Serikali ya Rais Samia kukusanya TZS 1.6BL ili kuchagiza Stars ifuzu kombe la dunia 2022 Qatar,

Naomba tu hizo bil 1.6 wazipeleke pale TBL au SBL wananchi tukabebe makreti tujipooze na hiki kitu kizito kilichotupiga
 
Walivyokaa utafkiri wanajadili kitu Cha maana
 
Bado kumbukumbu za Stars ilvyoendaga west Africa 'tukiwa na uhakika' wa 95% na timu ilivyorejea wakati huo PM aikiwa EL ikapelekwa moja kwa moja Dodoma lakini hatukujifunza.
Binafsi nilijihisi kusikitika na kwa vyoyote vile dunia ya wapenda michezo inatuamgalia na kutucheka, pale timu ya Biashara United iliyokuwa ikihitaji nauli tu ikiwa na magoli mawili mkononi ikakosa na upande wa pili eti zimechangwa billion kadhaa kwa ajili ya kuhamasisha timu ambayo inajisimamia.
Tatizo zikishaingia siasa katika michezo maana yake ni 'viongozi' ambao wengi ni ccm na hawa wana ushawishi wa moja kwa moja kwa kundi la wanachama wao wasiofikia hata million 5 dunia nzima wakati Tanzania ina watu karibia million 65 na kati yao zaidi ya 75% wanapenda michezo.
....ndio nikamsikia sijui nahodha jana akituahidi ushindi eti kwa sababu ,VIONGOZI WA SERIKALI' (na sio Watanzania wote) wako nyuma yao.

Mwenye hiyo clip ya Boko atusaidie ili tujifunze maana maisha yanaendelea. Katika uchambuzi wa hii mechi niliousikia leo asubuhi EFM alikuwa ni Meck Maxime, bahati nzuri sana yeye alikuwa miongoni mwa wachezaji wa hiyo timu iliyoendaga West Africa na baadae ikaja kutibuliwa na hizi siasa uchwala zetu. Katoa utabiri wa kitaalamu kabisa na kuahidi kuwa uchambuzi mzuri ni baada ya mchezo na sio hizi kelele za kishabiki
 
Safi sana hii, Tanzania nakupenda sana,

Hakuna Kama Rais Samia😍😍
 
Wacha weeeeee !! Mama anaupiga mwingi sana !

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
 
Ngoja tuone kama ni kweli au uongo,
 
Natangaza rasmi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…