Serikali ya Tanzania: Hatuajiri walimu wa sanaa

Honorable GPA

Senior Member
Joined
Mar 31, 2019
Posts
149
Reaction score
223
Serikali ya Tanzania imesema, itawaajiri walimu wa masomo ya sanaa pale idadi ya walimu wa sayansi, hisabati, kilimo, biashara, elimu maalum na mafundi sanifu wa maabara za shule za sekondari itakaporidhisha.

Serikali imetoa majibu hayo leo jumatatu tarehe 8 juni 2020 wakati ikijibu swali la mbunge wa korogwe mjini(CCM) Mary Chatanda aliyeuliza kwa njia ya mtandao wa bunge la Tanzania na kujibiwa kwa mfumo huo.

Aidha, wakati serikali ikiendelea na mchakato wa kujaza nafasi za walimu wa sayansi, wahitimu wa masomo ya sanaa wanahimizwa kutafuta ajira katika taasisi nyingine za umma na shule binafsi.

#mwanahalisi online
 
Ubaguzi wa ajira
 
Ila hii nchi ina watu wajinga na wapumbavu sana. Bado kuna wazazi na walezi wengi wanaendelea kuwalipia ada watoto wao wasomee ualimu wa sanaa huku baadhi ya walimu wa sayansi hawajaajiriwa mwaka wa nne tangu wamalize chuo.

Kama hujui kusoma majira na nyakati utapishana na gari la mshahara kila leo.
Kuna fani ukisoma kwa mwaka mmoja tu ada laki nane ajira serikalini ni uhakika kwa zama hizi but watu hawajui.

Kama una fedha ya kuanzisha private school ni sawa ili mwanao awe mkuu wa shule au director ila kama mwenzangu na Mimi imekula kwako.
 
Kozi ipi hio ya mwaka mmoja?
 
Soma matangazo ya ajira kama manne utaijua. Hapa itakuwa nishakupa maisha free nikiitaja. Niliwashauri ndugu zangu kadhaa miaka michache imepita sasa washaajiriwa.
 
Serikali ya Tanzania imesema, itawaajiri walimu wa masomo ya sanaa pale idadi ya walimu wa sayansi, hisabati, kilimo, biashara, elimu maalum na mafundi sanifu wa maabara za shule za sekondari itakaporidhisha.

Serikali imetoa majibu hayo leo jumatatu tarehe 8 juni 2020 wakati ikijibu swali la mbunge wa korogwe mjini(CCM) Mary Chatanda aliyeuliza kwa njia ya mtandao wa bunge la Tanzania na kujibiwa kwa mfumo huo.

Aidha, wakati serikali ikiendelea na mchakato wa kujaza nafasi za walimu wa sayansi, wahitimu wa masomo ya sanaa wanahimizwa kutafuta ajira katika taasisi nyingine za umma na shule binafsi.

#mwanahalisi online
Hivi hawa vijana wetu wanaingia madeni yatokayo na mikopo ya elimu ya juu huku wakiandaliwa maisha yao ya baadaye yawe ya ovyo, kutokana na kupewa kauli kama hizi za kuwakatisha tamaa, kukataliwa ili waje kuishia krk misongo ya mawazo nini?

Hivi kwa nini serikali inashindwa kuweka uwiano mzuri ktk ajira ili wahitimu wote wa vyou wapate kuona kuwa wanathaminiwa?

Hivi kwa nini serikali imejikita ktk miradi mikubwa mingi kwa wakati mmoja, huku inashindwa kuona umuhimu wa uwekezaji wa rasilimali watu zitokanazo na wahitimu wa vyuo?

Tunapoelekea huko mbele, jibu moja tu litapatikana kutoka kwa hawa vijana wetu, nalo ni mlipuko wa hasira kutoka kwao ambao ni lazima utaambatana na kulipeleka taifa letu ktk "social unrest"
 
Ukiwa na kadi ya uvccm kazi zipo nyingi tuu hata kama ni mwana-sanaa
 
Ila na wewe angalia dunia muelekeo wake usiwe na hasira tu. Pole kwa kusoma kiswahili fasihi halafu hawakuhitaji
 
Soma matangazo ya ajira kama manne utaijua. Hapa itakuwa nishakupa maisha free nikiitaja. Niliwashauri ndugu zangu kadhaa miaka michache imepita sasa washaajiriwa.
Waambie vijana hiyo kozi nao wasomee mbona unakuwa mchoyo mchoyo sana
 
Back
Top Bottom