Natoa maana ya Serikali ya Kigaidi, ili kila mwenye akili timamu na mwenye uwezo wa kutafakari, aone, Serikali ya Tz inapungukiwa na nini ili kupata sifa ya kuitwa "Serikali ya Kigaidi":
STATE TERRORISM:
State terrorism refers to violent acts, threats, or intimidation committed by a government or its agents against civilian populations. The primary objective is to instill fear, suppress domestic dissent, or exert political and social control.
MAANA YAKE KWA LUGHA YETU:
Ugaidi wa kidola humaanisha vitendo vya vurugu, vitisho, au vya ugandamizaji vinavyofanywa na Serikali au taasisi zake, dhidi ya raia, kwa lengo la kupandikiza woga, kugandamiza haki za watu ili Serikali iweze kudhibiti kila kitu bila ya kuhojiwa.
Je, Serikali ya Tanzania imepungukiwa na sifa gani ili kuwa Serikali ya kigaidi?
Tuangalie vitendo vya Serikali ya Tanzania:
1)VItendo vinavyolenga kupandikiza woga kwa raia:
Kuteka, kuwapoteza, kuwaua na kuwabambikia kesi za uhaini wote wanaowakosoa watawala au Serikali. Bila shaka lengo la vitendo hivi vya kishetani ni kuwatisha wananchi, na kuwafanya wawe waoga wa kuhoji chochote, wakitambua kuwa wakihoji, ama watatekwa, watapotezwa, kubambikiwa kesi zisizo na dhamana, au hata kuuawa. Tuna mifano mingi ya waliouawa, waliotekwa, waliopotezwa, na waliobambikiziwa kesi za ugaidi, wakati magaidi wakitamba kwa uhuru.
2) KUTENGENEZA HOFU ILI WASIOHIJIWE HATA WAKIFANYA UOVU:
Wote tulishuhudia kilichofanyika Oct 29. Ziliwekwa sheria na kanuni za kulinda wizi wa kura. Wananchi walipohoji na kutaka mabadiliko, waliambiwa hakuna cha nywinywi, uchaguzi utafanyika kwa kanuni hizo za kulinda uovu kwenye uchaguzi.
Wananchi walipoendelea kutoa maoni yao na kupinga sheria na kanuni hizo, Serikali iliongeza askari mabarabarani ili kutengeneza hofu kwa wananchi, wasiendelee kuhoji, na wevi wa uchaguzi wafanye chochote wanachokitaka bila ya kuhojiwa na yeyote.
Taasisi na Watu majasiri na wenye uzalendo wa hali ya juu, walipojaribu kuendelea kuhoji na kushauri, wote waliishia kwenye dhuluma za ajabu: TEC iliposhauri umuhimu wa majadiliano ya kujenga kabla ya uchaguzi, katibu wake mkuu Father Kitima, walimvamia na kutaka kumwua, Mungu akamlinda akanusurika. Gwajima alipopinga vitendo vya utekaji, Kanisa lake lilifungiwa, na yeye kuanza kuwindwa.
Tundu Lisu alipojaribu kufanya mikutano ya kuwaelimisha wananchi wasishiriki uchaguzi bandia, ambao kura zao hazina maana yoyote, alikamatwa na kubambikiwa kesi ya ugaidi. Vitendo hivi vyote vikilenga kujenga hofu kwa wananchi.
-Wananchi maana yake wajiulize, kama hawa wenye nafasi zinazoeleweka na wanaofahamika nchi nzima na kimataifa, wanatendewa hivi, mimi mwananchi wa Tandahimba, Namtumbo au Katoro nitafanywa nini!! Vijana walioamua kuvaa ujasiri na kufanya maandamano kuupinga uchaguzi bandia, waliuawa kama nzi.
Na hata wananchi ambao hawakuandamana, lakini walikuwa kwenye maeneo yaliyofikiwa kiurahisi na wauaji, waliuawa kama mende. Yote ikilenga kutengeneza hofu, na kupeleka ujumbe kwa raia kuwa wao wauaji wana uwezo wa kumwua yeyote, awe na hatia au asiwe na hatia, na hakuna wa kuwawajibisha.
Na hata hivi majuzi u/7, Watanzania wanaharakati wa haki za binadamu, walipowahamasisha watu waandamane kudai katiba mpya na kuachiwa huru watu waliobambikiwa kesi, na pia kupinga vitendo vya utekaji na kuwapoteza watu wanaohoji au kuikosoa Serikali, mara moja serikali ilikusanya mamia ya askari na kuwaweka maeneo mbalimbali, na kuwakamata baadhi ya wote walioonrkana kuunga mkono maandamano hayo kwa kauli tu; yote hiyo ikilenga kuwatisha wananchi (to terrorise people).
NB: in short, any institition, goverment or individual doing any act to terrorise people is a terrorist.
Tujiulize, serikali hii imepungukiwa na sifa gani, hata isiitwe Serikali ya Kigaidi?
Kama ni Serikali ya kigaidi, je ni lini tutaondokana na mifumo inayoruhusu taifa kuongozwa na serikali za kigaidi?
Tukumbume kuwa gaidi siku zote anatisha, na ndiyo lengo lake, uwezekano wa kutoka hapa tulipo, upoje? Au ndiyo tuseme tusendelea kuwa sisi na vizazi vyetu, tutaendelea kuishi kwenye laana hii ya uongozi wa kigaidi, maisha yetu yote kwa sababu walioshika mpini wameamua nchi iwe ni mfumo wa utawala wa kigaidi?
Yaani utawala ambao nyenzo yake kubwa ya kutawala siyo matakwa na maamuzi ya wananchi, uwezo wa watawala kudhulumu, kutisha na kutengeneza Taifa la wananchi wente hofu wakati wote.
Hii ni kinyume kabisa na ndoto ya Hayati Mwalimu Nyerere, ambaye alipoona mwelekeo wa nchi, alisema:
"Haikuwa dhamira yangu kutengeneza taifa la vijana waoga, vijana wenye hofu, vijana wasioweza kuhoji, vijana wa ndiyo mkuu, bali taifa lenye vijana jeuri, vijana wanaoweza kuhoji, kukosoa na hata kukataa, pale inapobidi".
Sasa tupo mbali kabisa na ndoto ya Muasisi wa Taifa letu, tumekuwa taifa la watu wanafiki, waongo, machawa wa kusifia kika jambo, mema na mabaya. Hatuna Bunge wala mahakama, kama mihimili inayojitegemea. Kila anayehoji, anayekosoa anaonekana ni adui, na wadhulumu haki huanza kumwinda ili wamwangamize.
Pamoja na jitihada zetu, tunaomba Mungu akaweke mkono wake wa ulinzi juu ya wote waliojitoa mhanga kulipeleka Taifa letu kwenye mifumo ya haki, itakayojenga umoja wa kweli, na amani halisia, siyo utulivu unaolindwa kwa mbinu za kigaidi.