Serikali: Watumishi 4,160 walioondolewa kwa vyeti feki warudishwa

Serikali: Watumishi 4,160 walioondolewa kwa vyeti feki warudishwa

Naibu Waziri – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Dkt. Mary Mwanjelwa amesema watumishi wa umma 4,160 kati 15,189 walioondolewa kazini kwa kuwa na vyeti vya kughushi wamerudishwa

Dkt. Mwanjelwa amesema Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kubainika kuwa Watumishi hao waliondolewa kimakosa
Katika hao, je wangapi washakufa kwa shinikizo la damu?
 
Serikali inakili kufanya makosa
Na inajipambanua zaidi kuwa ya wanyonge
 
Na mimi nilitamani niisikie hiyo kauli lakini bahati mbaya hajatoa maelezo.......RC Paul Makonda yupo kundi gani kwa maelezo ya Serikali tukufu ya JPM???
Cha ajabu hata kesi iliyofunguliwa na mstahiki meya wa Ubungo kwenye tume ya maadili ya viongozi wa umma mpaka sasa haijatolewa jibu. Kila mtu anamwogopa. Yaani wasomi wanamwogopa msomi fake
 
Acha unafiki huo umakini haujawahi kuwepo ndo maana walikuwa wanaajiri empty set

Weka jazba chini kada mtiifu...ajira za mwaka huu za walimu...zipo ajira hewa
 
Hawa maafisa utumishi waliweka figisu sana kwa chuki binafsi
 
Hovyo kabisa hawa watu!Kazi kutesa watu.

Mnastahili kushitakiwa na kuwalipa fidia wahusika.
 
Naibu Waziri – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Dkt. Mary Mwanjelwa amesema watumishi wa umma 4,160 kati 15,189 walioondolewa kazini kwa kuwa na vyeti vya kughushi wamerudishwa

Dkt. Mwanjelwa amesema Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kubainika kuwa Watumishi hao waliondolewa kimakosa

Wanajaribu kuficha ishu ya Mdude ee?
 
Wengi sana wameondolewa kazini kwa kisingizio cha vyeti feki ,lakini kuna wenye vyeti feki wako kazini mpaka leo ,mpaka wanaopokea mshahara miwili miwili wapo kazini ,Jiwe is a disgrace.
 
Mie mmachinga hapa makoroboi ila nina uncle nataka nijue Kama karudishwa
ooh, wenye kadi za " kijani "na kama ni wa kanda ya ziwa atakuwa karudishwa kazini, wengi ambao wamechinjiwa baharini inasemekana ni wale wanao jiita makamanda, wa mikoa yenye milima miwili mirefu Tanzania.
 
Rekebisha kichwa cha habari kisomeke "watumishi 4,160 walioondolewa kimakosa kwa vyeti feki warudishwa kazini"
Kichwa cha habari ni sahihi kabisa, wala kisirekebishwe.

Sababu: Walipoondolewa sababu ilikuwa vyeti feki, na watanzania wote tulipokutana na watu hao tulijua kuwa walikuwa na vyeti feki. Hivyo kichwa cha habari ni sahihi kabisa, nitakinukuu :
"Watumishi 4,160 walioodolewa kwa vyeti feki warudishwa"
Walioondolewa ni past tense, ni kilichofanyika wakati huo sio sasa.
 
Angeongeza neno walioondolewa "kimakosa"
 
Hii nayo ni gia ya Serikali kukwepa wajibu wa kutoa ajira kwa watumishi wapya , tunaomba kuona majina ya watumishi waliorejeshwa kazini
 
Safiiii serikali yangu... Utaona hata hili Chadema wataanza kupiga kelele na kulaumu, kwanini warudi kazini, yaani ni ngumu sana kuwaelewa chadema, ni ngumu sana
 
Angeongeza neno walioondolewa "kimakosa"
Hapana, walioondolewa kihalali kabisa kama ukimuamini Dr Magufuli. Kwani walifanya uhakiki si mara moja bali walirudia na kurudia na kurudia na baadae kutangaza namba ambayo serikali ilijiridhisha kuwa wana vyeti feki. Cha ajabu katika maelezo ya waziri sijasikia wala kusoma hata sentensi moja aliyosema watalipwa fidia kwa makosa ya serikali.

Na hatujui sijui ni wangapi kati ya hao tunaoaminishwa kuwa wanavyeti feki , serikali haikufanya hivyo kimakosa.

Nikueleze kitu, Zoezi zima lilifanywa kimakosa sana, wewe hujui juu ya uonevu uliofanyika hivyo hata matokeo yake yalikuwa na makosa sana. Tusubiri.
 
Computor ilikosea au Nini kilitokea mpaka usumbufu wote huo kutokea,maana wengine walikufa na plesha
. Si computer wala nini, waliorudishwa wengi wao walifanikiwa kunyofolewa vyeti fake vya f4 na defence ktk utetezi wao ikawa hawakuwahi soma sekondari!
 
jamani wengine wamepatwa na mauti kwa stress kutokana na suala hili!! itakuwaje? wapumzike kwa amani! so sad
 
Naibu Waziri ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Dr Marry Mwanjelwa amesema bungeni kwamba baada ya serikali kufanya ufutiliaji wa kina kuhusu malalamiko ya watumishi 15,189 waliokumbwa na zoezi la ukaguzi wa vyeti vya elimu mwaka 2016/17, walibaini madai ya watumishi 4,160 waliondolewa kimakosa katika mfumo wa malipoya mishahara hivyo wana haki ya kurudishwa kazini,aidha, serikali imewarejesha kwenye malipo ya watumishi hao.alisema hayo baada ya kujibu swali la Mbunge wa Musoma mjini kupitia CCM Mh Vedastus Manyinyi.
 
Back
Top Bottom