Serikali: Walimu wa Shule za Sekondari na Msingi walioajiriwa ni elfu nane pekee

Serikali: Walimu wa Shule za Sekondari na Msingi walioajiriwa ni elfu nane pekee

Mbona mkapa na kikwete walikua wanaajiri wote??
Swali gum mkuu, Sina jibu, waliokua kwenye serikali zao wanawaza tujuza, na nakubali kabisa kipindi hicho nafasi za kazi zilikuwa nyingi, KWA waliokua na uhitaji wa kufanya kazi serikalini, wengi walikua wanazikimbia kwenda secta binfsi kutokana na malipo,KWA Sasa kote kumebana,
 
Jaman c tumeambiwa ni dona kantri hii au????
Swali gum mkuu, Sina jibu, waliokua kwenye serikali zao wanawaza tujuza, na nakubali kabisa kipindi hicho nafasi za kazi zilikuwa nyingi, KWA waliokua na uhitaji wa kufanya kazi serikalini, wengi walikua wanazikimbia kwenda secta binfsi kutokana na malipo,KWA Sasa kote kumebana,
 
Mkuu ebu acha hesabu za kwenye Makaratasi hizi( ni sawa na hesabu za kilimo cha Tikiti au ufugaji wa kuku/sungura)
Twende field kwenye Uhalisia wa mambo. Umepewa Milioni5 hii, Je wewe utafanya biashara gani ya kukuingizia Kipato cha Shs 40,000/(arobaini elfu) kwa siku?
Ni biashara gani au uwekezaji gani utaufanya kwa Mtaji huo?
Tunaomba Uzoefu wako nasi tinufaike kupitia wewe

Mkuu ebu acha hesabu za kwenye Makaratasi hizi( ni sawa na hesabu za kilimo cha Tikiti au ufugaji wa kuku/sungura)
Twende field kwenye Uhalisia wa mambo. Umepewa Milioni5 hii, Je wewe utafanya biashara gani ya kukuingizia Kipato cha Shs 40,000/(arobaini elfu) kwa siku?
Ni biashara gani au uwekezaji gani utaufanya kwa Mtaji huo?
Tunaomba Uzoefu wako nasi tinufaike kupitia wewe
Mkuu tatizo tunafikilia mda wote kuanza na biashara kubwa,bila kujua biashara ndogo ndo huleta mtandao wa biashara kubwa
Mfano,hivi wa kawaida Sana, hata hapo ulipo ukipata vijana wako watatu, wakukutembezea kahawa kila moja hasubui na jion akuletee elfu tano KWA siku una sh 15, KWA elfu arobain imebaki 25,je Kuna biashara ndogo ndogo ngapi za kuongoza elfu 3 na zaidi KWA siku,
Wakati wewe ukiwa upo free unakimbizana ulipoweka mtaji mkubwa ,mfano vipo vitoroli vya kubebea mizigo watu ukodi KWA elfu moja ,mpaka 1500, vipi ukiwa navyo hata 5, mbona m5 mkuu Kama umetuliza kichwa waweza ingiza hata zaidi ya iyo, miezi 6 ya kwanza ndo itasumbua, bahada ya hapo utashangaa
Sasa tatizo ni pale ukisema we ni msomi na unataka anza na biashara ya kisomi zaidi elfu 40 KWA pesa iyo upati,
 
Ajira za kweli na uhakika ziliondoka na kikwete huo ni ukweli nitausema daima hii serikali ya sasa ni wababaishaji tu ila inabidi tuipende maana ndio inayo ongoza hata tulie tupasuke hatuna namna
 
Mkuu ebu acha hesabu za kwenye Makaratasi hizi( ni sawa na hesabu za kilimo cha Tikiti au ufugaji wa kuku/sungura)
Twende field kwenye Uhalisia wa mambo. Umepewa Milioni5 hii, Je wewe utafanya biashara gani ya kukuingizia Kipato cha Shs 40,000/(arobaini elfu) kwa siku?
Ni biashara gani au uwekezaji gani utaufanya kwa Mtaji huo?
Tunaomba Uzoefu wako nasi tinufaike kupitia wewe
Unauza juice za matunda na matunda pia na chipsi iyo Hela unapata sema shida ni matumizi yako tu
 
Ajira haitolewi kwa faida ya aliyeajiriwa bali kwa ajili ya mwajiri.
Hii ni kanuni ya msingi kabisa.
Ajira siyo msaada, ni mkataba wa kumnufaisha mwajiri kwa kuwa mwajiriwa anahitaji.
 
walimu waliohitimu miaka mitano tuu wako zaidi ya milion 5 sasa hao 8000 watatoshea...

