Serikali ya Rais Samia ilivyoirejesha Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya (EIB) nchini

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya (EIB) imeeleza sababu za kurejea Tanzania na kufanya uwekezaji mkubwa wenye thamani ya Euro milioni 540 baada ya kutokuwapo kwa miaka saba nchini.

Moja ya sababu hizo ni maboresho makubwa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoiongoza, ikiwamo kuhakikisha mazingira mazuri ya biashara kwa wawekezaji.

Makamu wa Rais wa EIB, Thomas Ostros aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa Kongamano la Biashara Kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) lililofunguliwa na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango kwa niaba ya Rais Samia Suluhu.

Ostros alisema maboresho na mazingira mazuri ya biashara ndiyo yaliyowafanya kurejea Tanzania na leo wanatarajia kutia saini hati ya makubaliano ya fedha hizo.

 
Kwamba walikua wanaitwa mabeberu ndo hawa 🤔🤔
 
Aliyepita ameshapita, tugange yajayo
Walioumia Kwa ukatili wake hawezi kukubaliana na kauli yako. Lazima wamseme mpaka maisha yao yote. Mke , watotona wazazi wa wa Ben watakuelewa kweli?
 
Safi sana haya ndio maendeleo tunataka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…