Serikali ya Rais Samia Haitasahaulika Wala Kufutika Katika Mioyo ya Watanzania

Ndugu zangu Watanzania,

Serikali ya Rais Samia itakumbukwa kwa miaka mingi sana, itaishi katika mioyo ya Watanzania na kusimuliwa vizazi na vizazi. Haiji kupotea wala kufutika katika mioyo ya Watanzania, itaendelea kudumu na kutawala fikira za Watanzania. Itaendelea kuongoza katika mioyo ya Watanzania kutokana na alama za kudumu zilizoandikwa kwa wino wa upendo katika vifua vya Watanzania. Kila wakati itasimuliwa kwa mema mengi iliyoyafanya na kukumbukwa kwa miaka mingi sana ijayo kama tunavyoendelea kuishi na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika mioyo yetu bila kujali itikadi zetu za kisiasa au dini zetu.

Ni serikali hii ya Rais Samia kwa miaka mingi ijayo ambapo kila kijana atasimulia kuwa ni wakati wa Rais Samia ambapo ajira zilianza kutolewa maelfu kwa maelfu, mikopo vyuoni ilianza kumwagwa na kutolewa kwa wote wenye sifa bila ubaguzi. Ni wakati wa Samia ambapo fedha ya kujikimu ilipanda mpaka kufikia elfu kumi kwa siku na kupelekea wanafunzi kusoma kwa utulivu na kuzingatia vyema masomo. Ni serikali hii itakumbukwa na mamilioni ya vijana kuwa ni wakati wake aliwapa vijana tabasamu, furaha, na matumaini ya kupata ajira na kujiajiri kwa wepesi kutokana na mazingira mazuri ya kibiashara, hasa baada ya kuweka utaratibu wa kutokulipa mapato katika mwaka wa kwanza wa biashara ili kutoa nafasi ya kukua kimtaji.

Ni serikali hii itakayosimuliwa na wakulima kuwa ni wakati wa Rais Samia walipofutwa machozi, walipopewa heshima wao na sekta ya kilimo. Ni wakati wa Rais Samia ambapo kilimo kilianza kuwa kimbilio la watu wote wakiwepo wasomi. Itasimuliwa na wakulima kuwa ni wakati na utawala wa Rais Samia ulipokigeukia kilimo na kuweka mikono yake kwa kuwekeza mabilioni ya pesa ili kuwainua migongo yao wakulima iliyokuwa imeinama na kupinda kutokana na dhoruba za jembe pasipo kupata wala kufaidika na jasho lao, mpaka Mama Samia alipokuja kama mkombozi wao na kutoa nuru katikati ya giza totoro katika kilimo.

Itasimuliwa kwa vizazi vijavyo na wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo kuwa ni wakati wa Rais Samia ambapo biashara nyingi zilifunguliwa, wafanyabiashara wakifanya biashara kwa amani na utulivu, maafisa wa TRA walikuwa marafiki zao na watu wa kutoa ushauri wa kitalaam hususani unaogusa masuala ya kikodi. Itasimuliwa ni wakati huu ambapo wafanyabiashara walianza kutunza pesa zao benki badala ya kwenda kufungia majumbani mwao au chini ya magodoro kwa hofu, kwa kuwa ni wakati huu walikuwa na imani na Rais Samia na serikali yake na hawakuwa na wasiwasi wa kuchotewa pesa na mtu yeyote pasipo utaratibu wa kisheria na kibenki.

Wazazi watasimulia kwa watoto na wajukuu zao kuwa ni wakati wa serikali ya Rais Samia ambapo elimu ikawa bure hadi kidato cha sita na kuwafanya watoto wao kusoma hadi vyuo vikuu bila kujali hali zao za kiuchumi kuwa duni, kwa kuwa mzigo wa ada ulikuwa umebwagwa na serikali ya Rais Samia. Itasimuliwa na wazazi kuwa ni wakati wa Rais Samia watoto na vijana wengi walisoma kwa bidii kutokana na kuwa na mazingira mazuri ya kusomea na kujifunzia pamoja na soko la ajira kuwa lenye kuleta matumaini kwa vijana wao.

Ni serikali hii ya Rais Samia itakumbukwa na kusimuliwa na watumishi wa umma kwote nchini kuwa ni wakati huu ambapo walianza kupata morali ya kazi na kujituma kazini. Ni wakati huu ambapo walianza kujiona kuthaminiwa mchango wao katika maendeleo na ukuaji wa uchumi. Ni wakati huu ambapo ajira serikalini ilikuwa ni kazi ya heshima katika kulitumikia taifa badala ya kuonekana kama utumwa na gereza, kwani ni wakati huu ambapo viongozi waliwaheshimu na kuwatia moyo katika utendaji kazi wao. Ni wakati huu ambapo walianza kupandishwa madaraja, nyongeza ya mishahara, kupewa posho ya kazi kulingana na majukumu ya mhusika, n.k.

Serikali ya Rais Samia itasimuliwa na Watanzania kuwa ni wakati wa Rais Samia ambapo kwa mara ya kwanza rais wa nchi, Mwenyekiti wa Chama Tawala katika historia ya taifa letu, alihudhuria siku ya Wanawake Duniani kwa kujumuika na akina mama kutoka chama kikuu cha upinzani CHADEMA. Itasimuliwa ni wakati huu ambapo hakukuwa na uhasama wa kisiasa, Watanzania kuishi kwa upendo, mshikamano na umoja wa hali ya juu sana kwa kushirikiana katika shughuli zote za kijamii.