Yan ni bora waache kuzalisha fani hii ya watumishi walimu waliopo wanatosha kwa miaka 20 ijayo .

Wasiipoteze rasilimali watu na rasilimali muda kuwapa watu vitu wasivyovitumia kwenye soko la ajira na maisha halisi yenye ushindani katika kupata rasilimali fedha
 
Hali ni tete sana Mtaani hata makada tuko taabani,Ajira hatuna tunachekwa tu😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Ndumbaro acha upumbavu wa kina ndugai na mahera. Tangazo la ajira lilikuwa walimu 13,000. Baada ya wananchi kuona mapungufu makubwa kwenye orodha yenu ya waajiriwa ndiyo unakuja na usanii wa kijinga eti eti hii ni awamu ya kwanza ya walimu 8000. Wengine 5000 itakuwa awamu ya pili. Bila ya kukosolewa haya maelezo ungetoa ahera? Kwa taarifa yako hata awamu hii ya kwanza hawajafikia idadi ya 8000. Majina wamejirudiarudia na wengine hawana sifa.bHivi ujinga huu mtaacha lini? Wote mmekuwa watu wa kuokotwa majalalani? Serikali gani hii?
Great mkuu
 
walimu waliohitimu miaka mitano tuu wako zaidi ya milion 5 sasa hao 8000 watatoshea...

Yan ni bora waache kuzalisha fani hii ya watumishi walimu waliopo wanatosha kwa miaka 20 ijayo .

Wasiipoteze rasilimali watu na rasilimali muda kuwapa watu vitu wasivyovitumia kwenye soko la ajira na maisha halisi yenye ushindani katika kupata rasilimali fedha
Hawafik million 5
 
Barua ya wazi kwa sekretarieti ya ajira na TAMISEMI
Ndg, Viongozi wenye dhamana inayohusiana na AJIRA hususani Ajira za ualimu Mimi kama Mtanzania wa kawaida mwenye akili timamu na ambae pia ni Mdau wa ELIMU Naiomba Ofisi yako iweze kutoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya majina ya waajiriwa wa Kada ya ELIMU Yaliyotolewa na Wizara yako pendwa na Nyeti ya TAMISEMI. Tarehe 27/11/2020 kuna baadhi ya majina ya waajiriwa yanaendelea kuwapatia watanzania TAHARUKI KUHUSU AJIRA ZAO

Naomba nizungumzie aina hizi za makosa yaliyofanyika kwenye AJIRA hizi ambazo mmeutangazia umma wa watanzaniaKuwa zilichambuliwa na walioajiriwa walikidhi vigezo na sifa. Rejea barua kutoka kwa KATIBU MKUU OFISI YA RAIS -TAMISEMI ya Tarehe 27 November, 2020 yenye Kichwa cha barua TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI PAMOJA NA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA

Makosa hayo nimeyaainisha hapa chini kama ifuatavyo;-

a) Waajiriwa ambao walihitimu kidato cha NNE 2019.

b) Waajiriwa ambao walipataufaulu hafifu wa daraja LA NNE kuanzia alama 30- 33

c) Waajiriwa ambao hawakufanya mtihani wa kidato cha NNE.

d) Waajiriwa Ambao vituo vyao vya kufanyia mitihani NECTA Haivitambui.

e) Waajiriwa ambao hawako kwenye orodha ya watahiniwa Wa mwaka husika kulingana na namba yake ya usajili wa kidato cha nne.

f) Waajiriwa ambao walisoma masomo tofauti na waliyopangiwa kufundisha kwenye ajira yao.

A). Waajiriwa ambao walihitimu kidato cha NNE 2019
Kwa akili ya kawaida ambayo haihitaji elimu kubwa tunajua kuwa mhitimu wa kidato cha NNE mwaka 2019 Moja kwa moja atakuwa hajahitimu mafunzo ya ualimu iwe Astashahada, Stashahada au shahada ya Ualimu kwa Mwaka mmoja kwani ni dhahiri shahiri kuwa mhitimu huyu wa mwaka 2019 Matokeo yake aliyapata Mwanzoni mwa mwaka 2020 au Mwishoni mwa mwaka 2019 sasa kama hivyo ndivyo imekuwaje MTU huyu akaajiriwa mwaka huu 2020 ile hali hana mafunzo ya ualimu? Au waliosomea Ualimu wameisha mpaka TAMISEMI imeanza kuajiri waliosomea VETA kuja kufundisha shule za msingi na sekondari. Mfano wa waajiriwa hao ni hao hapa ambao ni baadhi ya wengi mliowaajiri;-

