Serikali ya Rais Samia kukusanya TZS 1.6BL ili kuchagiza Stars ifuzu kombe la dunia 2022 Qatar,

asante sana Rais Samia
 
Nadhani hizo fedha zingetengwa ili kusuka Kikosi kipya na imara kwa ajili ya mashindano mengine ya baadaye kama AFCON,CECAFA,nk ikiwa ni pamoja na kuajiri Makocha wazuri zaidi.
Kuliko kuzitupa kwa kikosi hiki ambacho hakitafika ko kote kwenye mashindano hayo!
 
Kwanini usishauri zitafutwe zingine kwaajili hiyo?
 
😳😳
 
Kwa haki kabisa natamani tuishie hapa. Tukienda huko qatar tutaenda kupata aibu kama ile waliyopata Zaire ya Mobutu Seseseko.
Imagine tupangwe na timu kama ureno na Cr7 anataka kuwa mfungaji bora wa mashindano! Nadhano wote mnajua nini kitafuata hapo.

Afu game inayofuata tunapangiwa brazil. Uuuuuwiiiii neymar na bobby Firmino watatufanyaje unajua? Siwaambii.
Game ya mwisho tuna kutana na Kora ya kusini. Dangerous korean kim son. Kwa speede zake huyu mwamyeto atamfanyaje sasa. Naogopa sana.

Tuishie hapahapa inatosha.
 
😍
 
Ili baadaye wajisifu na misifa ya mama wa awamu ya siku ya kuumbwa binadamu, kwamba kaipaisha stars?
 
Hizi pesa zinazochangwa zitatumikaje? Sio kichaka cha kutakatisha fedha kweli? Kwa maoni yangu taifa stars,inachoitaji ni mbinu bora za kumsoma mpinzani na wachezaji kujituma na kufata maelekezo ya mwalimu, ambayo ni kazi ya mwalimu wao! hadi hapo sioni hizo pesa zitatumika wapi?

Nchi hii imejaa matapeli na wajanja janja watupu,tff kila mwaka inapokea fungu kubwa kutoka FIFA kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu ikiwemo na kuhudumia timu ya taifa,je fedha hizo hazitoshi? Hatuoni kuwaongezea pesa nyingine nje ya bajeti yao ni kuwakaribisha mchwa waje watafune hizo fedha?

Nani anasimamia matumizi ya hizo pesa?! Je kampeini yao ya kombe la dunia ikiisha tukiwa hatujafuzu au tumefuzu,watarudi kutupa mrejesho hizo fedha zimetumika vipi?! Maswali ni mengi ila uhalisia nchi hii ina matatizo mengi ila viongozi hawana muda wa kuyatatua zaidi ya kutafuta mbinu ya kutafuna pesa kwa utelezi tu bila kutumia nguvu.
 
Ikipita hatua hii, hatua ya play off haitachomoka.

Hiki ni kichwa cha mwendawazimu.

Naungana na mdau anayeshauri hela zitumike kuboresha viwanja vinavyomilikiwa na CCM ili mechi za ligi ziende vizuri

Huu ndio Ukweli...
Watu hawapendi kuusikia....
Afuzu jwa kiwango kipi?
Ndio Maana Nawaamini sana Wana Riadha,
Kina Alphonce Simbu aliekuwa wa 7 Olympic ya Dunia mwezi Uliopita Akijifua unajua kabisa akuwa Mshindi Hakudanganyi...Njoo kwenye Mpira sasa [emoji3516][emoji41][emoji851][emoji2][emoji2]Watanzania wanapenda sana sana Soka na Mafanikio ya Chaaap!
Akioangwa play off akakutana na Nchi ya Afrika kaskani na Magharibi kina nigeria Mali,Burkinafaso,Cameroon,Ghana,Nk chaliii[emoji3516][emoji2957]
 
Hii project imeshachelewa. Toka 2018 tulipaswa kufanya maandaliz.

Hizi presha zingeanza pale kuanzia mechi ya kwanza makundi huku tukiwa na kikosi chenye maandalizi mazuri.

Tusije kwenda tukawa kama Haiti.
 
Safi Sana hii
 
Majaliwa naye msanii tu, utakuta huyo rais wala hana habari na hiyo timu ya taifa wala hata labda hajui kwamba ina mechi na Congo DR.

Kwa nini serikali isitoe pesa ihudumie timu ya taifa na ilhali wanakusanya kodi kila siku? Bado wanarudi tena kuwakamua wafanya biashara walioelemewa na mzigo wa kodi.
This is very unfair and unacceptable.
 
Waziri mkuu tangu lini kawa msanii
 
Hongera Majaliwa
 
Khaaa
 
Kwahiyo zimechagiza au zimechagizwa hizo pesa, wafanye uwekezaji kwenye soka la vijana wajenge academy za serikali wazihidumie vizuri ndio uwekezaji wao wanawekeza kwenye hamasa ya mechi viongozi wetu wana vituko
 
Nashukuru sana Mungu mimi kama mfanyabiashara na muwekezaji sikuchangia katika kupata aibu hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…