Serikali ya Rais Samia Yarejesha rasmi mikopo ya asilimia 10 baada ya Vigezo kuboreshwa.Mtu Binafsi wa Hadi Miaka 30 Atapewa Mkopo

Serikali ya Rais Samia Yarejesha rasmi mikopo ya asilimia 10 baada ya Vigezo kuboreshwa.Mtu Binafsi wa Hadi Miaka 30 Atapewa Mkopo

Serikali imerejesha rasmi utaratibu wa Mikopo isiyo na riba ambayo ilikuwa inatolewa Kwa makundi maalumu kwa lengo la kuwainua Kiuchumi.

Awali mikopo ilisitishwa baada ya maafisa wa Serikali kutumia mwaya huo kukopesha Vikundi hewa na kisha kukwapua pesa za Umma hukunwalengwa wakishindwa kufikiwa.

Kwa Sasa vigezo vimeboreshwa na kuwa na mfumo rasmi wa utambuzi na ufuatiliaji Ili kudhibiti kupoteza Kwa Fedha za umma.

Kwa kuongezea Kwa Sasa mtu binafsi anaruhusiwa kukopa mwenye umri wa Hadi miaka 45 kinyume na swali ambapo mikopo ilitolewa Kwa makundi rika na lengwa yakiwa kwenye Vikundi na umri usiozidi miaka 35.

Makundi yanayolengwa kuoatiwa mikopo hii ni Vijana,wanawake na wenye ulemavu.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo, akizungumza katika mkutano wa hadhara unaoendelea kwenye viwanja vya Mji Mwema wilayani Kigamboni , ameweka wazi kuwa hali ya usalama wilayani humo ni shwari, na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kwa utulivu.

Katika hotuba yake ya kutoa salamu za wilaya hiyo, amewatangazia rasmi wananchi kuwa mikopo inayotokana na mapato ya ndani ya halmashauri maarufu kama mikopo ya asilimia 10, ambayo imelenga kuwanufaisha wanawake, vijana, na wenye ulemavu.

Mkuu huyo wa wilaya ameeleza pia kuwa, wananchi ikiwemo vijana wamefurahishwa na taarifa hiyo hususan maboresho ya sifa za kupata mkopo.

My Take
Ni hatua nzuri ila shida inakuja pale ambapo Waliopewa mikopo Huwa wanatumika kama mtaji wa kisiasa ambapo siku ya kupewa inakuwa sherehe ya Maonesho Kwa waliopata.

Hiyo haikai sawa,napo paboreshwe.,Vijana msio na mtaji Changamkieni pesa ndio hizo hapo.

View: https://www.instagram.com/p/DAyx01hNf1x/?igsh=MWZhbzdneTV5Njd2YQ==

HESLB au
 
Hii mikopo mara nyingi wakopaji hawarudishi marejesho japokuwa haina riba

ipo kisiasa sana
 
Kuna jamaa mwaka jana waliunda kikundi wakapewa huo mkopo baadae wakaja kuzulumiana sijui kivipi
 
Back
Top Bottom