Serikali ya Kenya Yatangaza Hali ya Hatari (Civil Danger)Yaamrisha Rasmi Jeshi la kenya (KDF) Kuingia Mtaani na Kutuliza Raia Wanaofanya maandamano

Kwa hali ilivyofikia, akisimama Odinga nakusema takbir/Su kwisha habari 😁😁
Kunoga zaidi Ruto anaowatuhumu wanaanzishaga maandamano hawapo na hawa comments chochote
Kifupi hana wakumbebesha lawama Sasa😂😂😂
 
Kenya National Debt inamchanganya President Ruto, sbb deni la Kenya lilipofikia ni 70% ya GDP ratio and IMF inasema ili kuwa salama, maximum ya National Debt to GDP ratio isizidi 55%..!! So, IMF and World Bank nadhani wameinyima mkopo Kenya, so kupata fedha za kuendesha Serikali na kulipa Deni la Taifa la Kenya ikawa hana option zaidi ya kuongeza kodi karibu kila kitu.. ikumbukwe ukizidisha kodi kuliko uhalisia biashara zinakufa pia, maana yake GDP inapungua, so ikiwa hata deni litabakia constant na GDP imeshuka, ratio inapanda zaidi, so suala la kodi ni issue ya kuangalia kwa macho ya ndani sana, la sivyo utaua uchumi, na Debt to GDP ratio inapanda, hukopesheki tena kwani uchumi haukuruhusu, kodi ni kuwa nayo makini kweli, ila ukikosea tena ukakusanya kodi kidogo sana, kuliko hali halisi, pato la Taifa linashuka, hutaweza kulipa madeni na mishahara na miradi ya maendeleo, so kodi sahihi inabidi ilipwe, yaani kodi sahihi ili uchumi ukue na kodi sahihi ilipwe kwa kila mfanya biashara na watumishi wa umma, kodi sahihi ni mandatory kulipa, Deni la Taifa ni issue serious sana hadi limefikia 70% of GPD ilishapita danger zone..!! Ndio napata ufahamu sasa kwanini Mh. Rais Ruto alienda US kwa Rais Biden, nadhani ilikuwa kupata msaada wa haraka sana kuinusuru budget ya Kenya, nadhani hakupata mkopo au msaada aliotegemea kwa haraka kwa budget inayofuata ya Kenya.

Tanzania tuko vizuri kwani National Debt to GDP ratio is 35% meaning bado tuko vizuri na kila mwezi wanalipa hapa Tz deni, ingawa tunakopa ila tunalipa kila mwezi na hiyo % kupanda ni kidogo kidogo kwani pamoja tunalipa, kipimo chetu cha National Debt to GDP kinapungua ikiwa uchumi wetu unakuwa, yaani GDP yetu ikikuwa pia ratio inapungua, yaani Uchumi unakuwa wa afya zaidi, tusisahau tulianzisha miradi mikubwa ya kimkakati kabisa, na miradi mikubwa ya msingi na maana sana kwa Taifa letu, mfano SGR ikiisha na JNHPP ishakamilika sehemu kubwa sana, mikopo mikubwa kwetu itakuwa hakuna tena, maana tusisahau hii miradi miwili inaongeza Deni la Taifa letu ila bado tuko salama kabisa kiuchumi, 35% ni salama kabisa na Uchumi unakuwa na deni letu Serikali ya Mama Samia, Rais wetu analipa, wote mashahidi, hivyo kikubwa ni kudhibiti rushwa kubwa yaani Grand Corruption na matumizi makubwa Serikalini mfano magari ya kifahari ya VX V8 hasa kwa viongozi kama Wakuu wa Mikoa au Makatibu wa Wizara au Naibu Waziri etc kwani tukidhibiti vyema matumizi yasiyo ya lazima, Tanzania tuko vizuri sana..!! Serikali inunue Land Cruiser Prado tu kwa viongozi wengine except Mh. Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake na Mungu mbariki Mama Samia Rais wetu…!!
 

Wala tusujisifu kuwa tupo vizuri. Ufahamu kuwa kwenye bajeti ya mwaka huu, karibia 40% ya bajeti itatumika kuhudumia madeni. Sasa fikiria hiyo 60% ndiyo iende kwenye miradi ya maendeleo na kwenye bajeti ya matumizi ya kawaida.

Kwa kuangalia uwiano wa bajeti kwa uwingi wa watu, bajeti yetu ni ndogo kuliko ya Kenya, kuliko ya Uganda, kuliko ya Rwanda. Halafu kwa ujinga tu, tunajisifu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…