Serikali ya Rais Samia Haitasahaulika Wala Kufutika Katika Mioyo ya Watanzania

Well said.
 
Wee peleka uchawa wako huko. Atakumbukwa kwa nini? Kwa kuwarudisha uongozini waliyokua wametumbuliwa na magufuli au kuwarudisha cheti feki kazini?. Kuwaamini wale waliyomkejeri na kumsengenya magufuli kumuita mshamba? Atakumbukwa kwa kukopa sana na kujaribu kuondoa dhana kwa watanzania kwamba nchi yao ni tajiri? Atakumbukwa kwa kujaribu kufuta kujitegemea watanzania badala yake wawe ombaomba?
Usilete utani wa maudhi kwa uchawa wako ndugu.
 
Naona umeandika ngonjera za uongo mtupu, Nani kakwambia Tanzania Ni omba omba,Tanzania inajitegemea ndio maana inao uwezo wa kugharamia Mambo yake mbalimbali ikiwepo miradi pamoja na kulipa mishahara watumishi wake wa umma,wakati majirani zetu wanashindwa hata kulipa mishahara watumishi wake wa umma.

Kila kiongozi hufanya kazi na kumteua mtu anayeona atafaa katika nafasi fulani kulingana na matarajio yake pamoja na uwezo wa mtu husika,usimpangie mh Rais wetu juu ya Nani na Nani afanye Naye kazi katika serikali Yake, ndio maana tunasema kila Zama na kitabu chake, Tanzania Ina watu zaidi ya million 61 hivyo Rais anao uwanja Mpana wa kuchagua na kuteua wabkifabya Naye kazi na siyo kusema afanye na kumteua huyu na huyu kosa tu alikuwepo awamu fulani,maana hii nchi Hakuna mwenye hati miliki ya uongozi katika Wizara fulani au secta fulani.

Unaposema fulani na fulani Ni wezi bila kuweka ushahidi huo Ni uhayawani tu maana umeandika kwa chuki binafsi tu na mihemko tu pasipo kuwa na ushahidi wa Aina yoyote Ile.

Habari za kukopa ningependaa kukujibu kuwa kukopa siyo dhambi na ndio maana kila awamu ilikopa Sana katika kuwekeza kwenye miradi yetu, kinachoangaliwa bni unakopa kwa ajili ya Nini,Aina ya mkopo,masharti ya mkopo,riba ya mkopo,muda wa kuanza kufanya marejesho,mahali unapokwenda kuweka au kuwekeza pesa za mkopo na faida ya mradi unaotokana na mkopo na uwezo wa kulipa mkopo kwa wakati,serikali yetu chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais wetu mama Samia imekuwa ikichukua mikopo ya masharti nafuu na inayoanza kulipwa baada ya muda mrefu,lakini pia Tanzania bado tunao uwezo wa kulipa madeni yetu na pia Deni letu bado Ni himilivu na ndio maana tunakopesheka na tunaaminika ni secta za kifedha za kimataifa na tunapongezwa kufanya vyema katika uchumi wetu.

Ukusanyajo wetu wa mapaato ya ndani Ni mzuri Sana,ndio maana mapato yetu yamepaa na kufikia Trioni mbili kwa Mwezi pasipo kukimbizana Wala kufungiana biashara mitaani na wafanyabiashara,hii Ni kutokana na kuboresha mazingira ya kiuwekezaji na kibiashara na kujenga Imani kwa wawekezaji na wafanyabiashara katika kuwekeza nchini.
 
Hayo mashairi kampelekee huyo rais wako. Hujui usemalo. Bado ni mapema kufanya assessment mwanangu vinginevyo una lako
 
Ukiwa kiongozi ukamkuta chawa ana kusifia hivi saa nyingine unatakiwa umlabue kofi maana anakupa sifa zingine za uwongo ili kufanikisha maslahi yake watu kama hawa wanachangia kulirudisha nyuma taifa letu
 
Ukiwa kiongozi ukamkuta chawa ana kusifia hivi saa nyingine unatakiwa umlabue kofi maana anakupa sifa zingine za uwongo ili kufanikisha maslahi yake watu kama hawa wanachangia kulirudisha nyuma taifa letu
Ilitakiwa uonyeshe Ni wapi nilipoweka maneno ya uongo kuliko kuongea kijumla jumla tu
 
Wewe utakuwa vyeti feki uliyetumbuliwa naona inatafuta huruma ya Mama Samia kwa kumsifia sifia
Mimi naandika ukweli juu ya Mambo makubwa aliyoyafanya ndani ya muda mfupi wa uongozi wake yaliyoleta Tabasamu, furaha na matumaini katika mioyo na maisha ya watanzania
 
Hayo mashairi kampelekee huyo rais wako. Hujui usemalo. Bado ni mapema kufanya assessment mwanangu vinginevyo una lako
Huwezi ukasema Ni mapema wakati unaona umapema huo umeleta mapinduzi makubwa Sana katika kila secta na kuleta nuru kila mahali palipokuwa na Giza ,kwa Sasa Ni matumaini kila mahali na kila mtu Anayo matumaini ya kutimiza Ndoto zake
 
Maneno mengiiiiii sisomi ila kiukweli huna akili wewe
 

Mzee usilazimishe kukaza fuvu.Kati ya viongozi ambao hawafuatiliwi ni huyo mama yako.

Wewe ni mjinga sana na wewe, pia wewe ni kielelezo kuwa kuna watanzania wengi wajinga ambao wanaficha njaa ya matumbo yao kwenye mgongo wa uzalendo.


Watu kama wewe walikuwepo kuanzia enzi za JK na wewe utapita tu kama upepo
 
KAMA KUSOMA KWA MACHO HUWEZI BASI TUMIA HAYO MATTER CALL.

HIVI HUONI TU HAPA JUKWAANI KUWA KATIKA KOMENTI 5 BASI 4 ZINAKUPINGA



MJINGA WEWE
 
Huyu mama siku anamaliza muda wake itakuwa siku ya wazalendo kupata uhuru.

Tutasheherekea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…