Ally Miraji Shalua S3838-0063/2019

Bakari Lauzi Bakari S3678-0064/2019

Mariam Said Dibwine S0208-0140/2019

Hao ni baadhi yao Ila wapo wengi sana na sababu ya wizara kuajiri hao ambao yawezekana hawana sifa za kuajiriwa sijazijua. Naomba ufafanuzi

B). Waajiriwa ambao walipata Ufaulu hafifu wa daraja la NNE kuanzia points 30-33.

Kulingana na miongozo ya Wizara ya elimu inasema wazi kuwa mhitimu wa kidato cha NNE anatakiwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Astashahada anatakiwa awe amepata ufaulu wa daraja LA kwanza hadi daraja la NNE LA points 28 lakini mwaka huu tumeshangazwa na kilichofanywa na TAMSEMI kuajiri wahitimu ambao walipata ufaulu wa daraja LA NNE LA points 30-33. Je, hapa tayari utaratibu ule wa awali ulikuwa umekiukwa au Sekretarieti ya ajira siku inaajiri ilikuwa imelala usingizi au ilirusha sandakalawe kwa waombaji wa ajira hizo?

Wafuatao ni baadhi ya waliopata ufaulu huo wa daraja LA NNE LA Points 30 hadi 33 ;-
A) ABDALLAH AHMED JIGWA S2732-0091/2019 alipata daraja LA NNE la points 31

B) BAKARI RAJABU KHALIFAN S1680-0064/2019 Alipata Daraja la NNE la points 30

C) FAUSTA SHAO ALEXANDRY S2019-0008/2019 Alipata daraja la NNE la points 32

D) DAVID LAMECK NDOSSA S1943-0147/2019 Alipata daraja la NNE la Points 33.
Hao ni baadhi ya wenye ufaulu hafifu ambao sasa wanaenda kuwafundisha wanafunzi wetu ili na sisi siku moja tupata wanafunzi Bora wenye umahili wa sayansi ya viumbe, sayansi ya Nyota n.k
Naomba ufafanuzi

C) Waajiriwa ambao hawakufanya mtihani wa kidato cha NNE
Kwenye orodha ya ajira hizo kuna MTU mmoja ambae Mimi nimembaini miongoni kwa wengine ambae hakufanya mtihani wa kidato cha NNE lakini Leo hii ameajiriwa na wizara yako shida iko wapi? Je, sekretarieti ya ajira iko sawa kwenye hili au lilikuwa ni takwa la kisiasa? Mwajiriwa huyo ni huyu hapa;-

Halima Saidi Mohamed P2735-0006/2019
Natambua kabisa inawezekana alijisajiri kurudia mtihani lakini hapa tena yanaweza yakaibua Maswali Mengi sana kama namba yake ni P ambayo inaonesha kuwa mtahini huyo alijisajiri kama mwanafunzi binafsi hivyo kupewa namba hii ndo ilikuwa Mara yake ya kwanza kutaka kufanya mtihani huo wa taifa ambao hakuufanya lakini Leo ameajiriwa na Anatarajiwa kwenda kazini kuripoti na kuwafundisha wanafunzi. Kwa tafsiri ya haraka haraka ametoka darasa la Saba na kwenda kufundisha.
Naomba ufafanuzi

D) Waajiriwa ambao vituo vyao vya kufanyia mitihani *NECTA haivitambui. Kuna baadhi ya waajiriwa ambao kwa namba ambazo zinawaelezea kwenye orodha ya ajira ukitafuta kwenye urodha ya shule unakuta namba hiyo ya mtahiniwa haipo yaani namba ya shule hiyo haipo na kama haipo inamaanisha mtahiniwa huyo ni HEWA kwani shule hiyo haipo Tanzania .
Mfano wa waajiriwa hao ni hawa hapa kwa baadhi hao kwani wako wengi;-

i) LUKAS EMMANUEL MTOI S1380-0852/2019

ii) PETRO ADRIANO KIOSHA S0566-1215/2019

iii) RAJABU STUART WILLIAM S0440-0963/2019

iv) SHOTO SOSTHENES NYANDA S1380-1058/2019
Naomba ufafanuzi kwanini mwajiriwa aweke namba ambayo haioneshi alisoma wapi elimu yake ya kidato cha NNE alafu pia TAMISEMI na sekretarieti ya Ajira ilitumia Matokeo kutoka wapi kumwajiri au kuwaajiri hawa inamaana hawapo wenye vyeti na sifa za ualimu kuajiriwa mpaka mkaajiri ambao wamedanganya mpaka vituo vyao vya kufanyia mtihani.

