Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia inatekeleza ahadi zake kwa 100%

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia inatekeleza ahadi zake kwa 100%

powercert_Tz

Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
45
Reaction score
44
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango ameweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Ziwa Victoria kwa mji wa Tinde. Hii ni baada ya miradi mingine mikubwa ya maji kukamilika ikiwemo:

Mradi wa maji Nzega (Igunga Tabora) wenye thamani ya shilingi bilioni 6.72 umekamilika kwa asilimia 100% na wananchi wanapata maji safi.

Mradi wa maji Orkesumeti mkoani Manyara wenye thamani ya shilingi bilioni 42.36 umekamilika kwa 100% na wananchi wanapata maji safi.

Mradi wa kigoma wenye thamani ya bilioni 9 umekamilika kwa 100% na wananchi wanapata maji

Mradi wa maji kimbiji Phase 1 wenye thamani ya bilioni 12.32 umekamilika kwa asilimia 100% na wananchi wananufaika kwa maji safi

Mradi wa maji Longido mkoani Arusha wenye thamani ya shilingi bilioni 6.90 umekamilika kwa asilimia 100% na wananchi wanapata maji safi

Serikali ya awamu ya sita inatekeleza ahadi yake, kwamba mpaka kufika mwaka 2025 maji safi yatakua yanapatikana kwa 90% maeneo ya mijini na 80% maeneo ya vijijini. Kwa utekelezaji huu, ni dhahiri kwamba #mamayukokazini
 
Twende mbele turudi nyuma, ukwel usemwe, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Mama Samia Suluhu anajituma sana, hana longolongo zaidi ya matendo, sisi wa kitaa Tunaijua , mama kwa kweli anajithidi sana, pongezi kwake
 
tabora mbona maji ya visima tena mjini kati yanauzwa kwa sana, au ya ziwa victoria hayatoshi
reference -soko kuu kuna kisima pale kinauza sana maji kwa maeneo ya jirani na pia humo sokoni
barabara ya sikonge mbele kidogo ya stand ya zamani ya sikonge, mjini kabisa kuna kisima pale, kinauza maji sana tu
 
Back
Top Bottom