Serikali ya Kenya yaburuzwa mahakamani kwa kukosekana uwazi mradi wa SGR

Serikali ya Kenya yaburuzwa mahakamani kwa kukosekana uwazi mradi wa SGR

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Asasi ya Kiraia ya Okoa Mombasa ikishirikiana na Taasisi ya Uwajibikaji wa Kijamii (TISA) wameiburuza Serikali ya Kenya mahakamani kudai kuwekwa wazi kwa mikataba ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Mombasa - Nairobi ya Standard Gauge Railway (SGR).

Mashirika hayo mawili yanadai serikali iweke wazi mikataba yote pamoja na utafiti uliofanywa wakati wa ujenzi na uendeshaji wa reli hiyo.

Mashtaka haya dhidi ya serikali yamechochewa na matokeo hasi ya reli hiyo kwa uchumi wa eneo la Pwani ya Kenya, huku kukiwa na hoja kuwa Katiba inazuia mikataba ya miradi ya umma kuwekwa siri, na kukosa ushirikishwaji wa umma katika fedha za mradi huo.

Uamuzi wa Serikali wa mwaka 2019 uliolazimu kontena za mizigo kwenda bara kutoka bandari ya Mombasa kusafirishwa kupitia reli ya SGR ulisababisha makampuni mengi kuhamisha operesheni zake na kusababisha kudorora kwa uchumi unaohusishwa na bandari hiyo.

Muungano huo umewahi kuomba kupatiwa nyaraka za taarifa katika baadhi ya ofisi za serikali mwaka 2019 bila mafanikio yoyote.

“Kutokana na serikali kushindwa kutujibu, Okoa Mombasa imefungua kesi Mahakama Kuu ya Kenya kudai haki ya kupata taarifa. Tunaamini kushindwa kutoa taarifa kama inavyoelezwa na Katiba ni kukiuka haki yetu ya kupata taarifa na ushiriki wa umma,” taasisi hizo zilieleza.

Chanzo: Citizen Digital

1624358139188.png
 
Back
Top Bottom