Serikali ya China yalaumu wahitimu wa vyuo vikuu kwamba ni wavivu, wabishi, hawataki kazi ngumu

Uko sahihi, wakisema elimu haina maana Hawa vijana hawatasomesha watoto wao na hilo litakuwa pigo kwa Taifa Kama China.

Yaani shule ni Jela ndogo,
Uvae masare,
Uchapwe viboko,
Ulimitiwe muda,
Bado ukariri mavitu
Sijui ufanye mitihani.
Yote unavumilia kwani mvumilivu hula mbivu, Kupata kazi nzuri na Mshahara mnono.
Alafu mwisho wa siku usipate kitu, pumbavu. Huo ni Utapeli
 
Sasaa mnataka mtu amalize law-School afu aende shambani akalime…. Non sence.
 
Hivi MTU ajipinde Usiku na Mchana kusoma alafu uje umpe kazi ngumu? Hao wanaotoa lawama ni wapumbavu.

Vijana walisoma ili wafanye kazi za maana, usomi ni Kwa Watu wavivu wasiotaka kazi ngumu naza kuvuja jasho.
Ukitumia nguvu nyingi kusoma ujue huna akili.
 
Pale tulipogeuza Elimu kuwa chanzo cha kipato ndipo tulipokosea.

Elimu maana yake ni kujipatia maarifa ya mambo ambayo huyafahamu ili kukabiliana na mazingira yanayokuzunguka..

Sasa endapo elimu inaweza kumuwezesha mtu kupata kipato hilo ni jambo lingine tofauti.
Yaani upate maarifa ambayo hayawezi kukupatia kipato? Acha utani basi.
 
Oh, kumbe tunasoma ili tupate pesa, mie nikajua tunasoma tupate maarifa ya utambuzi wa mazingira yanayotuzunguka, na kujipatia kipato ni component moja tu ndani ya uwanda mpana wa impact ya maarifa kwa mwanadamu.
 
Ingekuwa elimu ni kwa ajili ya utambuzi na sio kipato, basi shule zingekuwa na wanafunzi wachache sana.
 
Kutokana na kuongezeka kwa tatizo la ukosefu wa ajira, Serikali ya China imewaangushia wahitimu wa vyuo vikuu zigo la lawama kwamba ni wavivu, wabishi na hawataki kazi ngumu za shambani.

Hii ni kutokana na kwamba wahitimu wengi hawataki kurudi makwao vijijini kwa wazazi wako wakashiriki kazi za shamba ama kilimo, wanakatalia mjini.

Marekani wao wanasema kizazi cha wasomi wa sasa ni wabishi, wajuaji na hawana nidhamu.

=====

Beijing | China is shifting the blame for surging youth unemployment on to jobless university graduates, accusing them of refusing to put aside their professional ambitions and take on manual labour.

In recent weeks, state broadcasters and news agencies have published more than a dozen profiles of recent university graduates who allegedly made a fortune in low-skilled jobs such as selling street food or growing fruit, rather than pursuing a career in their area of study.

Zaidi soma=> Hapa
Wachina wenyewe wako Tiktok kuchapana minati ya midomo
 
Ingekuwa elimu ni kwa ajili ya utambuzi na sio kipato, basi shule zingekuwa na wanafunzi wachache sana.
Namanisha si kwamba elimu haiwezi kumsaidia mtu kujipatia kipato, ila kujipatia kipato ni component moja tu kati ya kapu lililobeba components nyingi. Sasa watu tumeacha mambo mengine na ku-focus kwenye kitu kimoja tu na kudhani tunasoma ili kupata pesa. Na vipi sasa ambao hawajasoma hayo ma-degree, hawapati hivyo vipato? Kwahiyo mtu anaweza kupata kipato bila hata kusoma hizo degree, na si lazima upate kipato ukiwanazo hizo degree. Na unaweza kutangulia kupata kipato kisha elimu ikafuatia baadae.

Mfano: Kati ya kupata maarifa ya kutatua changamoto flani katika jamii na kipato, ni njia ya kutatua hiyo changamoto kwa kutafuta maarifa ndio ilitangulia, kisha watu wakaona ili kutoa compensation ya muda wa huyu mtu anayetutatulia haya matatizo basi tumpe kipato.
 
Mkuu sibishi usemacho, lakini umejikita kwenye mtazamo wa kinadharia zaidi kuliko uhalisia. Uhalisia ni kuwa watu wanasoma ili wapate maarifa yatakayowawezesha kupata kipato. Hao wanaosoma tu ili wapate maarifa fulani ya kutatulia changamoto zinazowazunguka ni wachache mno, na sehemu kubwa huwa wameshajitosheleza kimapato, au wanapewa ufadhili kutoka watu ama taasisi mbalimbali. Hizo nyingine ni mbwembwe tu kaka yangu.
 
Sawa Mkuu "Tindo"
 
In the future people will be paid basic universal income due to Artificial intelligence said elon musk in one of his interview.
 
Back
Top Bottom