Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Pamoja na mapungufu ya hayati John Magufuli lakini hakupepesa macho wala kumung'unya maneno pale penye ukweli.
Bado Serikali yahangaika kujimwambafwai lakini ukweli wa matatizo yoote yaliyopo nchini kwa sasa uliwekwa wazi na Hayati Magufuli.
Alieleza matatizo ya baadhi ya wahujumu uchumi wa nchi na maisha ya watanzania juu ya upunguzaji maji wa bwawa la Mtera ili maji yauzwe, video zipo na watanzania wamezihifadhi.
Tatizo la umeme pia aliliezea kuhusu ufisadi na biashara ya majenereta ambayo kimazingira si mazuri na pia kwa afya ya binadamu kutokana na moshi, video zake zipo na wananchi wamezihifadhi,.
Uzuri wa watanzania wengi wa sasa ni kwamba wanauwezo wa kununua vifaa vya kidijitali na asilimia kubwa wanatumia mitandao ya kijamii hivyo wana access ya kila alichokisema hayati Magufuli.
Hayati Magufuli alikuwa akizunguka nchi nzima kuwafahamisha watanzania juu ya kujiletea maendeleo na namna jinsi nchi hii ilivyobarikiwa kila kitu na tatizo na namna ya kutumia vyanzo vya maji, ardhi safi ilijaa rutuba na akawa akisisitiza kulima na kuhifadhi chakula.
Sasa, serikali imekwishaharibu kila eneo ambalo angalu lilikuwa limeleta unafuu na kwa miaka mitano hakukuwa na tatizo la umeme wala maji.
Hivyo Serikali hiihii ingetumia mbinu zilezile alozitumia hayati Magufuli kuhakikisha umeme wa uhakika unakuwepo na kila mwananchi anapata maji safi na salama.
Nasema hivyo kwa kuwa wizara ya nishaji ilikuwa ikiongozwa na mtaalam wa sekta ya nishati na pia baadhi ya mawaziri walokuwapo na ambao wapo wengi waliona uendeshaji wa serikali ya awamu ya tano.
CCM itambue kuwa serikali yake inayumba kutokana na kuamua kurudi tulikotoka, hivyo ni kheri ifanye maamuzi magumu ya kuukubali ukweli kuwa imeshindwa kutekeleza kwa makini Ilani yake ya uchuguzi ya mwaka 2015 na pia imeweka rasmi kabatini Dira yake ya maendeleo ya Taifa ya 2025 au imeipoteza.
Kuna tetesi kuwa waziri wa madini huenda nae akaondolewa kwa shinikizo la kwamba ni "hardliner" na alikuwa "inner circle" ya hayati hivyo hawa hardliners ni lazima waondolewe.
Wale welevu wote wapo na waangalia na kuku bado watengeneza uzuri mikakati ya kufanya dua kubwa la kumdondosha mwewe.