Serikali ya Tanzania inaandaa Mpango wa Kuangamiza Wananchi Wake Maskini

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Mchawi si mpaka avae tunguli au hirizi. Utamwona tu ana ku wish nini.

Serikali ya Tanzania ina mpango dhabiti wa kuangamiza Wananchi wake kupitia kodi na tozo za kinyama, kinyonyaji na kibaradhuli.
1. Tozo ya Miamala
2. Tozo ya simu ya mshikamano (yaani maskini waendelee kushikamana katika umaskini wao
3. Tozo ya kadi za simu.
4. Kuongezeka kwa kodi ya Mafuta.

Wao hawana shaka sababu Mafuta wanalipiwana Serikali ambayo inachukua kwa kutukamua hizi kodi. Mishahara yao na Kiinua Mgongo wanapata kwa wakati na pasipo kukatwa kodi.

Watashindwa kutumiana pesa,watakosa pesa za chakula,matibabu n.k

Serikali inaangamiza watu wake.
 
Tutalipa tu kwa sababu ni kwa malengo ya maendeleo yetu ss watanzania.
 
Ukitoka hapo bado chanjo ambayo huku ulikotestiwa watu wanadedi tu
 
Wanatafuta tu njia za upigaji wakati serikalini kuna pesa ila usimamizi ni mbovu. Wakijenga vyumba saba vya madarasa utasikia wamatumia milioni mia sita kukamilisha ujenzi huo.
 
NSSF Fao la kujitoa ni uharamia bado tozo juu aiseeh Maombi ni muhimu sana....
 
Ndio tatizo la mfumo ccm na katiba mbovu tuliyonayo, watu watawaelewa CDM taratibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…