Serikali ya CCM kutoka kupambana na vyama pinzani hadi kupambana na Gen z

Serikali ya CCM kutoka kupambana na vyama pinzani hadi kupambana na Gen z

BiancaEA

Member
Joined
Nov 23, 2025
Posts
41
Reaction score
80
Miaka ya nyuma Serikali ilikuwa ikipambana kuzuia maandamano ya baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani.

Polisi wake walikuwa na kazi ya kuvamia venue wanazokutaniana wanasiasa kufanya shughuli za kisiasa na kuwasweka mahabusu na hata kuwafungulia kesi.

Walikuwa na uwezo wa kukamata kamata viongozi na waratibu wa maandamano kwa sababu walikuwa wanawafahamu kupitia vyama vyao.

Safari hii wale viongozi wa upinzani waliokuwa wakiwakamata hawapo tena wamebaki kupambana na millennials na Gen z ambao wengi wao sio wafuasi wa vyama vya siasa, shughuli zao rasmi hazijulikani, address zao hazijulikani na hata viongozi wao hawajulikani. Hii ni hatari.

Serikali imebaki kujidanganya kwa kuwazimia internet kwa sababu ndio inayowarahisishia mawasiliano kwa kuratibu na kuhamasisha maandamano, hii ni kutokana na kukandamizwa kwa vyama vya siasa, vyombo vya habari, kukandamizwa kwa wanaharakati na watetezi wote wa shughuli zinazoitaka serikali kutii haki za binadamu na utawala bora na kuwajibika kwa wananchi.

Sasa hivi internet imeanza kuwa mbovu kwa kupunguziwa kasi, serikali ikae ikijua kuzima interent hakuzuii maandamano wala kuathiri shughuli za Gen z pekee, ni watu wote wanaathirika na kudhorotesha shughuli za kijamii, kiuchumi na kisiasa kuanzia watoto hadi wazee, wazawa na wageni, matajiri kwa masikini.
 
Back
Top Bottom