Serikali: Watu 200,000 wanaoishi na VVU hawatambui hali za Afya zao

Serikali: Watu 200,000 wanaoishi na VVU hawatambui hali za Afya zao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Dar es Salaam.

Mchakato wa kuwapata watu 200,000 waishio na virusi vya ukimwi bila kujua ni mbinu mojawapo ambayo Wizara ya Afya imesema itaitumia ili kupunguza maambukizi mapya na kufikia malengo ya milenia mwaka 2030.

Pamoja na hayo Wizara imesema inakusudia kupunguza idadi ya watoto wachanga wanaozaliwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka 6000 wanaozaliwa kila mwaka kwa kuhakikisha inamfikia kila mwanamke mwenye ujauzito.

Hayo yamesemwa Januari 20, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akizindua mpango mkakati wa miaka mitano ya tafiti na mafunzo katika masuala ya afya ya jamii na lishe.

“Nchini Tanzania inakadiriwa watu milioni 1.7 wanaoishi na Virusi vya Ukimwi lakini wanaotambua hali zao za afya ni milioni 1.5 pekee, hii ni changamoto kwetu lazima tuwatafute hawa 200,000 kwani ndiyo wanaochangia maambukizi mapya bila kujua.

“Tutawapata hawa kwa kuwashauri na kuhamasisha ili wapime kupitia mtaa kwa mtaa, kata kwa kata, halmashauri kwa halmashauri lazima tuhakikishe tunamaliza ugonjwa huu Tanzania ifikapo mwaka 2030. Mpaka sasa wanaotambua hali zao ni asilimia 88, wanaotumia dawa ni asilimia 98 na waliofanikiwa kufubaza makali ya virusi ni asilimia 92,” amesema Waziri Ummy.

Amesema suala la mtoto kuzaliwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi halikubaliki.

“Matamanio ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona watoto wote wanazaliwa na afya njema pasipo virusi vya ukimwi, kaswende wala homa ya ini, hii ni changamoto kwetu lazima tuwatafute wote tuwapime na tukiwabaini tuwaingize kwenye dawa kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,” amesema.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk Donald wright amesema kati ya vipaumbele ambavyo ubalozi wa marekani umewekeza ni kusaidia tafiti za masuala ya ukimwi kupitia Usaid na mafunzo pamoja na tafiti za masuala ya afya na lishe.
 
Tafiti na huduma zinazoendelea kutolewa zinawezesha kukadiria vizuri tu.
 
Kumbe na wewe umeona usanii wao. Wacha watu wakulanenutamu bwana mambo ya kupimana ya nini alafu baadae wajinyonge mnaanza kuwalaumu
Hatuishi kwenye uhalisia.

Umetaja idadi, halafu unasema ni lazima tuwatafute.
Huwajui, lakini una taarifa za hali zao.

Inafikirisha
 
Tafiti na huduma zinazoendelea kutolewa zinawezesha kukadiria vizuri tu.

1: Ukikadiria haimaanishi wamepata.🤔

2: Unasemaje unataka kumaliza ugonjwa by 2030..., maana yake walio na maambukizi unawapeleka wapi? Unawaua/watakuwa wamekufa wenyewe/unawaponyesha??

Labda, kupunguza maambukizi mapya nayo huwezi kusema utamaliza.
 
Hiyo namba wameitoa wapi kama watu wenyewe hata hawajui hali zao za kiafya?

Anyway, tuheshimu taaluma za watu.
Mkuu, ukienda hospitali hata kupima malaria, pale maabara wanachukua sampuli yako ya damu wanakupima malaria na UKIMWI bila ya wewe kujua. Kisha watakupa majibu yako ya malaria tu na hizo taarifa za kuathirika wanazihifadhi kwaajili ya masuala ya takwimu kama hii taarifa ya watu 200k wasiojijua afya zao.
 
Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Nakubaliana na wewe kwa hili.

Unaniaminishaje kwamba idadi iliyotajwa kuwa hawajui hali zao ni kweli hawajui?
Hadithi za wale walio kwenye mpango wa dawa za kufubaza makali ya virusi tuziweke pembeni ili tujadili facts.
 
Mkuu, ukienda hospitali hata kupima malaria, pale maabara wanachukua sampuli yako ya damu wanakupima malaria na UKIMWI bila ya wewe kujua. Kisha watakupa majibu yako ya malaria tu na hizo taarifa za kuathirika wanazihifadhi kwaajili ya masuala ya takwimu kama hii taarifa ya watu 200k wasiojijua afya zao.

Matumizi mabaya ya resources ukiwaza huo mfumo, hauna maana.
Unampima mtu, unapata majibu unamwacha anaenda nyumbani. Kesho unaajili watu kwenda kumsaka/ kuwasaka???

1: Hiyo keshokutwa unamkuta ameambukiza wangapi? au

2: Kajipima vitu vingine kutafuta anaumwa nini mara ngapi? Resources?

3: Kaongeza msongamano kwenye vituo vya afya mara ngapi?

4: Wangapi wamekufa baada ya kuwapima kwa mtindo huo?

Umetumia muda wa mtu wa laboratory unaongeza kazi, unatumia vitendanishi na unatumia vitabu vya data. Unasaidikaje kama taifa?? Vifaa vyenyewe hata kuvinunua ni shida??

Si bora ungetunza mawasiliano yao?? Na huyo mtu akikushitaki kwa kumpima bila consent yake??

It's too theoretical, niambie kituo chenye data za waliopima na kwenda nyumbani kimyakimya kwa siku za hivi leo. Wakati kila anaegundulika ana HIV anatakiwa kuanza dawa.
 
Unajua siku hizi unapimwa kimya kimya kwa ambao hawapimi wanarekodi kila hospital
 
Hiyo namba wameitoa wapi kama watu wenyewe hata hawajui hali zao za kiafya?

Anyway, tuheshimu taaluma za watu.

Kuna proposals zimeshaandikwa huko.
Hakuna uhalisia hasa kwa mifumo yetu hii ya data collection, too manual with limited human resource.

Lakini pia, nature ya data zenyewe si rahisi kuzipata. Labda aweke neno tunakadilia kuwa na.........
 
Back
Top Bottom