Serikali ya Rais Samia ije na mpango wa kunusuru wasio na kazi

Serikali ya Rais Samia ije na mpango wa kunusuru wasio na kazi

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2013
Posts
749
Reaction score
875
Kimekuwa ni kilio cha muda mrefu sana kuhusu ukosefu wa ajira hapa nchini kwa makundi yote yaaani wenye elimu za juu, kati na hata chini ,lakini serikali za awamu zote zijaona kama zimekuja na mpango mkakati juu ya ili kundi ili kulinusuru maana hatua ya sasa hali imekuwa ni mbaya kuliko inavyodhaniwa na wanasiasa.

Napenda kuishauri serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh: Samia Suluhu Hassan kuja na mpango kabambe wa kunusuru kundi lisilo kuwa na ajira uwe unafanana na TASAF ila uwe unalenga watu wasio na ajira , uwe kama ule wa nchini Wingireza wa Unemployment Benifit.Mpango huu uwe unatoa ruzuku kila baada ya muda fulani kwa walengwa wa ili kundi.

Najua ili kundi lina mchango mkubwa sana katika taifa maana ndio vijana wanaotumika katika chaguzi mbali mbali na kurubuniwa watatatuliwa shida zao lakini huwa ni tofauti baada viongozi hao kushika madaraka.

Najua wazi kama taifa tukiandika wazo na kuwapelekea nchi waisani daima hawawezi kulikataa.Kutoa ajira sio suluisho maana serikali kamwe haiwezi kuajiri watu wote.
 
Back
Top Bottom