Serikali hii ya Rais Samia itasimuliwa kuwa ilisimama imara katika kipindi ambacho majirani zetu walifikia hatua ya kushindwa kulipa mishahara watumishi wake wa umma. Ilihali hapa nchini, serikali yetu ilikuwa inaendelea kuwahisha zaidi mishahara kwa watumishi wa umma pamoja na kutoa maelfu ya ajira kwa vijana.

Serikali ya Rais Samia itakumbukwa na mamilioni ya Watanzania kwa kutuusha kipindi kigumu cha ugonjwa hatari wa COVID-19 pamoja na vita ya Ukraine, uliyopelekea mfumuko wa bei duniani kote, hasa kwa bidhaa muhimu na kupelekea mdororo wa uchumi. Lakini ni kwa ushupavu wa Rais Samia na serikali yake, alisimama imara na kuchukua hatua za makusudi kwa kutoa mabilioni ya ruzuku katika mbolea kiasi cha bilioni mia moja hamsini, pamoja na kutoa ruzuku ya bilioni mia moja kila mwezi katika nishati ya mafuta. Jambo ambalo nchi jirani zilishindwa kufanya hivyo na kupelekea kulia na kuteseka kwa wananchi wao. Huku Tanzania tukiwa tumeisaidiwa na serikali yetu kupunguza makali ya mfumuko wa bei.

Ni serikali hii ya Rais Samia itakumbukwa kwa kutoa uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na uhuru wa mahakamani. Ni wakati huu itakumbukwa na Watanzania kuwa kila mmoja alijiona fahari kuzaliwa Tanzania na kila mmoja alijiona anayo nafasi ya kutimiza ndoto zake, lakini pia kila mmoja alijivunia mafanikio yaliyopatikana na kujiona ni sehemu ya mafanikio hayo.

Kila mmoja atasimulia kuwa ni wakati wa serikali ya Rais Samia ambapo ilikuwa mali ya Watanzania, serikali ikawa kwa ajili ya kuwatumikia watu, kuwasikiliza watu, kufanya maamuzi yenye maslahi kwa wengi, kupitisha sheria zenye afya kwa watu na tija kwa taifa letu. Ni wakati ambapo Watanzania walipewa nafasi ya kusikika sauti zao na kupewa majibu ya kina.

Kwa hakika, serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia haiji kufutika wala kusahaulika katika mioyo ya Watanzania kwa miaka mingi sana ijayo. Itaendelea kusimama kama rejea nzuri na kwa mambo yote mema katika taifa letu. Majina ya viongozi wake yataandikwa katika kuta za mioyo ya Watanzania kwa wino wa dhahabu.

Kazi iendeleee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Acha kujipendekeza... Wafundishe wanao kwamba,, mseleleko mixer kitonga huwa siku zote vinatokeaga puani....
 
CCM ni Chama cha wezi tokea lini mwizi akamfikisha mahakamani mwizi mwenzake?
CCM Ni sauti ya watanzania Ndio maana inaungwa mkono na mamillion ya watanzania,kila mmoja anatambua kuwa CCM haina Subira kwa wote wenye Kuchezea pesa za umma
 
Aliye haribu ni yule shetani ambae alidhani hatakufa.

Manina kafa nchi imetuliaaaa
 
Kulikoni Tena mnakataana hadharani?
Hamuwezi kufanani mitizamo wakati wote, kutofautiana kimtizamo ni Jambo la kawaida na ndio maendeleo ya kifikira hupatikana kupitia kutofautiana ,maana mwisho wa siku lazima mfike muafaka kwa kuchanganua hoja ya kila mmoja ili kuangalia Ni Nani yupo sahihi Ni kwa vigezo vipi
 
Kijana ninataka uandike makala ya kunisifia, taja kiasi gani nkutumie kwenye namba yako hiyo mana si kwa njaa uliyonayo.

KATIKA MARAISI WALIOPOTEZA MVUTO TANGU ENZI ZA NCHII HII NI HUYO UNAYEMSIFIAA,HISTORIA YAKE ITAFUTIKA HARAKA SANA NA HAKUNA ATAKAYEMKUMBUKA HATA MMOJA KWA JINSI ANAVYOTESA WATANZANIA
 
Rais Samia Ndio kiongozi ambaye hakauki katika midomo na vinywa vya watanzania kwa Sasa,Ni kiongozi mwenye ushawishi katika kila kundi na kwa Rika zote,ukienda kwa akina mama, vijana,wazee,Wana michezo ,wakulima n.k unakuta kwote huko anakubalika kwa Kiwango kikubwa Sana ,unakuta anaungwa mkono na mamillion ya watanzania,unakuta anazungumzwa kwa mema na mazuri Aliyolitendea Taifa letu,unakuta anapewa pongezi na sifa kwa ushupavu na umadhubuti wake kiuongozi,unakuta kila mtu anatamani na kumfuatilia Sana mh Rais ahutubiapo mahali popote pale .
 
Back
Top Bottom