
...Kwa hiyo sisi kazi yetu itakuwa ni kugombana na neighbors tuu? Ndiyo uchumi wa viwanda huo?
 
Kwani lazima yauzwe Kenya, hapo kwa wananchi wa Sumbawanga, Mbeya, Songwe na Ruvuma watayauza Zambia na Kenya watayanunua wakijua yametokea Zambia
....Someni threads between the lines...si umeambiwa Zambia wana mahindi mengi na bora?
 
Unaweza kudhani Ni lazima yapite Tanzania kumbe yakapita Msumbiji kwa Treni na kupakiwa kwenye Meli kisha kuletwa Kenya, kitu ambacho Ni cheaper kuliko kukatiza Tz na Malori! Zambia to Mozambique by Rail inawezekana ikawa cheap zaidi! So tusiringe Sana!
Hata sisi tuna tazara ambayo nafikiri ni cheap zaidi.
 
Kwani lazima yauzwe Kenya, hapo kwa wananchi wa Sumbawanga, Mbeya, Songwe na Ruvuma watayauza Zambia na Kenya watayanunua wakijua yametokea Zambia
Itabidi yauzwe cheaper zaidi kuliko ambavyo wangeuza moja kwa moja Kenya. Zambia pia wanaweza kuhitaji kulinda soko lao, hivyo wasinunue mahindi ya Tz! Kwani suala la Mbaazi na Choroko na Dengu limekuwaje? Tuache Akili za Kiburi, hakitusaidii!
 
Ndy fresh ungali uwe wa kumwaga hapa kwetu bora wagome tu moja kwa moja hiyo biashara ife wauze hapahapa ndani kwetu
 
Taarifa umeipata wapi ndugu?
Na mahindi ya Zambia si lazima yapitie Tanzania ndipo yaende Kenya?
Iwapo na sisi tukizuia yasipite itakuwaje?
Nadhani umefika wakati wawakilishi wa mataifa haya wakae na kuzungumza. Hizi "stunts" hazitamfaidisha yeyote yule.
Kwa hiyo hujui kuwa kuna aina mbalimbali za usafiri...Kenya wameshatuacha mbali hatuwezi kutunishiana nao msuli
 
Kenya bei ya bhangi imepanda sana baada Tanzania kufyeka mashamba ya bhangi, kumbuka 40% ya wakenya wanavutana bhangi wakiongozwa na rais wao
Watu wanajadili mstakabadhi wa taifa ww unazodoa.....
 
Back
Top Bottom