Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Itakumbukwa Mbowe alikamatwa Mwanza na kufunguliwa kesi ya uchochezi na uhaini na kukaa rumande kwa miezi nane (8). Kesi ya awali ilisikilizwa na Jaji Siyani ambaye baada ya kumkuta Mbowe ana kesi ya kujibu alipandishwa cheo na kuwa Jaji Kiongozi. Cheo hiki kilikuwa shukrani ya serikali ya Samia kwa Jaji Siyani.
Kilichofuata ni Rais Samia kuwaita Ikulu Mufti wa Tanzania Abubakar Zuberi, Askofu Shoo na Askofu Bagonza na kuwaelekeza wakamshawishi Mbowe akubali kuridhia masharti ya serikali ili aweze kufutiwa mashtaka yake. Mbowe alikubali masharti hayo baada ya kushawishiwa na viongozi hao wa dini na kesho yake Mbowe alifutiwa kesi na kuachiwa huru na moja kwa moja akaenda Ikulu kuonana na Samia ili kukamilisha masharti ya maridhiano.
Mlolongo wa matukio haya unaonyesha jinsi serikali inavyoingilia mahakama na pia kutoa rushwa ya mazingira kwa wote wanaokubaliana na serikali.
Tukio la kwanza ni kukamatwa kwa Mbowe na kibambikiwa kesi ya uchochezi na uhaini. Ni wazi kitendo hiki kililenga kumnyamazisha Mbowe na serikali ilifanikiwa.
Pili kitendo cha Jaji Siyani kumkuta Mbowe ana kesi ya kujibu kilimfurahisha sana Rais Samia na kumzawadia Jaji Siyani kuwa Jaji Kiongozi. Hii ni rushwa ya mazingira!
Tatu kitendo cha serikali kutoendelea na kesi ya uongo ambayo iliianzisha yenyewe na kumwachia huru Mbowe ni rushwa ya mazingira. Ni wazi Mbowe alikubali masharti ya serikali baada ya kusota gerezani kwa miezi nane (8)!
Nne kitendo cha Mbowe kuanza kumsifia Samia kinyume na msimamo wake wa awali kabla ya kusota gerezani inaonyesha ni moja ya maridhiano baina ya Samia na Mbowe.
Mbowe hakuishia kumsifia Samia tu bali alishawishi uongozi wa BAWACHA kumwalika Samia katika mkutano wao uliofanyika Moshi na kumkabidhi tunzo. Kitendo hiki kiliizika kabisa dhamira ya Chadema kuendeleza mapambano ya kudai Katiba Mpya ambayo ingezaa Tume huru ya Uchaguzi.
Samia amekwisha ipiga bao Chadema na kama Mbowe atachaguliwa kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Taifa ni wazi mbinu za mapambano dhidi ya serikali ya CCM zitadhoofika sana.
Kuinusuru Chadema ibaki na hadhi yake ya awali kama Chama Kikuu cha Upinzani nchini ni kubadilisha uongozi wa juu kwa kumuondoa Mbowe!