Serikali: Watanzania 66 wameukana Uraia

Serikali: Watanzania 66 wameukana Uraia

Kila mtu yuko huru kuamua lililo katika uhuru wake....

Nyumbani ni Tanzania....nakupenda Tanzania....[emoji7]

#SiempreJMT[emoji120]
 
Wala siyo mapenzi, hujapata fursa bado

Kwanini unapenda unachoamini wewe na wengine wawe hivyo. Fursa ipi kwa mfano. Kuna changamoto sana kuishi nje ya mahali ambapo umekuzoea na kukulia na kujiskia huru na home.

Ulaya hata Ukiwa na passport yao, utajua kabisa kuwa hapa Sio kwetu hata kama maisha umeyapatia. Wazungu hawataweza kukuona mwenzao Ila wanaweza kutumia ujuzi wako na akili Zako. Wanajua kuheshimu vipawa. Lakini watakukumbusha kwa namna nyingi kuhusu kwenu na uduni wetu.

So inategemea wewe binafsi na malengo yako maishani. Kuna raha sana unapotua nyumbani. Changamoto zipo pia. Unatua, then ukianza kuingia Sasa dar mtaani mpango wa majengo na uchafu nk. Unakutia simanzi. Ila ukishatulia unamaliza likizo kwa rahaaaaaa na uhuru usio na hata maelezo. Maswali ya wie lange sind sie schon in Deutschland, wie lange noch? Gibt es bei euch sauberes Wasser wie hier bei uns? Schaut man auch bei euch Fernseher an? Usw.

Kuna Wakati unapata Shida ukipanda train iliyojaa kwa maana ya seat Mbili moja Ina Mzungu tayari na nyingine leer oder frei. Wapo wenye busara anakuwahi na kukuuliza Kama utapenda kukaa. Ni changamoto sana hata kama una miaka 20 na zaidi huku.

Hakuna lebo ya rangi na muda mtu aliokaa na changamoto zitabaki. Mambo Kama haya kwa wengine ni madogo na wengine ni makubwa. Mimi ntakula ma purée yao lakini ntabaki Raia wa Tansania with unbefristetes viza. Lakini wengine wanaona kuna maslahi na haki zinawapita kwa kutokuwa raia. So wanaamua kukana ili wanufaike. Ila daheim ist daheim. Nyumbani Ni nyumbani.
 
Kwanini unapenda unachoamini wewe na wengine wawe hivyo. Fursa ipi kwa mfano. Kuna changamoto sana kuishi nje ya mahali ambapo umekuzoea na kukulia na kujiskia huru na home...
Mimi naona umeandika madikodiko tu, unauliza swali, haujajibiwa umeshalalamika, haujaulizwa umeshajibu.
Sasa ulitaraji kichwa kikiwa na mafaili yameparanganyika kwa mpangilio kama huu unaweza ukaona maisha ya nchi za watu ni mepesi kweli?
 
Kwanini unapenda unachoamini wewe na wengine wawe hivyo. Fursa ipi kwa mfano. Kuna changamoto sana kuishi nje ya mahali ambapo umekuzoea na kukulia na kujiskia huru na home...
Sasa we jamaa unajinasibu nyumbani ni nyumbani hafu unatupigia na kijerumani humo humo na unajua wataosoma hii comment ni wabongo au ndio ili tuamini kweli uko mambele.

Mkuu najifunza kijeruman nina siku tatu unaweza kunisaidia apps ya bure au kunipa abc nipate au mwanga kwa mbali kama iyp wasser nimesoma jana inatamkwa vazaa maana yake maji hahaha.
 
Nina wivu na nchi yangu hasa nikiangalia nchi zote Duniani zinavyodhibiti Raia wa kigeni katika nchi zao lakini Tanzania WAGENI wanaingia kiholela na kununua viongozi wote wananua Ardhi kupitia viongozi Wetu lakini tunachekelea wanaishi Nchini Kwa kiburi na kufanya dhuruma mbalimbali EBU WA Tanzania tuamke jamani.
 
Hiyo idadi ni kwa walioenda kutoa taarifa kwenye balozi zetu wapo ambao hata hawana huo muda wa kutoa hizo taarifa ni wengi zaidi...
 
Hiyo idadi ni kwa walioenda kutoa taarifa kwenye balozi zetu wapo ambao hata hawana huo muda wa kutoa hizo taarifa ni wengi zaidi...
Watanzania hata wakishaingia hizo nchi kwanza hata hawajisumbui kutaka kujua ubalozi wao ulipo au balozi wao ni nani, sababu hata likitokea la kutokea hizo balozi hazijawahi kuwa na misaada sanasana watakua wanawatafuteni kuwapigeni virungu vya ooh changieni nyumbani tujenge barabara, changieni nyumbani kuna mafuriko, changieni nyumbani tukajenge shule, changieni nyumbani tukajenge hospital wakati wenyewe wakiishi maisha ya anasa na wakopewa posho kubwa na kila kitu utafikiri hawatoki hiyo nchi ombaomba
 
Unaukana uraia unaenda kuwa mganda?
Inategemea yeye binafsi ana maslai yapi huko Uganda Kuna mwingine anakana urai ili andeshe biashara za mamilioni huko Uganda na mwingine anakana uraia ili akaendelee kudeki vyoo kwa uhuru huko Canada
 
Back
Top Bottom