Serikali ya CCM haifurahi ukiwa na kiasi kikubwa cha fedha benki, unafilisiwa kwa kupewa kesi ya Uhujumu Uchumi

Salaam Wakuu,

Nmeanza kuelewa kwanini Matajiri wengi wa Tanzania wanaficha fedha zao nje ya Nchi. Siwalaumu tena. Na kama hii hali ikiendelea, Benki nyingi zitatikisika kiuchumi kwani watu watasusa kupeleka hela.

Zamani Watanzania wengi walikuwa hawapeleki fedha zao benki. Walikuwa wanazichimbia mashambani na wengine kuzilalia kwenye Vitanda vya Kamba. Hii walikuwa wanafanya kwa kuhofia kunyang'anywa fedha zao na Serikali. Mabenki yalifanya Kampeni kubwa kuwabembeleza watu wapeleke fedha benki na Wakafanikiwa.

Hii hali sasa imerudi kwa kasi hivi Karibuni. Nini kinafanyika?

1. Wanafuatilia benki una kiasi gani, Wakikuta hela ni nyingi Wanazizuia, Ukienda kutoa hazitoki wanakuambia zinafanyiwa Uchunguzi.

2. Wanabuni mbinu watazipataje hizo hela, hivyo ramani inachorwa ya kuzipata kwa kuangalia makando kando yako. eidha unaweza ambiwa:
i) Unamiliki fedha zisizoendana na Kipato chajo
ii) Hujalipia kodi, au umepata kwa Udanganyifu.

3. Utakamatwa na kufunguliwa kesi isiyo na dhamana Uhujumu Uchumi.
i) Utakatishaji fedha
ii) Kuongoza genge la Uharifu
iii) Kukwepa kodi nk

4. Unalazimishwa uonge nao mfanye Makubaliano ni kiasi gani cha fedha utawapa ili Uachiliwe huru

5. Unalazimishwa ukiri kosa halafu Unapigwa faini na fedha zako zinachukuliwa. Faini haizidi fedha ulizo nazo, wanazijua hivyo wanajua utalipa tu.

Baada ya hapo Wanakuachia huru unaendelea na kazi zako. Unaanza upya kujitafutia kipato, kikiongezeka Mzunguko unaanza tena hapo kwenye maelezo namba moja.

Hakika aduni wa Mtanzania ni Mtanzania.

Hapa chini naweka Mifano Michache ya Watu waliochezewa hii style ya kunyang'anya watu fedha zao ukiachilia mbali Tariq Machibya maarufu Mr Kuku.

1. Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Ndugu Erick Kabendera

2. Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika

3. Wafanyabiashara saba wa mafuta wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya SHIN UP Tanzania limited Zhang Zhi XIN, LINCOLN

4. Mkurugenzi mkuu wa Benki M Tanzania, Sanjeev Kumar

5. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura

6. Astery Ndege aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers

7. Mfanyabiashara Daniel Chizua aliyedaiwa kukutwa na Kobe Wawili

8. Raia wa China, Liang Hu aliyedaiwa kuua Tembo 511

9. MKURUGENZI wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet

10. Wafanyabiashara Noah Mmasanga, Richard Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo na wengine wengi.

Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.

Je, ni lini Tutapata Mabilionea Wapya sababu Waliopo Wanazidi kuaga dunia.

Nashauri wachunguzi wa mambo wafanyie kazi Vifo vya hawa Matajiri wa Kitanzania ambao wamekufa kwa kufuatana . Isijekuwa ni hela zao zimewatoa roho. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi Subhash Patel, Mr Reginald Mengi, Dr Rajni Kanabar, Ali Mufuruki, Salim Hassan Turky, Mr Salum Shamte nk.

Hongera kwa kutengeneza fitna na serikali, utafanikiwa sana kwa wasio fanya biashara. Kwa wafanya biashara tunakucheka tuu.

FANYA BIASHARA LIPA KODI STAHIKI.
 
Popote pale hapa duniani huwezi kuwa na pesa bila kuwa na chanzo kinachoonyesha kwamba pesa hiyo umelipia kodi. Mengine yoyote ni majungu tu. Unapokuwa umelipa kodi stahiki hakuna atakaye kusumbua popote pale duniani. Hakuna hata nchi moja ambayo haifanyi hivyo.

Lipa kodi utabaki kuwa salama, wacha kulipa kodi utalia na kusaga meno.
 
Ja
Tutaanza kuzichimbia ndani Tena chumbani, tunachimba shimo chumbani chini ya uvungu wa kitanda na kuweka cement na chuma hafu tunapiga kufuli. Hakuna atakaye jua.
Hahaaa umenifurahisha utafikiria ni mazuri
Mkuu tafuta safe box yapo kila Aina na bei rahisi unaweza kuliweka hata ukutani kwa kificho
Ukalitumia kuhifadhi fedha, hati zako muhimu Kama za viwanja, kadi za magari, document nyingine nyeti hata silaha za moto kama pistol
 
Matajiri kua km mashetani na masikini kua km malaika...
Hizi principle za uchumi zipo ktk nchi ya majuha tu....
 
Usifikiri ni utani.

Leo hii ukipata tu hela nyingi, fikiria mara mbili kabla hujapeleka bank.

Kuna wakati nililkuwa nalipwa mshahara wa dola 9,000 kwa mwezi. Nilikuwa nimeajiriwa nje ya nchi lakini niliomba mshahara wangu ulipwe kwenye akaunti yangu ya nyumbani hapa Tanzania.

