Serikali ya Rais Samia Yarejesha rasmi mikopo ya asilimia 10 baada ya Vigezo kuboreshwa.Mtu Binafsi wa Hadi Miaka 30 Atapewa Mkopo

Serikali ya Rais Samia Yarejesha rasmi mikopo ya asilimia 10 baada ya Vigezo kuboreshwa.Mtu Binafsi wa Hadi Miaka 30 Atapewa Mkopo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Serikali imerejesha rasmi utaratibu wa Mikopo isiyo na riba ambayo ilikuwa inatolewa Kwa makundi maalumu kwa lengo la kuwainua Kiuchumi.

Awali mikopo ilisitishwa baada ya maafisa wa Serikali kutumia mwaya huo kukopesha Vikundi hewa na kisha kukwapua pesa za Umma hukunwalengwa wakishindwa kufikiwa.

Kwa Sasa vigezo vimeboreshwa na kuwa na mfumo rasmi wa utambuzi na ufuatiliaji Ili kudhibiti kupoteza Kwa Fedha za umma.

Kwa kuongezea Kwa Sasa mtu binafsi anaruhusiwa kukopa mwenye umri wa Hadi miaka 45 kinyume na swali ambapo mikopo ilitolewa Kwa makundi rika na lengwa yakiwa kwenye Vikundi na umri usiozidi miaka 35.

Makundi yanayolengwa kuoatiwa mikopo hii ni Vijana,wanawake na wenye ulemavu.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo, akizungumza katika mkutano wa hadhara unaoendelea kwenye viwanja vya Mji Mwema wilayani Kigamboni , ameweka wazi kuwa hali ya usalama wilayani humo ni shwari, na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kwa utulivu.

Katika hotuba yake ya kutoa salamu za wilaya hiyo, amewatangazia rasmi wananchi kuwa mikopo inayotokana na mapato ya ndani ya halmashauri maarufu kama mikopo ya asilimia 10, ambayo imelenga kuwanufaisha wanawake, vijana, na wenye ulemavu.

Mkuu huyo wa wilaya ameeleza pia kuwa, wananchi ikiwemo vijana wamefurahishwa na taarifa hiyo hususan maboresho ya sifa za kupata mkopo.

My Take
Ni hatua nzuri ila shida inakuja pale ambapo Waliopewa mikopo Huwa wanatumika kama mtaji wa kisiasa ambapo siku ya kupewa inakuwa sherehe ya Maonesho Kwa waliopata.

Hiyo haikai sawa,napo paboreshwe.,Vijana msio na mtaji Changamkieni pesa ndio hizo hapo.

View: https://www.instagram.com/p/DAyx01hNf1x/?igsh=MWZhbzdneTV5Njd2YQ==
 
vingetengenezwa vyama vya ushirika vya mikopo ambavyo vingetumika kukopesha wahitaji ambavyo majina yangetoka kwa mwenyekiti wa mtaa/kijiji kwenda kwa mtendaji

baada ya hapo majina yaende chama cha ushirika cha mikopo na watoa taaarifa,kwenye serikali kila robo mwaka

hawa watu wasajiliwe kwenye mfumo wa mikopo ambao utaunganishwa na namba ya nida na namba ya simu
 
Mchakato wa Benki ya ushirika umeanza na mtaji wa kuanzia Bilioni 5 umeshapatiwa.
 
vingetengenezwa vyama vya ushirika vya kutoa mchango vingetumika kukopesha wahitaji majina yangetoka kwa mwenyekiti wa mtaa/kijiji kwenda kwa mtendaji.

baada ya hapo majina yaende chama cha ushirika cha mikopo na watoa taaarifa,kwenye serikali kila robo mwaka

hawa watu wasajiliwe kwenye mfumo wa mikopo ambao utaunganishwa na namba ya namba na namba ya simu
Hilo lilimnufaisha mwenyekiti wa mtaa fulani hadi akawa anajinadi kuwa yeye ndiye Rais wa mtaa
 
Attachments

  • Screenshot_2024-10-06-19-12-22-32.jpg
    Screenshot_2024-10-06-19-12-22-32.jpg
    223.7 KB · Views: 19
Uchaguzi unapokaribia mambo yanakuwa laini kama kumsukuma mlevi vile,hata wazurulaji na wapika gongo huwakuti gerezani wanasamehewa dhambi zao.
Bila kusahau ujenzi wa barabara mbalimbali kuendelea kwa kasi ya ajabu.
Vifusi vinatolewa na kuwekwa kila kukicha, huku wachina wakipishana kukagua maendeleo ya ujenzi.
 
Makundi maalumu kwa maana ya aina ya watu wanaostahili kuangaliwa Kwa jicho la huruma kutoka serikalini na ndani ya jamii..

Mtu mwenye 40+ naye ni kundi maalumu?

Wangeweka tu watu wote wawe wanufaika as long as ni raia halali wa Tanzania...
 
vingetengenezwa vyama vya ushirika vya mikopo ambavyo vingetumika kukopesha wahitaji ambavyo majina yangetoka kwa mwenyekiti wa mtaa/kijiji kwenda kwa mtendaji

baada ya hapo majina yaende chama cha ushirika cha mikopo na watoa taaarifa,kwenye serikali kila robo mwaka

hawa watu wasajiliwe kwenye mfumo wa mikopo ambao utaunganishwa na namba ya nida na namba ya simu
Ndo ipo hivyo mkuu, wanajisajili Kwa kutumia namba ya nida, kwahyo kama ulishakopa na hujamalza kulipa huwezi kopa tena
 
Shabaha kubwa ya mikopo hii ni kuwanufaisha Wanawake chini ya mwamvuli wa vijana.

Sheria imeigawa hiyo 10% ya own source kuwanufaisha wanawake wote wanaoitwa wanawake kwa 4%
Vijana 4% (wakiwemo wanawake tena)

2% walemavu (wakiwemo wanawake tena)

Nafasi za vijana wanaume zipo too limited.

Kijana mdada, ana nafasi ya kuvushwa kimaisha kwa kuolewa kama shortcut.

Lakini yule mwingine hana namna.
 
Makundi maalumu kwa maana ya aina ya watu wanaostahili kuangaliwa Kwa jicho la huruma kutoka serikalini na ndani ya jamii..

Mtu mwenye 40+ naye ni kundi maalumu?

Wangeweka tu watu wote wawe wanufaika as long as ni raia halali wa Tanzania...
🤣🤣🤣 fanya kaz bdo unamiaka 25 ya kuish uspendee mteremko
 
Back
Top Bottom