Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Wakuu,
Mambo yameendelea kuwa sukari kwenye hili sakata la Tanzania na Kenya. Yaani inaonekana kuwa Serikali ya Kenya ime-align na serikali ya Tanzania kwenye hili suala la CHADEMA na Martha Karua.
Yaani hizi serikali za kiafrika zinafanana wakuu!
===============================================
Msemaji wa serikali ya Kenya Isaac Mwaura amesema Tanzania imetenda kwa mujibu wa haki yake ya uhuru kwa kuwazuia watu kadhaa wa kisiasa na wanaharakati wa Kenya, wakiongozwa na Martha Karua na kwamba Kenya haikuwa na jukumu katika uamuzi huo.
Mwaura ameyasema hayo leo wakati akijibu kuhusu hatua ya kiongozi wa Chama cha Ukombozi wa Watu, Martha Karua, aliyekuwa Jaji Mkuu Willy Mutunga, na wanaharakati wengine wanne kuzuiwa kuingia Tanzania juzi.
Inaelezwa kuwa Mather na wenzake walitaka kuingia nchini kwa lengo la kwenda kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu ambayo inaendelea kusikilizwa kwatika mahakama ya kisutu mkoani Dar es Salaam.
“Ikiwa serikali ya moja ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki itaamua kumkataa mtu binafsi kuingia nchini mwao, ina mamlaka ya kufanya hivyo,” Mwaura amesema.
Amesisitiza kuwa serikali ya Kenya inaheshimu uhuru wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na haiingilii maamuzi yao ya ndani.
“Ikiwa wameamua hivyo, huo ni uamuzi wao. Hatujui kwa nini watamzuia mtu, na serikali ya Kenya haihusiki,” amesema.
Source: Citizen Digital