Serikali ya Rais Samia Haitasahaulika Wala Kufutika Katika Mioyo ya Watanzania

Uwe unajibu kwa ufupi utamaliza wino kwenye simu.
 
Huwezi ukasema Ni mapema wakati unaona umapema huo umeleta mapinduzi makubwa Sana katika kila secta na kuleta nuru kila mahali palipokuwa na Giza ,kwa Sasa Ni matumaini kila mahali na kila mtu Anayo matumaini ya kutimiza Ndoto zake
Una sifa ya kujipendekeza na kukurupuka. Kama unataka kumridhisha rais akutupie morsel sie uende CCM Lumumba wakukague na kuona kama unafaa kuwa cheerleader wao. Ni mapema hasa ikizingatiwa kuwa kuna uchaguzi ujao na urais wa Samia ni wa accident. Tanzania bado ina matatizo mengi ambayo ni vipofu tu hawawezi kuona. Ufisadi ukoje sasa ambapo taarifa ya CAG imeanika kila kitu bila kuchukuliwa hatua? Wewe kubali una lako. Tafuta namna ya kujiongeza na siyo kujikomba komba kwa kusifia hata visivyosifika.
 
Tanzania chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia inafanya vizuri Sana katika kila secta, mfano katika suala la uchumi inaendelea kuwa mstari wa mbele katika kufanya vizuri mpaka kupongezwa na shirika la Fedha la kimataifa ,pamoja na Taasisi mbalimbali za kifedha,

Ukija katika suala la uboreshaji wa huduma za kijamii nako pia Tanzania ya Rais Samia imefanya vyema Sana kwa kusogeza huduma karibu ya mwananchi na hivyo kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma.
 
Huyu mama siku anamaliza muda wake itakuwa siku ya wazalendo kupata uhuru.

Tutasheherekea.
Labda wewe,lakini mamilioni ya watanzania wanatamani Rais Samia aendelee kutuongoza mpaka achoke mwenyewe
 
KAMA KUSOMA KWA MACHO HUWEZI BASI TUMIA HAYO MATTER CALL.

HIVI HUONI TU HAPA JUKWAANI KUWA KATIKA KOMENTI 5 BASI 4 ZINAKUPINGA



MJINGA WEWE
Kasome historia ya Galileo ndio utaelewa na kupanuka akili yako.Ukweli Ni ukweli tu hata upingwe na watu wangapi utabakia kuwa ukweli tu
 
Mimi sijipendekezi lakini pia siandiki hapa kwa ajili ya kutarajia malipo Kama unavyowaza wewe
Haipo hiyo kitu..... KWa hali hii mchele super mzuri kilo 3500 kweli? Tena Hapo KWa wakulima huko ambako hawalimi je? Afu unasifia eti... Hivi mtu anakuwasha kofi afu unamchekea huku unamsifia.... KWa akili ya kawaida watasema wewe chawa... Kukenue meno kwako hovyo hata kama umechezea makofi.. ni njia ya kujipatia kipato....
 
Kilimo Ni Biashara acha wakulima nao wafaidike na jasho lao ,lakini pia msimu wa mavuno umewadia kwa mazao mbalimbali ya chakula huku nyanda za juu kusini ambako ndiko chakula kingi hutokea,hivyo Bei itapungua kiasi lakini ambacho hakimpi hasara mkulima kulingana na gharama za uzalishaji.
 
Huwa sisome threads zako
Unaboa sana.
Natamani km nikuhamishie upande wa watetea legacy ya Chato.
 
Hebu tumia akili japo kidogo.
Yaani comments zote hakuna ht anayekuunga mkono. Hebu jishtukie kidogo km kweli wewe ni timamu
Ukweli huwa haujalishi Ni wangapi wanaopinga , ukweli unabaki kuwa ukweli hata Kama itachukua muda kueleweka kwa wenye kuona karibu.
 
Kwa kweli kuna watu wanajua kusifia! Ila wewe wewe mwenzetu umezidi.

Maana hata mhusika akisoma hii habari yako, atagundua mapema sana ya kuwa wewe ni zaidi ya chawa.
Ndiyo maana anarukwa kwenye mikeka ya teuzi,hata huyo msifiwa mwenyewe amekinai hizo sifa.
 
Ndiyo maana anarukwa kwenye mikeka ya teuzi,hata huyo msifiwa mwenyewe amekinai hizo sifa.
Mimi naongea ukweli juu ya kazi njema na ya kupigiwa mfano iliyofanywa na serikali ya Rais Samia katika kugusa maisha ya watanzania,Sitafuti uteuzi Bali naandika kile kinachoonekana kuwa matunda ya juhudi na uchapa kazi wa mh Rais wetu
 
Upinde unakunyemelea kwa mdemko huu wa kutukuza mtu mwenye mji wake .ama njaa bro
 
Duuh! BASI Sawa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…