Hiki siyo kigezo cha kuwapora watu pesa zao kienyeji kishamba kwa njia haramu za kishetani, watu wanalipa kodi pesa zao halali lakini bado TRA mnawabambikia VAT hewa kodi kubwa kufunga Account zao kihuni kwa Takwimu za kupika kutengeneza kihuni tu, acha kutetea wizi wa pesa za watu kwa visingizio vya kipumbavu
Hizi mambo asili yake rwanda.M7 hana hizi yeye ugomvi wake ni kumtoa kitini.
Ug awaulizi ulipo pata pesa Wala kuchungulia akaunti yako we wekeza tu.M7 asomeshi namba watu wake alipata nchi kwa mtutu na sio kupita bila kupingwa.
Hizi mambo asili yake rwanda.M7 hana hizi yeye ugomvi wake ni kumtoa kitini.
Ug awaulizi ulipo pata pesa Wala kuchungulia akaunti yako we wekeza tu.M7 asomeshi namba watu wake alipata nchi kwa mtutu na sio kupita bila kupingwa.
Nchi zingine hata ulaya watumishi wa umma hutumia magari ya kawaida tu isipokuwa wale viongozi wakuu tu, Tanzania ndiyo Taifa hutumia gharama kubwa kununua magari ya Toyota V8 kwa kila mkuu wa mkoa, wilaya, katibu Tawala, wakurugenzi mameya, makatibu wakuu, mawaziri, wakati Rwanda wao waziri hukopeshwa Gari
Weka kenya Uganda Zambia ambapo hawana usumbufu kama wa BOT kisha unaenda kuchukua unapita panya road mipaka bubu ipo mingi unarudi Tanzania unakula pesa zako bila kelele
Mabenk ya Nchi jirani sasa yanasitawi kwa pesa za watanzania waliokosa imani na mabenk ya Tanzania kutokana na usumbufu wa TRA kufunga Account kihuni kienyeji kwa njia haramu za kishetani na pia vyombo vingine kuwabambikia kesi za utakatishaji fedha uhujumu uchumi wafanyabiashara kwa nia ya kuwapora pesa zao kienyeji kishamba kwa njia haramu.
naomba niongelee tukio nililosimuliwa na mshkaji wangu funzi ujenzi....
wale wa mwanza mnapajua eneo la nyamongolo musoma road kuna jamaa alikuwa anaporomosha bonge la jumba kiukweli ingawa mitaa ile kuna nyumba nzuri mpyampya ila ya jamaa ni tamu sana
sasa kumbe siku moja jamaa wakapita,kwa mujibu wa fundi alisema ni TRA...wakawauliza maswali ghorofa la nani ikabidi contacts zitolewe,boss akaendewa hewani maswali ya kutosha tu ikiwepo unafanya biashara gani, Tin number yako ni ipi...bla bla blaaa
Jamaa anakuambia baada ya siku 2 ujenzi ulisimama kwa muda usiojulikana na kuwaathiri sababu hata malipo ya jamaa yalikuwa mazuri sana hadi msosi wa uhakika walikuwa wanaletewa site
Bila shaka hata mama ntilie walikiona ch amoto,mafundi,ma supplier wa vifaa vya ujenzi,madereva....
sad....
Serikali hii ukitaka wakupende ,we Jenga nyumba ya nyasi tu wanafurahia sana, na tunakoelekea wataanza kuchunguza vyakula tunavyokula,utatakiwa kula ugali tembele ,ukila wali nyama mixa madikodiko na peps baridi tra wanakuhusu
Wamekufa baada ya TRA kufunga Account zao kienyeji kwa njia haramu za kishetani na kisha vyombo vingine kuwatishia kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi,
Serikali hii ukitaka wakupende ,we Jenga nyumba ya nyasi tu wanafurahia sana, na tunakoelekea wataanza kuchunguza vyakula tunavyokula,utatakiwa kula ugali tembele ,ukila wali nyama mixa madikodiko na peps baridi tra wanakuhusu
Nunua dola weka ndani mapesa ya madafu nayo hayaaminiki kukaa nayo mengi ndani.
sasa hivi benki sio salama kuweka fedha tena!
Au nunua ardhi ni salama zaidi kuliko kuweka fedha ndani au benki.
Inatia hasira sana hii,ma DC, RC ,wakurugenzi,mawaziri nk wao ruksa kufanya chochote,ila wavuja jasho ambao hata hawajui mitaji wameipataje wanahenyeshwa sana
Tutaanza kuzichimbia ndani Tena chumbani, tunachimba shimo chumbani chini ya uvungu wa kitanda na kuweka cement na chuma hafu tunapiga kufuli. Hakuna atakaye jua.
Hivi nyie mlikuwa mnaweka pesa zenu nyingi Benki? Benki huwekwa pesa ndogo ndogo tu, kama 1milioni mpaka 50 milioni. Zaidi ya hapo tafuta pahala pengine pa kuweka.
Nmeanza kuelewa kwanini Matajiri wengi wa Tanzania wanaficha fedha zao nje ya Nchi. Siwalaumu tena. Na kama hii hali ikiendelea, Benki nyingi zitatikisika kiuchumi kwani watu watasusa kupeleka hela.
