Zegreaty
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 2,504
- 3,188
Kama babu Tale yupo FA yupo Msukuma yupo na wale wazenji wa jana shida iko wpaiUnafikiri bungeni unaenda tu!?
Kama babu Tale yupo FA yupo Msukuma yupo na wale wazenji wa jana shida iko wpaiUnafikiri bungeni unaenda tu!?
Home and away, au siyo?Mechi lazima ichezwe nje na ndani ya uwanja. Hapo ndo ushindi utapatikana.
Humu jukwaani ni sehemu yao ya kutamba, huko mtaani lazima mikia irudi matumboni mbele ya virungu visivyo na macho vya mapolisi.Mna makelele nyie watu, ila Vitendo ziro.
Kwa lugha nyingine wao ndio wenye ajenda sasa.Pana kitu inaitwa nature instinct yaani nguvu ya ndani Pana watu wapo hivyo wapo tayari kufa kutetea wengine.
We ukiogopa kifo kwao kifo ni njia au daraja kuelekea dimensions ingine tu.
Mfano mtu kama T Lisu Kwan ccm wanashindwa kumpa bilioni zozote atakazo ili asiwasumbue mezani.
Hawa watu kwao pesa fedha utajiri havina thamani thamani kwao ni kuona haki inatendeka.
Ndo kina Mandela,Che Guevara, Lumumba,Traore yaani huwezi wabadailisha.
Wanaitwa God messenger wapo dunia nzima hawanunuliki na pesa
You're not serious.Maria ameongea vizuri sana ila kitu kimoja alichokosea mno ni kuongea kwa sauti (voice, tone) ya hasira, chuki, ghadhabu, kisasi, mashtaka na dukuduku, hiyo staili hufanya anaekusikiliza hasa wazungu kuelewa kwamba you have an inside agenda beside giving out information about what has happened. She needs to learn public speaking skills and become the best politician in the future. I believe she can make a better person to fight the system from inside and not from outside, huko nje anapoteza nguvu nyingi mno and nobody listens, she needs to be part of the government now so that Tanzania can benefit from her courage, confidence, knowledge and patriotism.
My take: next time someone should teach Maria how to speak in big conferences without attaching her emotions and grievances to the tone, the best teacher for her for me is Mbowe, yaani unaweza kumkaba Mbowe shingo na ataongea kwa staha points kali na utamuachia tu.
Huyu Maria ni hazina ya taifa , japo anatakiwa kuanza haraka masomo ya anger management. Maria Sasa ameiva na anafaa kuingia ndani akapambane na ufisadi wa pesa za kujenga madaraja na shule, huyu inafaa aanze na ukuu wa wilaya kwanza, kuna mambo huwezi kujua kwanini yapo hivyo hadi uingie ndani, mfano unaweza kuona baba yako hapigi pamba kumbe hela yake ya kupiga pamba ndo wewe unakula na kulipiwa ada,
Mama Sa100 naomba huyu Binti umpe japo ukuu wa wilaya au mwenyekiti wa kamati mpya ya kuhakikisha ujenzi wa reli ya SGR unakwenda kwa kasi na kumalizika kabla ya muda maana uchumi utapaa tukibeba mizigo ya nchi jirani na kubeba abiria na tozo zishuke tumechoka na reli ikifika Mwanza na Kigoma tutaanza utalii mpya wa kupokea Waafrika wanaokuja tz kushangaa SGR ndefu zaidi Africa , washamba watakuja kibao kwa makundi kila siku!! Mama Samia huu mradi wa SGR ndio legacy yako pekee tafadhali naomba mengine achana nayo watafanya wengine.
Binti akiwa Mkuu wa wilaya akapambane huko na tamisemi huku akikua taratibu kisiasa, for now she is unused golden asset for the country. Ila Maria pia nae atulie basi akubali kusaidia nchi akiwa ndani ya system, apunguze ukali na misimamo, ukiwa huko nje ya system huwezi kujua moto ulioko ndani na mapungufu yaliyoko.
Aisee mambo yanazidi kubamba, Kitanzi kinazidi kukaza, na hali imekuwa si hali tena, kiufupi hamkani si shwari tena.
