Serikali ya kata ya Kalobe jijini Mbeya imeshindwa kuwajali wananchi wake wanaotumia uwanja wa Kalobe shule ya msingi kufanya mazoezi

Serikali ya kata ya Kalobe jijini Mbeya imeshindwa kuwajali wananchi wake wanaotumia uwanja wa Kalobe shule ya msingi kufanya mazoezi

A

Anonymous

Guest
Mnamo tarehe 14/2/2024 wananchi wa mtaa wa Kalobe wanaotumia uwanja wa Kalobe walipeleka malalamiko kuhusiana na uwanja wao kuaribiwa na watu wanaotumia barabara ya Kalobe kuenda itende kupita uwanjani kwao. Na kuaribu mazingira ya uwanja huo mmoja unaotumiwa na mtaa mzima vijana waliongea na Serikali ya mtaa na kuomba kusawaidia barabara irekebishwe sehemu chache zenye matatizo ili watu hawa waweze kupita kwenye barabara yao na waache kupita uwanjani. Vijana baada ya kuona hakuna msaada wanaopata wakaona warekebishe wenyewe ili uwanja wao usiaribike zaidi.

Wiki iliyopita vijana wa mtaa huo walijikuta katika wakati mgumu zaidi baada ya vijana hao kukuta magari yote yanayotumia njia kuu kupita uwanjani kwao jambo ambalo lilisababisha taharuki kati ya vijana ao na serikali ya mtaa hii ilitoka ni baada ya serikali ya mtaa kuchimba mtalo katikati ya barabara na kuzuia magari kuenda upande wapili.

Vijana walifanya jitihada kuongea na diwani wa mtaa na mtendaji wa mtaa wa DDC na kumueleza kero yao mtendaji aliishia kusema kuwa hajui jambo linaloendelea.

Vijana hao hawakuishia hapo walipeleka malalamiko yao kwa mtendaji wa kata. Jambo linalo sikitisha nikuwa huu uwanja unatumiwa na shule zote za msingi na sekondari kuchezea michezo yao kwasababu shule zao hazina uwanja wa mpira wa miguu.

Vijana wamejikuta wakipata shida wakati wa mazoezi yao kwakuwa wanacheza sehemu ambayo wanapisha na vyombo vya moto.
 
Back
Top Bottom