Zamani Watanzania wengi walikuwa hawapeleki fedha zao benki. Walikuwa wanazichimbia mashambani na wengine kuzilalia kwenye Vitanda vya Kamba. Hii walikuwa wanafanya kwa kuhofia kunyang'anywa fedha zao na Serikali. Mabenki yalifanya Kampeni kubwa kuwabembeleza watu wapeleke fedha benki na Wakafanikiwa.
Hii hali sasa imerudi kwa kasi hivi Karibuni. Nini kinafanyika?
1. Wanafuatilia benki una kiasi gani, Wakikuta hela ni nyingi Wanazizuia, Ukienda kutoa hazitoki wanakuambia zinafanyiwa Uchunguzi.
2. Wanabuni mbinu watazipataje hizo hela, hivyo ramani inachorwa ya kuzipata kwa kuangalia makando kando yako. eidha unaweza ambiwa:
i) Unamiliki fedha zisizoendana na Kipato chajo
ii) Hujalipia kodi, au umepata kwa Udanganyifu.
3. Utakamatwa na kufunguliwa kesi isiyo na dhamana Uhujumu Uchumi.
i) Utakatishaji fedha
ii) Kuongoza genge la Uharifu
iii) Kukwepa kodi nk
4. Unalazimishwa uonge nao mfanye Makubaliano ni kiasi gani cha fedha utawapa ili Uachiliwe huru
5. Unalazimishwa ukiri kosa halafu Unapigwa faini na fedha zako zinachukuliwa. Faini haizidi fedha ulizo nazo, wanazijua hivyo wanajua utalipa tu.
Baada ya hapo Wanakuachia huru unaendelea na kazi zako. Unaanza upya kujitafutia kipato, kikiongezeka Mzunguko unaanza tena hapo kwenye maelezo namba moja.
Hakika aduni wa Mtanzania ni Mtanzania.
Hapa chini naweka Mifano Michache ya Watu waliochezewa hii style ya kunyang'anya watu fedha zao ukiachilia mbali Tariq Machibya maarufu Mr Kuku.
1. Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Ndugu Erick Kabendera
2. Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika
3. Wafanyabiashara saba wa mafuta wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya SHIN UP Tanzania limited Zhang Zhi XIN, LINCOLN
4. Mkurugenzi mkuu wa Benki M Tanzania, Sanjeev Kumar
5. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura
6. Astery Ndege aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers
7. Mfanyabiashara Daniel Chizua aliyedaiwa kukutwa na Kobe Wawili
8. Raia wa China, Liang Hu aliyedaiwa kuua Tembo 511
9. MKURUGENZI wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet
10. Wafanyabiashara Noah Mmasanga, Richard Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo na wengine wengi.
Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.
Je, ni lini Tutapata Mabilionea Wapya sababu Waliopo Wanazidi kuaga dunia.
Nashauri wachunguzi wa mambo wafanyie kazi Vifo vya hawa Matajiri wa Kitanzania ambao wamekufa kwa kufuatana . Isijekuwa ni hela zao zimewatoa roho. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi Subhash Patel, Mr Reginald Mengi, Dr Rajni Kanabar, Ali Mufuruki, Salim Hassan Turky, Mr Salum Shamte nk.
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE UTANGULIZII 1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi...
Zanzimana sio mtu kabisaaa , yaani Ni jizi la hatari , uchawi , lenyewe , dhulumati , roho mbaya lenyewe sijui Lina nini shamba na Limbukeni la kutupa .
Kama naiona nchi ya Kenya ikienda kunufaika na mapesa ya watanzania yatakayoanza kumiminika kwenye mabank yao.
Maana hawa majiniwatu wakishamalizana na wenye million 100 and above watashuka mpaka na wenye < tsh milioni 1.
Nchi imevamiwa hii, mtawala kichaa anataka watu wawe mafukara ili awahonge chumvi na vijikanga wakati wa kampeni lakini akae akitambua dunia imebadilika sana hawezi kutufirisi huku tukimuangalia tu.
Kinachompa kiburi ni hirizi na matambiko anayojifanyia kila mwezi sijui anafikiri yeye ndie anaeujua uchawi kuliko akina Mobutu na the like.
TRA na Huyo waziri wao wa fedha wakae wakijua sasa dunia inaendeshwa na teknolojia soon mwakani kutakuwa na digital yuan,digital Euro,digital ksh nk amabazo zitahifadhiwa kwenye software wallets na ukumbuke hizi zitakuwa ni borderless kwahiyo hata sisi tutaweza kuzitumia
Kama naiona shilingi ya Tanzania ikenda sifuri mud mfupi ujao maana siku hizi hakuna anaetaka ujinga na ujuha kama wa hili liserikali la kiuwendawazimu na kishetani
Unatakiwa kuelewa kodi ni nini na aina za kodi. Unaweza kuwa na fedha nyingi benki lakini kusiwe na uhitaji wa kulipa kodi. Kwa maoni yangu naisihi serikali kupitia TRA iachane na huu mtindo wa kuzuia account. Hakuna kazi kubwa kama kuwafanya raia waamini bank.
Tuliletewa barua na BOT yakureporty kila mteja wetu anayeleta cash nyingi mara kwa mara. Majina yatumwe Bot nikataka kushare hiyo barua hapa miezi ile ya sita na saba lakini nikasita.
Kwa kifupi kla mteja analeta cash nyingi tunatuma jina
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.