PreGE2025 Serikali ya Samia yazidi kuanikwa dunia nzima-Maria Sarungi atoa presentation kali kuieleza dunia yanayojiri Tanzania

PreGE2025 Serikali ya Samia yazidi kuanikwa dunia nzima-Maria Sarungi atoa presentation kali kuieleza dunia yanayojiri Tanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Nimemsikiliza na kumwangalia kwa makini, kumbe taifa lina watu wazuri kiasi hiki wakati kina jerry mulo, msukuma na wale vilaza kule bungeni wanatamba...

Ukiwasikiliza wanasiasa wetu wengi walivyo mbumbumbu unaweza dhani ndivyo watanzania wote tulivyo kiakili kumbe watu makini wapo nje ya mfumo wa utawala wetu.

Hongera sana Maria
Mfumo wetu unataka watu vilaza hili iwe easily to be controlled
 
Point yangu ni kwamba hayo alioongea hayana effects yoyote kwa nchi, wamemsikiliza na yameishia hapo hapo.
Mkuu, umethibitisha nukta ya jamaa kwamba hakika huelewi dunia inavyoenda.

Ni kheri kukiri udhaifu, hapo utasaidika kuliko kukaza shingo na kubaki na ujinga wako milele.

Soma hapa chini kuna jibu lako (refer kilichowatokea Venezuela wenye hazina kuu ya mafuta duniani lakini nchi ni hoi bin fukara)!!!

Mashirika kama Freedom House, Amnesty International, na Human Rights Watch watapata hizi habari lazima.. hii inaweza kupelekea kuchafua taswira ya Tanzania kimataifa, hasa ikiwa hizo tuhuma hazijakanushwa kwa hoja zenye mashiko pia kuathiri uwekezaji wa nje kutoka kwa nchi zinazothamini demokrasia na haki.

Hivi huelewi kwamba kutokuwepo kwa utulivu wa kisiasa katika nchi yoyote ni moja ya sababu kuu zinazowafanya wawekezaji kusita kuwekeza. Hii ni kanuni inayokubalika katika uchumi wa kimataifa... yaani wewe leo ni bilionea unaweza kwenda kufungua kiwanda cha gharama DRC, Somalia ama Sudan?

Hata kama nchi ina rasilimali nyingi, wawekezaji watakwepa au watawekeza kwa masharti magumu, ambayo hayawanufaishi raia wa kawaida.

Na jinsi tulivyo omba omba hii inakwenda kuwa shida, hutoona matokeo haraka lakini utakuja kukiri...
 
Ukiskiiiia kupigwa kwe ye mshono ndo huuuku...yaani kagusaaaaaaaaa penyewe.

Yeees..
 
Andikeni kwa maandishi basi hizo nondo za shangazi na sisi tusome hatuna hela ya bando la u tyubu maisha magumu mnoo
 
Huyu sasa ndio angeweza kuwa raisi wa Tanzania sio kifutu muuaji.
Kwahiyo mtu akishaongea hivyo kwako anafaa kua rais.Unatakiwa ujue kuongea ni rahisi sana kuliko kuongoza.Tena kuongea kwa kushutumu ni rahisi zaidi kuliko kutenda.
 
Kwahiyo mtu akishaongea hivyo kwako anafaa kua rais.Unatakiwa ujue kuongea ni rahisi sana kuliko kuongoza.Tena kuongea kwa kushutumu ni rahisi zaidi kuliko kutenda.
Tunaangalia uwezo wa mtu
 
Aisee mambo yanazidi kubamba, Kitanzi kinazidi kukaza, na hali imekuwa si hali tena, kiufupi hamkani si shwari tena.

Huku wajinga wakiamini kuwa kwa kuteka na kupoteza watu sauti ya kudai haki na mabadiliko ya msingi itanyamazishwa, lakini ukweli na haki siku zote huwa havipendwi kupuuzwapuuzwa.

Shangazi Maria leo amewasimamisha wafadhili na wapenda haki duniani kwa kutoa presentation moja kali sana.

Aisee usiogope mwenye msuli mnene bali ogopa mwenye akili kubwa.

Shangazi kapiga, katandika kwelikweli. Kapukutisha sifa na credentials zote za wapenda vyeo. Sijui Bi mkubwa akienda huko nje atajisikiaje maana wenyeji watakuwa wanamg'ong'a pindi akizingumzia 4R au democracy. Maana alichokifanya Maria huko ni counter attack moja kali sana kwenye credentials za mtu fulani.

Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa uone shangazi alivyokinukisha kwa medani za kifield marshall.

Tumeshawaambia hawa wakubwa hapa nchini, kuwa bila kuleta mabadiliko ya msingi hapa nchini ni kujitoa ufahamu kama Ceasescu wa Romania, alisubiri wanaompinga wawe wengi zaidi, kilichotokea baada ya hapo the rest is history.

Tunataka mabadiliko nchini, la sivyo hii nchi itastuck, mbele haitokwenda, nyuma haitorudi


View: https://youtu.be/8lNHdfF15tk?si=eP21aiSnKrIYNrYu

Ni bora isee Tanzania si salama
 
Back
Top Bottom