Camilo Cienfuegos
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 18,960
- 67,654
Tukio La Varginha (Roswell ya Brazil).
Tarehe 13 Januari 1996 Komandi Ya Anga Ya Anga Ya Amerika Kaskazini (NORAD) ilitoa tahadhari kwa majeshi ya Brazil, kwamba kuna kitu kisichotambuliwa (UFO) kilomita 300 katika anga la mji wa Sao Paulo.
Wakati jeshi la Brazil linaanza kuchukua hatua walikuwa washachelewa na wageni walishaingia kitambo sana.
Mtu wa kwanza kuona chombo kilichokuja na Aliens alikuwa Carlos de Souza.
Siku hiyo ya tarehe 13, de Souza akiwa misele na gari yake kwenye mji wa Varginha aliona kitu mithili ya sigara kikiwa kinapepesuka angani kama kimekosa uelekeo, akaanza kufuatilia baadae kikandoka kabisa.
de Souza alidhani ni ndege imeanguka hivyo akawahi kwenda kutoa msaada kwa majeruhi,
hakuamini alichokutana nacho alikuta moshi mzito na mabaki ya chombo hicho yakiwa kama aluminum huku kukiwa na harufu kali ya Sulfa na nzito kama yai, pasipokuwa na manusura wa ajali.
Kwa maelezo ya de Souza hazikupita dakika tano kabla vikosi vya jeshi la Brazil kufika eneo la tukio na kuanza kukusanya mabaki ya chombo cha 'aliens' kilichoanguka pia walimfumkuza kwenye eneo la tukio na kumpa onyo na vitisho asahau alichokiona (hizi zikiwa ni juhudi za kuzima kusambaa kwa taarifa za uwepo wa Aliens).
Hii bado ikiwa kama siri ya jeshi, wiki moja baadae Aliens walianza kuzurura katika mitaa ya mji wa Varginha.
Siku ambayo haitosahaulika ni tarehe Januari 20 1996 ambapo wasichana watatu Liliane, Valquíria na Katia walikutana Alien live mchana kweupe.
Walieza kuona kiumbe mwenye urefu kati ya futi 4 au 5, ngozi ya kuteleza, macho mekundu, kichwa chenye nundu tatu na mikono yenye vidole vitatu na harufu kali ya Salfa kama kwenye maelezo ya de Souza, pia walimwona kiumbe huyo akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa huzuni na kutaka msaada.
Hata hivyo walishtushwa na kukimbia kuenda kueleza watu wengine pia, taarifa na hofu vikawa vimeenea sio Varginha tu ni Brazil kwa ujumla.
Watu waliendelea kuhisi usalama wao ni mdogo kwasababu aliens wapo kwa mtaa wanazurura tu, jeshi nalo likaendelea kukaza doria Varginha nzima, ikiwa ni oparesheni ya kijeshi.
Wakati oparesheni ya kijeshi ikiendelea askari wawili Eric Lopes na Marco Chereze wakiwa na gari walifanikiwa kukutana na Alien mmoja. Marco Chereze aliamua kumbeba na kumwingiza ndani ya gari.
Lakini katika harakati za kumkamata Chereze aling'atwa na alien kwenye bega na kumsababishia ugonjwa usiotibika wiki mbili baadae Chereze alikufa na kuzikwa bila ndugu kushiriki maana hakuna aliyeruhusiwa, kimyakimya na haraka haraka.
Inaelezwa kwenye oparesheni 'kamata aliens' jeshi la Brazil lilifanikiwa kukamata aliens wawili.
Na kila walipokuwa wakiwa kamata waliwapeleka hospitali kuwafanyia x-rays ila madaktari waliambiwa wajifanye hawajaona kitu au wakijifanya wajuaji wapotezwa, full vitisho.
Wakati haya yote yakiendelea ndege ya USAF yaani U.S Air Force ilionekana maeneo karibu na Varginha, baadae inaelezwa aliens waliokamatwa na jeshi la Brazil walichukuliwa na USAF mpaka Marekani, 'kwa wenye mali wenyewe'.
Baada ya aliens kusafirishwa Marekani, serikali ya Brazil ilibaki ikitoa 'ufafanuzi', yote hiyo ni kupoteza maboya watu wasielewe nini kinaendelea.
Kuna muda maafisa wa jeshi walipigwa maswali mpaka sukari ikipanda.
Mfano serikali ya Brazil ilieleza wale wasichana watatu yaani Liliane, Valquíria na Katia hawakuona alien waliyemuona ni Mudinho, Mudinho alikuwa mtu mwenye matatizo ya akili na mapozi kama ya alien aliyeonekana.
Katika suala la hospitali serikali ilieleza kule hospitali walikuwa ni mbilikimo anajifungua wanamsaidia na sio aliens.😁 (Watu sio wajinga bwana).
Pia mama wa wale wasichana watatu alileza kujiwa na watu wa suti nyeusi wakiwataka madogo wanyamaze kimya wapewe briefcase 💼 lenye mapene au wabadilishe stori, bimkubwa akagoma.
Kutokana na wasiwasi mashahidi wengi wa tukio la Varginha waliingia mitini hawakutaka kusema chochote.
Kwenye documentary ya Moment of Contact ya James Fox ya mwaka 2022 hapa baadhi ya mashuhuda wameelezea tena baada ya miaka 26 ikiwemo madaktari walio wafanyia x-ray aliens.
Pia Eric Lopes aliyekuwa na Chereze ameongea japo bado alikuwa na wasiwasi.
Pamoja na tukio hilo kufichwa sana na serikali ya Brazil na Marekani bado linabaki alama kwenye mji wa Varginha. Pia linabaki kama tukio lenye kukumbukwa zaidi baada ya lile la Roswell Marekani 1947.
Nakushauri angalia documentary ya Moment of Contact, kuna mambo mengi yameelezwa humo.
Katika mji wa Varginha kuna sanamu, vinyago na ishara za kuonyesha kukumbusha tukio la ujio wa aliens.