E) Waajiriwa ambao hawako kwenye orodha ya watahiniwa wa mwaka husika kulingana na namba yake ya usajili wa kidato cha nne.
Kuna baadhi ya waajiriwa wameoneshwa kwa namba za usajiri wa kidato cha nne Ambao ukiangalia orodha ya waliofanya mtihani mwako huo mhusika hayuko kwenye orodha hiyo kwa Tafsiri ya haraka ni kwamba mhusika hakufanya mtihani kwani hakusajiriwa. Mfano ni Mwajiriwa
SHAFII MOHAMMEND NAMKURUNG'UNDU S0738-0076/2019 Mwajiriwa huyu kwa namba hii ya usajiri inaonesha alisoma Shule ya sekondari Ridhwaa Seminary mwaka 2019 lakini cha ajabu mwaka huo kwenye shule hiyo watahiniwa walikuwa 61 Ila Mwajiriwa namba namba yake ilikuwa ni no 76. Kwa maneno mepesi mtahiniwa wa mwisho kwenye mtihani huo alikuwa mwenye no S0738/0061/2019 ila Mtajwa hapo juu namba yake ya Mtihani ni S0738/0076/2019
Kwa maneno na ushahidi huo hakukuwepo na mtahiniwa anaeitwa SHAFII MOHAMMED NAMKURUNG'UNDU.
Naomba ufafanuzi yeye alifanyia wapi mtihani wa kidato cha nne?

F) Waajiriwa ambao walisoma masomo tofauti na waliyopangiwa kufundisha kwenye ajira yao

Kuna baadhi ya waajiriwa kwenye orodha yako wameoneshwa kwenda kufundisha au kuandaa vifaa vya maabara ile hali MTU huyo hakufaulu somo lolote lile linalohusiana na Maabara yaani kama aliyasoma masomo hayo basi hakufaulu alipata alama F
Mfano ni Mwajiriwa David Lameck Ndossa S1943-0147/2019 Mwajiriwa huyu alifeli somo la Biology lakini Leo ameajiriwa kwenda kuwa Laboratory Technician Lugufu wasichana Sekondari Hata kama kuna kurudia Mwajiriwa alirudia mtihani lini na akafaulu lini? Maana ni mhitimu wa mwaka 2019?.

ZINGATIA Kwenye orodha ya majina ya walimu waliopangiwa vituo vya Nazi Novemba 2020 kuna jedwali ambalo lina neno Applicant Id Nimejiridhisha pasi na shaka kwa waajiriwa ambao walifanya mtihani miaka ya 2009 na 2010 hii Applicant Id ni Index no ya Mwajiriwa ya mtihani wa kidato cha NNE .
Mfano
Abbas Juma Malungo S1222-0100/200

Abdallah Rajabu Dumwe S0811-0102/2009

Zuhura Musaka Majaliwa S0316-0238/2010 MAJINA HAYO PASI NA SHAKA YANASOMEKA HIVYOHIVYO KWA WAHUSIKA NA NAMBA ZAO ZA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NI HIYOHIYO.

Kulingana na maelezo hayo na ushahidi huu nilioutoa TAMISEMI HAIONI AJIRA HIZI ZINAIBUA MASWALI MENGI KULIKO MAJIBU *

1. Je, ni ajira kweli na walioorodheswa ni sahihi?
2. Hazijakaa kisiasa kwa sababu ya mapungufu yake? Maana tuliwahi kuambiwa kuwa Serikali ya awamu ya Tano inaangalia uchapaji kazi wa MTU na sio Vyeti.
3. Hamuoni kwa mapungufu haya na mengine ukafanyika uchunguzi wa wazi kuhusu ajira hizi?

4. Walioidhinisha ajira hizo wanalitakia nini taifa kwenye Tasnia ya Elimu?

5. Kwa makosa hayo ofisi na mishahara wanayolipwa hawa waliotoa ajira hizi hawaoni hawatutendei haki sisi walipakodi wa Nchi hii?

Wako,
Prof Hans
Mwalimu asiyekuwa na Kituo maalumu cha Kufundishia
4⁴n7
 
Back
Top Bottom