Niliporudi likizo, kutaka kuchukua hela, nikaambiwa nikamwone manager wa branch. Baadaye nilifanikiwa lakini baada ya kupeleka documents za mkataba, work permit, nakala ya dicuments za kodi za nchi nilikokuwa nafanya kazi, n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yako nahisi ni kwa ajili ya mambo ya 'money laundering'/utakatishaji fedha

usingethibitisha zilikotoka ungeenda ndani bila shaka
 
Inaumiza sana,

Yaani unatesa wafanyabiashara kwa kupora mitaji yao sijui wakiisha serikali nayo itaanza kujitoza kodi kwenye asset zake.....!
 
Ela ni kama first law of thermodynamic inayohusiana sana na principle of energy conservation! Inasema energy is neither created nor destroyed. Lakini inaweza kubadilishwa. Ela hivyo, hivyo ukiona umepata kiasi cha ela ujue kuna mwingine kakosa/poteza ela hiyo hiyo! Vinginevyo uwe muumba pesa!

Hicho ni kibwagizo.
====
Paskali amezungumza sana habari za karma!! Mnapojadili mada hii, basi na suala la karma mnlizingatie.
 
Salaam Wakuu,

Nmeanza kuelewa kwanini Matajiri wengi wa Tanzania wanaficha fedha zao nje ya Nchi. Siwalaumu tena. Na kama hii hali ikiendelea, Benki nyingi zitatikisika kiuchumi kwani watu watasusa kupeleka hela.

Zamani Watanzania wengi walikuwa hawapeleki fedha zao benki. Walikuwa wanazichimbia mashambani na wengine kuzilalia kwenye Vitanda vya Kamba. Hii walikuwa wanafanya kwa kuhofia kunyang'anywa fedha zao na Serikali. Mabenki yalifanya Kampeni kubwa kuwabembeleza watu wapeleke fedha benki na Wakafanikiwa.

Hii hali sasa imerudi kwa kasi hivi Karibuni. Nini kinafanyika?

1. Wanafuatilia benki una kiasi gani, Wakikuta hela ni nyingi Wanazizuia, Ukienda kutoa hazitoki wanakuambia zinafanyiwa Uchunguzi.

2. Wanabuni mbinu watazipataje hizo hela, hivyo ramani inachorwa ya kuzipata kwa kuangalia makando kando yako. eidha unaweza ambiwa:
i) Unamiliki fedha zisizoendana na Kipato chajo
ii) Hujalipia kodi, au umepata kwa Udanganyifu.

3. Utakamatwa na kufunguliwa kesi isiyo na dhamana Uhujumu Uchumi.
i) Utakatishaji fedha
ii) Kuongoza genge la Uharifu
iii) Kukwepa kodi nk

4. Unalazimishwa uonge nao mfanye Makubaliano ni kiasi gani cha fedha utawapa ili Uachiliwe huru

5. Unalazimishwa ukiri kosa halafu Unapigwa faini na fedha zako zinachukuliwa. Faini haizidi fedha ulizo nazo, wanazijua hivyo wanajua utalipa tu.

Baada ya hapo Wanakuachia huru unaendelea na kazi zako. Unaanza upya kujitafutia kipato, kikiongezeka Mzunguko unaanza tena hapo kwenye maelezo namba moja.

Hakika aduni wa Mtanzania ni Mtanzania.

Hapa chini naweka Mifano Michache ya Watu waliochezewa hii style ya kunyang'anya watu fedha zao ukiachilia mbali Tariq Machibya maarufu Mr Kuku.

1. Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Ndugu Erick Kabendera

2. Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika

3. Wafanyabiashara saba wa mafuta wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya SHIN UP Tanzania limited Zhang Zhi XIN, LINCOLN

4. Mkurugenzi mkuu wa Benki M Tanzania, Sanjeev Kumar

5. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura

6. Astery Ndege aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers

7. Mfanyabiashara Daniel Chizua aliyedaiwa kukutwa na Kobe Wawili

8. Raia wa China, Liang Hu aliyedaiwa kuua Tembo 511

9. MKURUGENZI wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet

10. Wafanyabiashara Noah Mmasanga, Richard Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo na wengine wengi.

Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.

Je, ni lini Tutapata Mabilionea Wapya sababu Waliopo Wanazidi kuaga dunia.

Nashauri wachunguzi wa mambo wafanyie kazi Vifo vya hawa Matajiri wa Kitanzania ambao wamekufa kwa kufuatana . Isijekuwa ni hela zao zimewatoa roho. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi Subhash Patel, Mr Reginald Mengi, Dr Rajni Kanabar, Ali Mufuruki, Salim Hassan Turky, Mr Salum Shamte nk.

Bank siyo mahala salama pa kuweka pesa tena kwani hata TRA vinara wa Rushwa huwafungia Account zao wafanyabiashara kienyeji kwa njia haramu za kishetani, kuna mbinu mpya hufanywa na Baadhi ya mameneja wa Bank wasiokuwa waaminifu ambao huwapa siri za wateja wenye pesa nyingi kisha kutengeneza mazingira ya kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi, Benk zinaenda kufirisika kwani wafanyabiashara wakubwa sasa wamehamishia pesa zao kenya Uganda Zambia kusiko na usumbufu wa pesa za mtu
 
Ela ni kama first law of thermodynamic inayohusiana sana na principle of energy conservation! Inasema energy is neither created nor destroyed. Lakini inaweza kubadilishwa. Ela hivyo, hivyo ukiona umepata kiasi cha ela ujue kuna mwingine kakosa/poteza ela hiyo hiyo! Vinginevyo uwe muumba pesa!

Hicho ni kibwagizo.
====
Paskali amezungumza sana habari za karma!! Mnapojadili mada hii, basi na suala la karma mnlizingatie.

Karma itatembea kwenye familia yake Kama inavyotembea kwenye familia za wajamaa wale ukikutwa na colgate sabuni ya ayu au yolanda unapewa uhujumu uchumi Zama za Giza
 
Back
Top Bottom