FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Hususan kwa watendaji, washauri wa Rais na vyombo vyetu vya intelijensia.
Nchi ndogo za magharibi ya Afrika zimeonesha jinsi Afrika inavyohitaji mabadiliko ya namna tunavyoongoza nchi na kusimamia Serikali.
Tanzania ni wakati umefika itazame uhalisia. Ya nchi hizo ndogo ni mfano mzuri sana, na tusidhani hayajafika Afrika Mashariki, yameshafika. Yanasambaa kama moto wa makumbi.
Leo tunashuhudia Kenya hata Polisi na Jeshi hawataki kuhusishwa na siasa na uongozi mbovu.
Tutakopa mpaka lini? Tutaendelea na kila kitu cha uongozi kukifanya siasa mpaka lini?
Tumeshuhudia watu kama Makonda wanaondokana na siasa za kulindana na kuingia kwenye uhalisia wa kumtumikia mwananchi. Naona mawaziri wachache sana wameliona hilo, lakini hawaonekani vilivyo na hawatumii media kuonesha dhahiri shahiri kuwa sasa siyo wakati wa siasa, ni wakati wa vitendo.
Tunataka tuone mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wakiondokana na dhanna ya kujitetea na kutetea ujinga, tunataka tuwaone wakitumikia wananchi muda wote.
Serikali iwachane kabisa na anasa za kijinga za magari ya kifahari kwa kila mkuu wa idara mpaka wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya. Hiyo ni dharau kubwa kwa wananchi wanyonge.
Kuna mengi sana ya kurekebisha na waziri wa fedha leo hii anakuja na bajeti ambayo haitekelezeki kwa jinsi fungu kubwa linavyokwenda kwenye matumiazi ya anasa. Anasa ya kwanza inayojionesha wazi wazi ni kwa Mtanzania wa kawaida, ni wakuu wote, kuaniza wa idara mpaka mawaziri kutembelea magari ya anasa ambayo ni mzigo mkubwa kwa nchi ya kimasikini.
Serikali ijirekebishe, tusifikiri sisi ni kisiwa, sisi ni nchi inayopakana na nchi nyingi Afrika. mabadiliko ya mama anayoyataka kwenye R zake nne yawekwe wazi, siyo kutangaza mabadiliko wakati naamini hata mawaziri hawaelewi ni mabadiliko yepi.
Naamini katika watendaji na idara zote za serikali waliyoelewa dhanna ya R nne ni wachache sana. Ofisi ya Rais inayohusika na habari inatakiwa itowe elimu kubwa kwa serikali na wananchi ili wote tuelewe ni kupi, kupatana, kustahamili, kubadilika na kujenga upya kuliko kusudiwa na falsafa ya R nne za mama Samia.
Ukifatilia habari za Burkina Faso kwa sasa, utaona kuwa wanaziishi R nne za mama Samia bila kuwa nazo.
Sisi tulionazo tunashindwa kuziishi.