Huku wajinga wakiamini kuwa kwa kuteka na kupoteza watu sauti ya kudai haki na mabadiliko ya msingi itanyamazishwa, lakini ukweli na haki siku zote huwa havipendwi kupuuzwapuuzwa.
Shangazi Maria leo amewasimamisha wafadhili na wapenda haki duniani kwa kutoa presentation moja kali sana.
Aisee usiogope mwenye msuli mnene bali ogopa mwenye akili kubwa.
Shangazi kapiga, katandika kwelikweli. Kapukutisha sifa na credentials zote za wapenda vyeo. Sijui Bi mkubwa akienda huko nje atajisikiaje maana wenyeji watakuwa wanamg'ong'a pindi akizingumzia 4R au democracy. Maana alichokifanya Maria huko ni counter attack moja kali sana kwenye credentials za mtu fulani.
Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa uone shangazi alivyokinukisha kwa medani za kifield marshall.
Tumeshawaambia hawa wakubwa hapa nchini, kuwa bila kuleta mabadiliko ya msingi hapa nchini ni kujitoa ufahamu kama Ceasescu wa Romania, alisubiri wanaompinga wawe wengi zaidi, kilichotokea baada ya hapo the rest is history.
Tunataka mabadiliko nchini, la sivyo hii nchi itastuck, mbele haitokwenda, nyuma haitorudi
View: https://youtu.be/8lNHdfF15tk?si=eP21aiSnKrIYNrYu
yani ameweza kwa kweliUmeona shangazi alivyotandika mtu huko mkutanoni?
Yaani kachapa, kachapa kwelikweli
Forget about the money for a sec.Huyo dada, Mwangi, Mama Karua , yule mwandishi aliyekimbia wakati JPM anaingia ikulu, wote hao lao ni moja.
Huu ni msimu wao wa kuchuma pesa za wafadhili, hii mikutano ni mojawapo tu ya namna za upataji wa pesa za kina Soros na wengine wenye harufu za kibeberu.
Unahisi hao anaoongea nao watafanya nini?Mnajipa moyo..
Kwa sababu ya kingereza chake?. Hao wanazeeka na machungu yao hawana jipya lenye kuweza kulifikisha pazuri Tanzania.Forget about the money for a sec.
Ujumbe umeusikiliza?
Huo ujumbe tuseme ndio mbunge wetu fulani angeuwasilisha pale mjengoni Idodomya, dunia nzima ingezizima kwa sababu tu ya maudhui yake ya moto kuliko conc. H2S04!
Mkuu, umeshawahi kujiuliza hao watumwa walikuwa wanatekwa na kukusanywa huko maporini na akina nani?Wazungu wale wale waliyotupiga minyororo, wakatulimisha kwetu, wakatutumia kwa manufaa yao, leo bado anasimamisha nyapera atusemezee kwao. Cha kustaajabu watumwa kwa lugha ya wakombozi wanawashabikia. Usaliti.
Umenisoma kweli, mkuu?Kwa sababu ya kingereza chake?. Hao wanazeeka na machungu yao hawana jipya lenye kuweza kulifikisha pazuri Tanzania.
Mwanaharakati Maria jana kaingiza pesa kwa hiyo presentation.Umenisoma kweli, mkuu?
Nashawishika kuamini wasemacho wengi kwamba mara nyingi watu wanajibu hoja kwa hisia, bila kusoma na kuelewa kilichoandikwa.
Nilitaka kusema pengine lugha ya Inglishi imekupiga chenga, lakini nilipoangalia kumbe nimetumia Kiswahili rahisi sana kwenye maelezo yangu.
Mkuu, you're better than this!
Mashirika kama Freedom House, Amnesty International, na Human Rights Watch watapata hizi habari lazima.. hii inaweza kupelekea kuchafua taswira ya Tanzania kimataifa, hasa ikiwa hizo tuhuma hazijakanushwa kwa hoja zenye mashiko pia kuathiri uwekezaji wa nje kutoka kwa nchi zinazothamini demokrasia na haki.Unahisi hao anaoongea nao watafanya nini?
afu nmegundua chadema hawana tofaut na mwanamke, naona wanaongozwa na hisia badara ya tafakari.Humu jukwaani ni sehemu yao ya kutamba, huko mtaani lazima mikia irudi matumboni mbele ya virungu visivyo na macho vya mapolisi.