The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Serikali ya Marekani imekifungia Chuo Kikuu cha Harvard kudahili wanafunzi wa kimataifa, na kuamuru wanafunzi wa kigeni waliopo wahamie vyuo vingine au wapoteze sifa ya kisheria ya kuishi nchini humo.
Uamuzi huo umetokana na chuo hicho kuchochea vurugu na chuki dhidi ya Wayahudi, na kushirikiana na Chama cha Kikomunisti cha China ndani ya chuo.
“Ni heshima, si haki, kwa vyuo vikuu kuandikisha wanafunzi wa kigeni na kunufaika na ada zao za juu ili kuongeza hazina zao za mabilioni ya dola,” alisema. “Harvard walipata nafasi nyingi za kufanya kilicho sahihi. Walikataa.”
Katika barua kwa uongozi wa chuo hicho, Noem alisema kuwa cheti cha Harvard cha Programu ya Wanafunzi wa Kubadilishana na Wageni (Student Exchange Visitor Program) kimefutwa. Programu hiyo inasimamiwa na kitengo cha Upelelezi wa Usalama wa Ndani cha Marekani, ambacho kiko chini ya wakala anayesimamiwa na Noem.
Hatua hiyo inamaanisha kwamba si tu kuwa Harvard haitaruhusiwa kupokea wanafunzi wa kimataifa katika kampasi yake, bali pia wanafunzi waliopo watalazimika “kuhamia chuo kingine ili kudumisha hadhi yao ya kutokua wahamiaji,” barua hiyo ilisema.
Katika taarifa, Harvard iliitaja hatua hiyo kuwa “haramu” na “kitendo cha kisasi”.
“Tumejidhatiti kikamilifu kulinda uwezo wa Harvard wa kuwakaribisha wanafunzi na wasomi wetu wa kimataifa, ambao wanatoka katika zaidi ya nchi 140 na wanaifanya chuo hiki – na taifa hili – kuwa na thamani isiyo na kipimo,” chuo hicho kilisema.
Hatua hiyo inaashiria kuongezeka kwa mvutano kati ya chuo kikuu hicho – ambacho kimekataa kukubaliana na orodha ya madai yanayohusiana na programu zake za utofauti na jinsi kilivyoshughulikia maandamano ya kuunga mkono Palestina – na utawala wa Trump.
Utawala huo umejibu kwa kupunguza ufadhili na ruzuku ya serikali kwa raundi tatu, jumla yake ikifikia zaidi ya dola bilioni 2.6. Ya hivi karibuni ilikuwa siku ya Jumatatu. Kwa sasa, Harvard imefungua kesi ikidai kuwa utawala huo unakiuka Katiba ya Marekani kwa hatua zake.
Mapema wiki hii, Rais wa Harvard, Alan Garber, aliwahimiza wahitimu wa chuo hicho kuonyesha msaada wao – na michango yao – kwa chuo kikuu.
“Taasis hii tuliyoaminiwa kuiongoza sasa inakabiliwa na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa katika historia yetu ndefu,” aliandika Garber katika barua pepe, ambamo alizindua Mfuko wa Vipaumbele vya Urais na Mfuko wa Utafiti wa Urais. Mifuko hiyo miwili inalenga kushughulikia mapungufu yaliyosababishwa na upunguzaji wa ufadhili.
Kwa mujibu wa wakili wa masuala ya uhamiaji Leon Fresco, hatua ya utawala wa Trump itakuwa pigo la kifedha kwa chuo hicho na “tatizo kubwa” kwa wanafunzi.
“Ikiwa wanafunzi wa kimataifa hawataweza kuhudhuria chuo kikuu, watalipwa tena ada walizolipa kwa ajili ya muhula ujao,” aliambia Al Jazeera, na kuongeza kuwa Harvard ilitegemea fedha hizo kwa mwaka ujao.
Fresco alieleza kuwa kuna njia halali za kupinga kufutwa kwa programu ya kubadilishana wanafunzi wa kimataifa.
“Kanuni za kufuta cheti hicho ni maalum sana – lazima kuwepo na taarifa ya nia ya kufuta inayotolewa. Lazima kuwepo na sababu zinazohusiana na kutotii masharti ya programu ya wanafunzi wa kubadilishana,” alisema. “Haiwezi kuwa kufutwa kwa msingi wa kisiasa au kiitikadi, hilo halipo kwenye kanuni.”